Declassified KGB documents: Churchill alimuua Stalin

Masamila

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
6,411
7,306
Mmoja wa wanakamati ya kudeclassify files za iliyokuwa KGB anaelezea sababu za kuuawa kwa aliyekuwa mbabe wa USSR Joseph Stalin, na udhaifu wa KGB katika Counterintelligence mpaka kiongozi wa taifa hilo kuuawa na majasusi kutoka nchi za magharibi

Mkuu umeitoa wapi hii ???
Halafu kama KGB ndiyo imefanya ku-declassify hizi nyaraka utasemaje kwamba Counter=Intelligence ya Urusi ya Kisovieti ilikuwa dhaifu, wakati walikuwa wanajua mpango wote ??? (Hapa pana ukakasi sana) Hizi nyaraka zingetolewa na MI6 ndiyo zingekuwa na uhalisia kidogo, kuna mengi yana walakini hapa.

Siwezi kukupinga sana lakini tukitumia Common Sense tutabaki na maswali mengi sana:
1. Kwanini walisubiri wamuue Joseph Stalin wakati ameshakuwa mzee na miaka 73 ??
2. Kwanini mnawasahau maadui zake wakubwa wa ndani kama Nikita Khrushchev ??
3. Kwanini hao MI6 hawakuwaua Leonid Brezhnev na Yuri Andropov ??

NB: Kama KGB walikuwa na Intelijensia kinzani dhaifu basi hujawahi kumsikia mtu anaitwa Yuri Totrov (The most ruthless spy catcher in KGB history)..CIA walimfuata kumhonga mabilioni ya pesa baada ya kuanguka Urusi ya Kisovieti ili kujua alikuwa anatumia mbinu gani kukamata CIA na MI6 wengi vile.....
 
Mkuu umeitoa wapi hii ???
Halafu kama KGB ndiyo imefanya ku-declassify hizi nyaraka utasemaje kwamba Counter=Intelligence ya Urusi ya Kisovieti ilikuwa dhaifu ??? (Hapa pana ukakasi sana)
Hizi nyaraka zingetolewa na MI6 ndiyo zingekuwa na uhalisia kidogo, kune mengi yana walakini hapa.

Siwezi kukupinga sana lakini tukutumia Common Sense tutabaki na maswali mengi sana:
1. Kwanini walisubiri wamuue Joseph Stalin wakati ameshakuwa mzee na miaka 73 ??
2. Kwanini mnawasahau maadui zake wakubwa wa ndani kama Nikita Khrushchev ??
3. Kwanini hao MI6 hawakuwaua Leonid Brezhnev na Yuri Andropov ??

NB: Kama KGB walikuwa na Intelijensia kinzani dhaifu basi hujawahi kumsikia mtu anaitwa Yuri Titrov (The most ruthless spy catcher in KGB history)..CIA walimfuata kumhonga mabilioni ya pesa baada ya kuanguka Urusi ya Kisovieti ili kujua alikuwa anatumia mbinu gani kukamata CIA na MI6 wengi vile.....

Huyo mwanakamati anasema kuwa Kumuua Stalin hao majasusi walitumia kidonge, sasa mpaka Mkuu wa nchi anauawa kirahisi hivyo we mkuu huoni huo ni udhaifu mkubwa?
 
Sikubishii kabisa mkuu kwasababu wote hapa hatuna Uhakika na Ukweli na wala hatuujui.
Lakini kama utachukua muda kufuatilia historia ya Urusi ya Kisovieti utakuja kugundua kwamba Secretary Joseph Stalin alikuwa na maaudui wengi sana sanaa ndani ya Chama cha kikomunisti (CPSU) kuliko hata nje ya nchi. Ndiyo maana hata kabla ya kufa aliwaambia kabisa vijana ndani na NKVD (KGB) kwamba wajiandae maana yeye akifa watapata sana shida.

Baada ya Joseph Stalin kufa wafuasia wake waliuawa na kuteswa sana kwenye kampeni ya Nikita Khrushchev ya De-Stalinazation of the Soviet Union. Hili tu linadhihirisha kwamba Joseph Stalin alikuwa na maadui wengi sana nchini Urusi.
Au upande wa pili tukubali kwamba kweli Sir Winston Churchill alimuu Secretary Joseph Stalin, unadhani angeweza kufanya hivyo bila msaada wa NKVD (KGB) ???

NB 1: Maraisi wote watatu wa mwanzo wa Urusi ya Kisovieti walifanyiwa majaribio ya kuuwawa na Warusi wenyewe.
1. Vladmir Illych Ulyanov Lenin alipigwa risasi na mwanamke wa Kirusi mwenye asili ya Kiyahudi.
2. Joseph Stalin alinusurika mara nyingi sana kuuawawa na ndiyo maana alikuwa haamini mtu kabisa.
3. Nikita Khrushchev alipinduliwa na KGB na wakamweka Leonid Brezhnev...

NB 2: Usisahau kwamba kuanzia miaka ya 45-53 Joseph Stalin alikuwa na Ugomvi mkubwa sana na Josip Broz Tito wa Yugoslavia hadi wakatishiana kuuana na kutumiana majasusi. Hili nalo usilisahau kabisa......
 
Mkuu umeitoa wapi hii ???
Halafu kama KGB ndiyo imefanya ku-declassify hizi nyaraka utasemaje kwamba Counter=Intelligence ya Urusi ya Kisovieti ilikuwa dhaifu ??? (Hapa pana ukakasi sana)
Hizi nyaraka zingetolewa na MI6 ndiyo zingekuwa na uhalisia kidogo, kune mengi yana walakini hapa.

Siwezi kukupinga sana lakini tukutumia Common Sense tutabaki na maswali mengi sana:
1. Kwanini walisubiri wamuue Joseph Stalin wakati ameshakuwa mzee na miaka 73 ??
2. Kwanini mnawasahau maadui zake wakubwa wa ndani kama Nikita Khrushchev ??
3. Kwanini hao MI6 hawakuwaua Leonid Brezhnev na Yuri Andropov ??

NB: Kama KGB walikuwa na Intelijensia kinzani dhaifu basi hujawahi kumsikia mtu anaitwa Yuri Titrov (The most ruthless spy catcher in KGB history)..CIA walimfuata kumhonga mabilioni ya pesa baada ya kuanguka Urusi ya Kisovieti ili kujua alikuwa anatumia mbinu gani kukamata CIA na MI6 wengi vile.....
Sio Yuri droZdov mkuu
 
Sio Yuri droZdov mkuu

Achana na General Yuri Drozdov wa Illegals Program.
Huyu alikuwa ni Counter Intelligence Officer based in Japan.
Yaani yeye alikuwa ni msomi wa Chuo Kikuu na alikamata sana majasusi wa CIA na MI6 kwa wingi.

NATO walichanganyikiwa sana wakawa wanahisi labda kuna watu wanatoa siri za CIA na MI6; kumbe jamaa katembelea nchi zote za Warsaw Pact na zile za Kikomunisti duniani akafanya utafiti mkubwa kuhusu tabia za kipekee (Peculiar Human Behavior) za majasusi wa CIA na MI6 na akatengeneza Bango-Kitita (Matrix) kubwa kweli akawapelekea KGB.

Hivyo mle ndani kukawa na somo kabisa wanafundishwa majasusi wa KGB-Counter Intelligence kuhusu CIA behaviour. Wanakwambia zaidi ya asilimia 85% ya tabia zilizoorodheshwa mle zilikuwa ni za majasusi wa CIA na MI6. Baada ya kuanguka Urusi ya kisovieti CIA walimfuata awaeleze alitumia mbinu gani kuwakamata wengi vile. Baadae wakaja kuambiwa ni kutumia Peni, Karatasi na kuangalia kwa jicho la tatu tu......!

NB 1: Tafuta kitabu cha Oxford kinaitwa "Near and distant neighbours: A new history of soviet Intelligence (The Extraordinary achievements of Yuri Totrov Page 251 na Page 252)" kimeandikwa na Jonathan Haslam. Sasa huwa najiuliza sana maswali kama: Hivi miaka ya 70's na 80's KGB walikuwa wanafanya hivi unategemea leo ndiyo nchi yenu inakutana na majasusi wa namna hii hivi kuna kupona kweli ???

NB 2: Yuri Totrov ni uthibitisho tosha kwamba hakuna silaha kubwa duniani kama Ubongo wa mwanadamu, pia hakuna kitu chenye nguvu kama Human Intelligence. Aliweza kufanya ujasusi kwa kutumia COMMON SENSE na kuweza kushindana na CIA ambayo ilikuwa iko mbele sana kwenye swala la teknolojia na fedha.

Watanzania tuna nini cha kujifunza hapa ???
Tunaweza tusiwe na pesa nyingi na teknolojia kubwa sana lakini tukafanikiwa kwa kiasi kikubwa mno katika kulinda maslahi mapana ya nchi. Japo ni kweli kwa dunia ya sasa tunahitaji pesa na teknolojia lakini hili halitakiwi kutufanya tulemae na kutegemea kuomba msaada wa taarifa au kununua vyombo vya kijasusi kutoka nchi za nje: Ni hatari sana kwetu.......

NB: Ukitaka hiki kitabu kinachomzungumzia Yuri Totrov utakipata kwenye bandiko namba [HASHTAG]#120[/HASHTAG], tunamshukuru sana Mkuu Palantir kwa kufanya jitihada za ziada kututafutia nakala yake (Softcopy) ili wengi wakisome.
 
Mkuu umeitoa wapi hii ???
Halafu kama KGB ndiyo imefanya ku-declassify hizi nyaraka utasemaje kwamba Counter=Intelligence ya Urusi ya Kisovieti ilikuwa dhaifu ??? (Hapa pana ukakasi sana)
Hizi nyaraka zingetolewa na MI6 ndiyo zingekuwa na uhalisia kidogo, kune mengi yana walakini hapa.

Siwezi kukupinga sana lakini tukutumia Common Sense tutabaki na maswali mengi sana:
1. Kwanini walisubiri wamuue Joseph Stalin wakati ameshakuwa mzee na miaka 73 ??
2. Kwanini mnawasahau maadui zake wakubwa wa ndani kama Nikita Khrushchev ??
3. Kwanini hao MI6 hawakuwaua Leonid Brezhnev na Yuri Andropov ??

NB: Kama KGB walikuwa na Intelijensia kinzani dhaifu basi hujawahi kumsikia mtu anaitwa Yuri Titrov (The most ruthless spy catcher in KGB history)..CIA walimfuata kumhonga mabilioni ya pesa baada ya kuanguka Urusi ya Kisovieti ili kujua alikuwa anatumia mbinu gani kukamata CIA na MI6 wengi vile.....

Heshima yako mkuu, naamini mkuu wewe kama mimi ni wafuatiliaji wazuri wa history. Na kama unakumbuka vizuri huyo Leonid Brezhnev hakuwa solid leader kama Stalin.

Yeye(Brezhnev) na Khrushev ni viongozi wa USSR waliokuwa waoga kweli kweli pamona na mwenzao Gorbachev.

Katika History, kiongozi wa USSR aliekuwa anaogopwa na US kupita maelezo ni Joseph Stalin. Alikuwa ni mtu pengine unaweza dhani ni wa ovyo katika vitendo, kama pia una kumbukumbu nzuri Chairman Mao kabla hajafa, alisema kuwa kiongozi aliemheshime pekee USSR ni Stalin pekee.

Chini ya uongozi wa Stalin tulishuhudia Marubani wa USSR red army wakiwa pamoja na marubani wa Chinese red army jointly wakiwa vitani na wanajeshi wa Marekani walioongozwa na General Douglas McArthur (kama sijasahau jina la General).

Baada ya hapo sidhani kama USSR red army wamewahi engage in battlefield na US/Allied directly/live. Viongozi waliofatia baada ya Stalin wote walikuwa waoga
 
Heshima yako mkuu, naamini mkuu wewe kama mimi ni wafuatiliaji wazuri wa history. Na kama unakumbuka vizuri huyo Leonid Brezhnev hakuwa solid leader kama Stalin.
Yeye(Brezhnev) na Khrushev ni viongozi wa USSR waliokuwa waoga kweli kweli pamona na mwenzao Gorbachev.

