DED wa Gairo na wenzake warudisha mabati waliyoiba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale na watumishi saba wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa waliodaiwa kuiba mabati 1,172 wameyarejesha wilayani humo.

Hivi karibuni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim alieleza kuwatia mbaroni watumishi saba wa halmshauri hiyo (Kilosa) akiwemo DED huyo kabla hajahamishiwa wilayani Gairo.

Akizungumza leo Septemba 7 katika urejeshwaji wa mabati hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Majid Mwanga amewaonya watumishi wa umma watakaohusika na ubadhirifu wa mali za umma kuwa hawataachwa bali hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mwanga amesema wale watumishi waliokuwa wakihusishwa na wizi huo wa mabati wamerejesha na tayari yamepokelewa na kugaiwa kwenye shule zote zilizotakiwa kugawiwa mabati hayo kutokana na upungufu uliyokuwepo wa mabati.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Kisena Mabuba amesema kwa kuwa mabati hayo yalikuwa kwa ajili ya miradi ya serikali kwemye shule za msingi na sekondari yataezekwa kwa haraka na walimu tarari wamekabidhiwa.

Watumishi wanaodaiwa kufanya wizi huo ni maafisa ugavi wanne na madereva watatu wa halmashauri hiyo wakituhumiwa kuhusika na wizi huo wa mabati yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye stoo ya halmashauri ya Kilosa kwaajili ya kuezeka shule ya msingi Mzaganza kata ya Kidete.

Mwananchi
 
Mimi hapo sijaelewa.Inamaana walivyorudisha hayo mabati basi hakuna kesi tena?

Hilo nalo linawezekana maana tunajua % kubwa ya watu ni wezi
Yaani ni mzunguko wa wizi
Usikute hata huko shule wakaezeka ya zamani na mapya wakagawana wengine

Mzunguko wa kuiba tu kila unapoenda ni laana fulani hivi
 
Mimi hapo sijaelewa.Inamaana walivyorudisha hayo mabati basi hakuna kesi tena?
Hiyo ndio serikali ya CCM.
Unamkumbuka yule mbunge jangili aliyekua anamiliki silaha nyingi kuliko vituo vya polisi.
ALIACHIWA HURU
Unamkumbuka aliyekua mkurugenzi ws Temeke mwenye kesi ya kuhujumu uchumi kosa ambalo halina dhamana? Yuko nje kwa dhamana.
 
Hiyo ndio serikali ya CCM.
Unamkumbuka yule mbunge jangili aliyekua anamiliki silaha nyingi kuliko vituo vya polisi.
ALIACHIWA HURU
Unamkumbuka aliyekua mkurugenzi ws Temeke mwenye kesi ya kuhujumu uchumi kosa ambalo halina dhamana? Yuko nje kwa dhamana.
Mhhhhh, ngoja tuone.
 
Back
Top Bottom