Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,448
- 16,313
UTEUZI:
Rais wa Tanzania, Dtk. Samia Suluhu Hassan amemteua Michael Kachoma kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega akichukua nafasi nafasi ya Veronica Vicent Sayore ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Rais Samia pia amemteua Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Wanging’ombe Maryam Ahmed Muhaji kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara akichukua nafasi ya Karoline Albert Mthapula ambaye atapangiwa kazi nyingine na amemteua Afisa Mwandamizi katika Mfuko wa Taifa wa Maji, Zuhura Abdulrahman Rashid kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa akichukua nafasi ya Shamim Sadiq ambaye atapangiwa kazi nyingine.
UHAMISHO:
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa Wakuu wa Wilaya sita ambapo amemuhamisha Maveka Simon Maveka kutoka Wilaya ya Chunya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa na Remidius Mwema Emmanuel amehamishwa kutoka Wilaya ya Kongwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto.
Amemuhamisha pia Mbaraka Alhaji Batenga kutoka Wilaya ya Kiteto kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya na Kanali Hamis Mayamba Maiga amehamishwa kutoka Wilaya ya Rombo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi huku Kanali Wilson Christian Sakullo akihamishwa kutoka Wilaya ya Misenyi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro na Raymond Stephen Mwangwala amehamishwa kutoka Wilaya ya Ngorongoro kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo.
Katika hatua nyingine Rais Samia amefanya uhamisho wa Wakurugenzi wa Halmashauri 15 ambapo amemuhamisha Rose Robert Manumba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Rehema Said Bwasi amehamishwa kutoka Malinyi kwenda kuwa Mkurugenzi Mendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Yefred Edson Myenzi amehamishwa kutoka Mbulu kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita akichukua nafasi ya Zahara Muhiddin Michuzi ambaye amehamishiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara.
Lena Martin Nkya amehamishwa kutoka Ifakara kwenda kuwa DED
Tunduma na Chiriku Hams Chilumba amehamishwa kutoka Namtumbo kwenda kuwa Mkurugenzi DED Kigoma, Kisena Magena Mabuba amehamishwa kutoka Kilosa kwenda kuwa DED Shinyanga akichukua nafasi ya Simon Sales Berege ambaye anakwenda kuwa DED Rufiji akichukua nafasi ya Michael John Gwimile ambaye anakwenda kuwa DED Kilosa.
Wengine ni Regina Lazaro Bieda ambaye amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Momba kwenda kuwa DED Kibaha, Mwajuma Abasy Nasombe amehamishwa kutoka Mwanga kwenda kuwa DED Moshi na Rashid Karim Gembe amehamishwa kutoka Moshi kwenda kuwa DED Mkinga.
Zahara Abdul Msangi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na Philemon Mwita Magesa amehamishwa kutoka Tunduma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo na Butamo Nuru Ndalahwa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Momba.