DED Halmashauri ya Igunga akamatwa, siku chache baada ya kudaiwa kuwepo kwa upigaji kwenye Halmashauri aliyotoka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Athumani Francis Msabila amekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani humo na kuwekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi wilayni humo.

Mkurugenzi huyo alikamatwa Novemba 05, 2023 majira ya mchana wakati akiwa amerejea kutoka mkoani Dodoma ambako alikwenda kikazi.

Taarifa za kukamatwa kwa mkurugenzi huyo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi Richard Abwao.

”Ni kweli Mkurugenzi huyo tunamshikilia akisubiri kupelekwa mkoani Kigoma alikokuwa anafanyakazi awali kabla ya kuhamishiwa Igunga kwani ndiko ana kesi.”

Hata hivyo, Kamanda Abwao hakuweza kutaja tuhuma zinazomkabili Mkurugenzi huyo zaidi ya kusema " Tunamshikilia lakini sisi kama mkoa wa Tabora hatuna kesi naye, tunafanya utaratibu wa kumrejesha Kigoma ndiyo wana kesi naye."

Kukamatwa kwa DED huyo huenda ni matokeo ya uchunguzi wa Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambayo ilikabidhi ripoti yake Oktoba 25 mwaka huu jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa alipokea taarifa hiyo ya uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo ilibainika kuwa watu 10 wanahusika na mtandao wa uhamishaji fedha kinyume cha taratibu.

Akipokea ripoti hiyo, Waziri mkuu alisema kila mtumishi wa umma ni lazima atunze na kuratibu vizuri matumizi ya fedha ambapo aliagiza hatua za haraka za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika hao.

“Zichukuliwe hatua kwa sababu Mheshimiwa Rais anahangaika kutafuta fedha kwa ajili ya maendeleo lakini watu wachache wanazifanyia ubadhirifu” alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Source: Matukio Daima Media

Pia soma - Waziri Mchengerwa amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tabora, Athumani Msabila
 
Mbona watumishi wa hazina ambako fedha zilikokuwa zinatoka hawajakamatwa?

Wanahangaika na vidagaa tu,mafisadi papa yametulia,huko halmashauri hizo pesa zilipitishwa tu,waende hazina ziliko toka hizo pesa,halmashauri ni mbuzi wa kafara tu.

Na hii kesi itazimwa kama kesi nyinginezo,wahuni wapo kazini.
 
Wasanii hawa na mbinu zao za kila wakati
Siku wakiamua kuwakamata na kuwafunga majizi 200 ndio na kuwaambia wazitapike zote, hapo ndio ntajua Tz inakuja kuwa nchi ya kweli la sivyo haya ni maigizo tu na huyu atatoka na atatamba mtaani
 
"Zichukuliwe hatua kwa sababu Mheshimiwa Rais anahangaika kutafuta fedha kwa ajili ya maendeleo lakini watu wachache wanazifanyia ubadhirifu” alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom