DED wa Gairo na wenzake warudisha mabati waliyoiba

Kitendo cha kurudisha hayo mabati tayari ni ushahidi tosha mahakamani kuwa hao watuhumiwa wamekiri kuwa waliiba na wameiraishia kazi mahakama. Kwa hiyo kama kweli wapo huru na wanaendelea na kazi basi ni vyema kuanzia sasa wale watuhumiwa wote waliopo magerezani nchi nzima kwa kesi za wizi na wao wapewe nafasi wale wenye uwezo wa kurudisha walivyoiba warudishe ili waachiwe huru.
 
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale na watumishi saba wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa waliodaiwa kuiba mabati 1,172 wameyarejesha wilayani humo.

Hivi karibuni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim alieleza kuwatia mbaroni watumishi saba wa halmshauri hiyo (Kilosa) akiwemo DED huyo kabla hajahamishiwa wilayani Gairo.

Akizungumza leo Septemba 7 katika urejeshwaji wa mabati hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Majid Mwanga amewaonya watumishi wa umma watakaohusika na ubadhirifu wa mali za umma kuwa hawataachwa bali hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mwanga amesema wale watumishi waliokuwa wakihusishwa na wizi huo wa mabati wamerejesha na tayari yamepokelewa na kugaiwa kwenye shule zote zilizotakiwa kugawiwa mabati hayo kutokana na upungufu uliyokuwepo wa mabati.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Kisena Mabuba amesema kwa kuwa mabati hayo yalikuwa kwa ajili ya miradi ya serikali kwemye shule za msingi na sekondari yataezekwa kwa haraka na walimu tarari wamekabidhiwa.

Watumishi wanaodaiwa kufanya wizi huo ni maafisa ugavi wanne na madereva watatu wa halmashauri hiyo wakituhumiwa kuhusika na wizi huo wa mabati yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye stoo ya halmashauri ya Kilosa kwaajili ya kuezeka shule ya msingi Mzaganza kata ya Kidete.

Mwananchi
Mwizi ni mkurugenzi aliyeteuliwa na CCM, mabati yaliyoibiwa ni ya serikali ya CCM. Yamerudishwa na mkurugenzi Hana kosa tena Yuko ofisini anachapa kazi.
 
Kitendo cha kurudisha hayo mabati tayari ni ushahidi tosha mahakamani kuwa hao watuhumiwa wamekiri kuwa waliiba na wameiraishia kazi mahakama. Kwa hiyo kama kweli wapo huru na wanaendelea na kazi basi ni vyema kuanzia sasa wale watuhumiwa wote waliopo magerezani nchi nzima kwa kesi za wizi na wao wapewe nafasi wale wenye uwezo wa kurudisha walivyoiba warudishe ili waachiwe huru.
Nasubiria tu report ya ukwapuaji wa tozo kwa Sandarusi pale BOT 😂😂😂 ambavyo watu watagawana majasho ya wananchi na wakaendelea kupeta tu
 
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale na watumishi saba wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa waliodaiwa kuiba mabati 1,172 wameyarejesha wilayani humo.

Hivi karibuni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim alieleza kuwatia mbaroni watumishi saba wa halmshauri hiyo (Kilosa) akiwemo DED huyo kabla hajahamishiwa wilayani Gairo.

Akizungumza leo Septemba 7 katika urejeshwaji wa mabati hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Majid Mwanga amewaonya watumishi wa umma watakaohusika na ubadhirifu wa mali za umma kuwa hawataachwa bali hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mwanga amesema wale watumishi waliokuwa wakihusishwa na wizi huo wa mabati wamerejesha na tayari yamepokelewa na kugaiwa kwenye shule zote zilizotakiwa kugawiwa mabati hayo kutokana na upungufu uliyokuwepo wa mabati.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Kisena Mabuba amesema kwa kuwa mabati hayo yalikuwa kwa ajili ya miradi ya serikali kwemye shule za msingi na sekondari yataezekwa kwa haraka na walimu tarari wamekabidhiwa.

Watumishi wanaodaiwa kufanya wizi huo ni maafisa ugavi wanne na madereva watatu wa halmashauri hiyo wakituhumiwa kuhusika na wizi huo wa mabati yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye stoo ya halmashauri ya Kilosa kwaajili ya kuezeka shule ya msingi Mzaganza kata ya Kidete.

Mwananchi
Watu walioingia kwenye Madaraka kwa konekisheni kali ndiyo hao, hata wakichana mbeleko mamlaka zao zinashona na kuwabeba tena...ushenzi na ujinga. RIP JPM awamu hii ni ya 4 iliyojigeuza na kujiita 6
 
Back
Top Bottom