Mkuu umemsoma vizuri Leonid Brezhnev ???
Kama ungemsoma vizuri usingemfananisha kabisa na akina Gorbachev au Khrushchev.
Kama kuua Wakomunisti wote walikuwa wanauwana sana bila woga wowote ule, Vladmir Lenin aliua sana watu kama Joseph Stalin kipindi kile cha The Civil War na Red Terror. Yuri Andropov alipokuwa kiongozi wa nchi ndiyo alikuwa anajiandaa kabisa kupigana vita ya Kinyuklia na USA, Konstantin Chernenko alipokuwa kiongozi wa nchi naye akaja na yele yale ya wakina Brezhnev..Pitia vizuri mkuu utaona.

Mikhail Gorbachev pekee ndiye alikuwa mlaini na alikuwa mwoga sana,
Alitaka kuwabadilisha Wasovieti na kuwafurahisha wazungu wakati huo huo.

NB: Kinachomtofautisha Joseph Stalin na viongozi wengine wa Urusi ni kwamba yeye ndiye aliyeifanya Urusi ya Kisovieti iwe ndiyo nchi yengu nguvu sana kijeshi baada ya Vita ya dunia ( He was a political, Scientific and Military Reformer). He understood the setbacks of International Communism and he concentrated much energy in modernizing Russia at the threshold no other Soviet Leader did....!
 
Achana na Genereal Yuri Drozdov wa Illegal Program.
Huyu alikuwa ni Counter Intelligence Officer based in Japan.
Yaani yeye alikuwa ni msomi wa Chuo Kikuu na alikamata sana majasusi wa CIA na MI6 kwa wingi.
NATO walichanganyikiwa sana wakawa wanahisi labda kuna watu wanatoa siri za CIA na MI6; kumbe jamaa katembelea nchi zote za Warsaw Pact na zile za Kikomunisti duniani akafanya utafiti mkubwa kuhusu tabia za kipekee (Peculiara Human Behavior) za majasusi wa CIA na MI6 na akatengeneza Bango-Kitita (Matrix) kubwa kweli akawapelekea KGB.

Hivyo mle ndani kukawa na somo kabisa wanafundishwa majasusi wa KGB-Counter Intelligence kuhusu CIA behaviour. Wanakwambia zaidi ya asilimia 85% ya tabia zilizoorodheshwa mle zilikuwa ni za majasusi wa CIA na MI6. Baada ya kuanguka Urusi ya kisovieti CIA walimfuata awaeleze alitumia mbinu gani kuwakamata wengi vile. Baadae wakaja kuambiwa ni kutumia Peni, Karatasi na kuangalia kwa jicho la tatu tu......!

NB 1: Tafuta kitabu cha Oxford kinaitwa "Near and distant neighbours: A new history of soviet Intelligence (The Extraordinary achievements of Yuri Totrov Page 251 na Page 252)" kimeandikwa na Jonathan Haslam. Sasa huwa najiuliza sana maswali kama: Hivi miaka ya 70's na 80's KGB walikuwa wanafanya hivi unategemea leo ndiyo nchi yenu inakutana na majasusi wa namna hii hivi kuna kupona kweli ???

NB 2: Yuri Totrov ni uthibitisho tosha kwamba hakuna silaha kubwa duniani kama Ubongo wa mwanadamu, pia hakuna kitu chenye nguvu kama Human Intelligence. Aliweza kufanya ujasusi kwa kutumia COMMON SENSE na kuweza kushindana na CIA ambayo ilikuwa iko mbele sana kwenye swala la teknolojia na fedha.

Watanzania tuna nini cha kujifunza hapa ???
Tunaweza tusiwe na pesa nyingi na teknolojia kubwa sana lakini tukafanikiwa kwa kiasi kikubwa mno katika kulinda maslahi mapana ya nchi. Japo ni kweli kwa dunia ya sasa tunahitaji pesa na teknolojia lakini hili halitakiwi kutufanya tulemae na kutegemea kuomba msaada wa taarifa au kununua vyombo vya kijasusi kutoka nchi za nje: Ni hatari sana kwetu.......

CC: Consigliere, Red Giant , zitto junior , chige , mng'ato
Nimekusoma sana mkuu na ni elimu pana mnooo
I owe u
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom