Double agents, double impacts

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
2,991
9,332
Majasusi ambao wanakuwa ni double agent wanakuwa changamoto sana kwa idara nyingi za usalama duniani ingawaje wanatumiwa sana mpaka sasa. Wengi wao hujifanya kuifanyia kazi kitengo Cha nchi yake ila kiuhalisia huifanyia kazi kitengo au vitengo vya nje ya nchi yake.

Richard helms ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa shirika la CIA kati ya mwaka 1973 Hadi 1976, aliwahi kukiri mbele ya bunge la congress kwamba kumjua jasusi ambaye ni double agent ni Moja kati ya kazi ngumu na imekaa kimtego sana . Na vilevile akaenda mbali zaidi kwa kusema kwamba double agents wengi hugundulika muda umeeenda huku akiacha damage ya kutosha kwenye idara. Mashirika mengi ya kijasusi duniani huathiriwa muda mwingine na Hawa double agent kiasi kwamba kuhatarisha uwepo wa idara hizi.

Kipindi Cha vita baridi shirika la CIA lilipendekeza kupitishwa sheria ya wastani ya kuwaajiri Hawa majasusi ambao ni double agents kwenye nchi ambazo walizilenga ikiwemo Russia,Cuba na huko ujerumani mashariki. Uamuzi huu ulileta matokeo mazuri kwa Marekani lakini pia kulikuwa na hasara zake . Kwa mfano kwa mujibu wa wachambuzi wa intelligence, inasemekana kwamba wengi wa Hawa double agent walikuwa wanasahauliwa baada ya kutumika

. Mwisho wa siku hugeuka kuwa mole au wasaliti ambao wapo kwenye vyeo vya juu au rank ndani ya kitengo. Tokea zamani shirika la CIA lianzishwe ,hakuna kitu shirika hili lilikuwa likikiogopa kama kuwepo kwa msaliti/mole ndani yake . Na mbaya zaidi huyu mole awe ameshika wadhifa wa nafasi nyeti kitengoni. Kwa mfano miaka ya 1960s enzi za mkurugenzi James angleton shirika la CIA lilianzisha msako mkali wa wasaliti na mole waliojipenyeza ndani ya idara za usalama za marekani . Msako huu ilipelekea shirika Hilo kutikisika na pia watu wengi muhimu ndani ya shirika Hilo waliachishwa kazi na pia lilipata kashfa nyingi sana kama kushirikiana na mafia pamoja kutumika kisiasa kuficha madudu ya Richard Nixon na kashfa ya WATERGATE SCANDAL na Mambo mengine mengi machafu. Msako huu ulilenga kuwapukutisha nje mapandikizi ya Russia ndani ya marekani ambao huenda Walikuwepo au kutokuwepo kwa wakati huo. Msako huu ulipelekea wazuri kutupwa nje na moles halisi wakaachwa. Shida ndipo ilipoanzia.

Tafiti zilizokuja kufanyika baadaye kuhusiana na huu msako ulionyesha kwamba moles hawakuwa na damage impact zaidi ya wale ambao ni double agents. Kwa mfano Aldrich Ames afisa wa CIA ambaye alikuwa ni double agent akiifanyia kazi Russia hakushtukiwa mapema kwa zaidi ya miaka 10.

Na iliwahi bainika kwamba kipindi Cha vita baridi CIA waliweza kupenyeza makachero wao kwa wingi ndani ya ujerumani mashariki kipindi Cha vita baridi ,lakini hao hao waligeuka kuwa double agents na kuanza kuuza Siri za CIA kwa nchi za Soviet.

Marekani hawakuwahi jua madhara na risk ya kumtumia double agent ni kubwa kiasi gani. Kwa mfano mwaka 2009 ilitoka Repoti ambapo double agent ambaye alikuwa akiitumikia marekani na Russia aliamua kujitoa mhanga kwa kujilipua sababu hazikuwekwa wazi kuhusiana na tukio hili. Hili tukio lilitokea kwenye kambi ya kijeshi ya forward base Chapman kwenye mji wa mashariki mwa Afghanistan wa Khost. Katika tukio hili maafisa Saba wa CIA,wakandarasi pamoja na raia wawili wa kigeni waliuawa.

Markus wolf jasusi wa ujerumani pia aliwahi kuweka wazi kwamba hakuna afisa yoyote wa CIA aliyekuwa akifanya kazi huko east German kipindi hicho kuanzia 1960s hakuwa double agent. Hawa double agent walikuwa wanapewa infos ambazo zipo highly selected kwa ajili ya kuwapa CIA. Na vilevile hawa double agent walikuwa wanauza info za CIA kwa East German pasipo CIA kushtuka mapema mbali na kuwa na resources zote na za kila aina.

Madai haya ya wolf yalipata nguvu kutoka kwa aliyekuwa deputy wa shirika la CIA admiral Bobby Ray Inman miaka hiyo akiwa mbele ya kamati za bunge la congress aliwahi kusema nanukuu" Most, if not all[East German] Human intelligence agents over 20 years were double agents ". Maana yake ni kwamba majasusi wengi wa CIA waliokuwa kikazi huko ujerumani kwa namna Moja ama nyingine walikuwa wakitumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja .

Hata mkurugenzi mstaafu wa CIA miaka hiyo bwana Robert M.gates na aliyekuwa mkuu wa kitengo Cha kijasusi hususan wa German na Soviet division Milton bearden ,wote Hawa walikiri baadaye kwa nyakati tofauti kwamba makachero wengi wa CIA walikuwa ni double agents walipokuwa East German na Soviet.

Baada ya haya mambo kutokea hadharani ilikuwa ni kama udhalilishaji kwa shirika la CIA lililokuwa likijinasibu kuwa na nguvu ya kijasusi duniani. Kwa mfano inasemekana kwamba baada ya ujenzi wa ukuta wa Berlin 1961, marekani kupitia shirika lake la CIA hawakuweza kujua Nini kingefuata baada ya ujenzi huo kukamilika . Ni kwamba CIA walikuwa wakipewa wrong info au matango pori na double agents kuhusiana na ukuta huo.

Shirika la habari la CNN baadaye kwa kuchelewa Sana kupitia kwa waandishi investigative walikuja kutoa habari kamili kuhusiana na ujenzi huo na matukio yaliombatana nayo mwaka 1989 kwa umma wa marekani . Kwa kifupi Hawa double agents waliokuwa wakitumikia CIA huku wanatumikia Soviet , walikuwa wanachagua Cha kuwapa CIA kama ni matango pori au info zenye ukweli ila hazijakamilika.

Kwa mfano CIA mbali na kuwa na makachero wake ndani ya ujerumani mashariki lakini marekani haikuweza ku connect matukio ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin mwaka 1989 ndio mwanzo wa kuvunjika kwa muungano wa Soviet miaka miwili baadaye.

Mbaya zaidi Marekani haikutegemea kama bwana Aldrich Ames aliyekuwa na wadhifa mzito ndani ya CIA angekuwa double agent ambaye hakushtukiwa mapema Japo kulikuwa na warning signs. Huyu Ames alikamatwa na maafisa wa FBI mwaka 1994 akihusishwa kuwa ni double agent akiitumikia KGB kwa muda mrefu. Hii ilipelekea mshtuko na mtikisiko kwenye korido za ofisi za CIA huko Langley Virginia. Kwani baada ya kuuza info kwa KGb miezi kama 18 na maafisa wa CIA waliokuwa huko Russia kupotezwa mmoja mmoja ,ilbainika kwamba Ames alikuwa anatoa infoza CIA ambazo ziliisaidia KGB kutoa taarifa za kijasusi ambazo zilikuwa ni fake kwa ajili ya wamarekani kupitia agents maalumu. Na zaidi taarifa alizokuwa akitoa Ames alizitoa kimkakati Ili kujilinda yeye kama yeye pasipo kushtukiwa na CIA.

CIA walikuwa wanachezewa mchezo wa kitoto kupitia double agents. Hawa double agents waliamua kucheza na fursa. Kwa mfano kulikuwa na afisa wa KGB aliyeitwa Alexander zhomov alipewa kazi maalumu na Russia ya ku monitor shughuli za ubalozi wa marekani hapo Moscow na pia maafisa wote wa CIA waliokuwa nchini Russia kipindi hicho. Lakini huyu Zhomov baadaye aliamua kukutana na afisa mmoja wa hapo ubalozi wa marekani kwa Siri akisema kwamba yupo tayari kuuza info za Soviet kwa CIA Ili apate pesa na apate nafasi ya kuishi marekani. Huyu bwana alidai kwamba angewapa CIA mafaili ya taarifa zote kuhusiana ni namna gani KGB waliweza kuwagundua agents wa CIA wote waliokuwa Soviet kuanzia mwaka 1985-1986.

Kiuhalisia CIA walikuwa wanahitaji taarifa kuhusiana ni Namna gani assets zake zilikamatwa na wengine kupotezwa..(lakini kumbuka hizi assets za CIA zilizopotea walichomeshwa na Ames kwa KGB ). Na kweli idara ya CIA iliyokuwa inahusika na Soviet eastern division wakaamua kuikubali ofa ya bwana huyu ya kuwapa info hizo. Lakini kitu CIA hawakuweza kujua ni kwamba huyu bwana zhomov alikuwa ni kama chambo kwa CIA na vilevile alikuwa ni kama ngao ya kumkinga Ames asishtukiwe kwamba yeye ndiye anayewachoma wenzake kwa KGB hivyo aendelee kula pesa ya KGB kiulaini. Huyu bwana baada ya ya kupokea Hela Sasa akawa anatunga fake infos kwa ajili ya kuwapa CIA kuhusiana na wachomaji wanaowachoma agents wa CIA kwa Russia. Huu mchezo aliuendeleza kwa zaidi ya miaka mitatu lengo ni kumkinga Ames asishtukiwe.

Huyu Zhomov aliendelea kuwalisha matango pori CIA , akidai kwamba KGB wanampango wa kuweka "watu" wao maalumu ndani ya CIA ambao marekani ilikuwa inawajua na huko baadaye marekani ingewatumia kwa ajili ya kupata info za huko Russia. Hivyo marekani wangewahi hii fursa kabla ya Russia . Info hizi zilimpa zhomov pesa ndefu kutoka kwa CIA. Baadaye ikaja kugundulika wametapeliwa na huyu bwana . Naye zhomov akapotea mazima . Kwani marekani walitoa ofa ya milioni $1 kwa mtu ambaye angeweza kutoa infos za kuhusiana na maagent wake wengi kupotezwa ,Sasa ikasemekana bwana Zhomov huenda alipokea hiki kiasi au karibia kabla ya kutokomea kusikojulikana. Madhara ya kutumia double agent .
Mbali na gharama kubwa walizokuwa wanatumia CIA kwa double agent,ni kwamba information zilikuwa nyingi sana za uongo au zimepikwa.

Kwa mfano ilitoka ripoti kwamba CIA mwaka 1995,walikuja kutambua high classified informations zilizokuwa zinatolewa na idara ya Soviet-east division (SE) zilitoka kwa vyanzo ambavyo havikueleweka vizuri. Kumbuka CIA wao wakipata info ambazo walikuwa wanazihitaji na ni za Thamani walitaka kujua chanzo chake halisi..

Kwenye taarifa nyeti hizi, taarifa 35 zilitoka kwa double agents waliojulikana na taarifa Zaidi ya 60
Zilitoka kwa waliokuwa suspect wa kijasusi kwenye Baadhi ya nchi kama Cuba, German na Soviet. Taarifa hizi nyeti zilikuwa zinapaswa kuchujwa kabla ya kufika level za maamuzi kutoka kwa serikali lakini ikabainikia zilikuwa zinapenyezwa Hadi juu pasipo kuchujwa. Kwa mfano taarifa zote zilizokuwa zinatoka kwa double agents mafaili yake yalikuwa yanaandikwa kwa juu TOP SECRET na kuwekwa stempu ya "eyes only" kutokana na unyeti wake Ili yasiguswe Kwa maslahi fulani Fulani. Na ikishafika kwa wahusika wa ngazi juu mfano rais na Kisha kusainiwa ,faili hurudishwa kwa CIA kwa ajili ya kufanyiwa kazi . Sasa changamoto ni kwamba informations za hivi nyingi zilikuwa tayari zimekuwa compromised na hao double agents na vyanzo visivyoeleweka.

Baadaye kamati mbalimbali za bunge la congress na pia media zilipokuja kugundua huu mchezo walipendekeza idara za directorate operations zilizokuwa chini ya CIA ziwe accountable kisheria.
Na hili swala lilimfanya bwana Robert Gates mkurugenzi mstaafu wa CIA kukiri kwamba mchezo huu wa matumizi ya double agents inapelekea CIA kutoaminika Tena na idara zingine za usalama ya marekani katika kutunga sera zake za kiusalama dhidi ya Russia. Hili swala lilipofika bungeni , wawakilishi wa Baraza la usalama la seneti lililokuwa Linahusika na maswala ya ku oversight mambo yote ya usalama yalitoa maoni Yao na kusema marekani kwa kipindi Cha miaka kadhaa nyuma imetumia mabilioni ya Dola kwa hasara katika kuwekeza kijeshi zaidi kutokana na informations ambazo kwa upande mmoja au nyingine zilikuwa fake Na zilikuwa Zina favor Soviet kipindi hicho Cha vita baridi. Taarifa hizo ziliwafanya ku underestimate au ku overestimate uwezo wa Soviet kijeshi pasipo kujua zilikuwa ni taarifa za matango pori.

Baadaye pentagon wakaamua kufanya uchunguzi wao kuhusiana na info hizi za double agents ambazo nyingi zilikuwa ni za kupotosha na baadaye Aldrich Ames alikuja kugundulika kwa kuwa alikuwa behind za hizi information zote ambazo zilikuwa nyingine ni matango pori.

Maafisa wengi walitupiwa lawama kutokana na uzembe wa kupokea wrong info kutoka kwa double agents pasipo kuzitathimini. Na la zaidi kutomtilia maanani Aldrich Ames tokea mwanzo kuwa ni double agent ambaye alikuwa recruited na KGB pasipo kujua.

Maafisa wa ngazi za juu wa zamani na Walioko madarakani walioshtumiwa alikuwa Robert Gates, William Webster na James woolsey kutokana na uzembe walioonyesha kuhusiana na hii kadhia ya Ames na fake informations. Maafisa Hawa wa ngazi za juu waliamriwa kusaini fomu maalumu ya kukiri kosa na kuapa uzembe wa aina hiyo kutokujirudia Tena . Swali likabaki Je CIA hawakuwahi jua tokea mwanzo informations hizi kutoka kwa double agents zilikuwa fake kabla hazijafika pentagon? Lakini ikaja kusemekana kwamba CIA walikuwa wanajua na hata Ames walijua usaliti wake lakini hawakuweza kuchukua hatua haraka kutokana na kutaka kuficha taarifa za majasusi waliopotezwa (kutokana na usaliti wa Aldrich Ames)wake waliokuwa ndani ya KGB kuepushwa kuwajibishwa kisheria na bunge la congress na watunga sera za kiusalama wa marekani.

Na vilevile majasusi wanamsemo wao kwamba hakuna kitu kibaya kama kugundua ndani ya Kitengo Kuna msaliti au mole. Kwa maana hiyo kama ndani ya kitengo Kuna wasaliti wengi maana yake wote watakamatwa na kushtakiwa na mwisho wa siku kitengo kitengenezewe picha mbaya na umma. Lakini mwisho wa siku Ames aliposhtukiwa na kukamatwa , CIA iliingia kwenye mgogoro na bunge la congress Japo baadaye mambo yalikuja kutulia. CIA wakapata funzo dhidi ya double agent

MOLE .... PROTECTION.......
Kwa miaka Tisa KGb waliweza kuwachezea CIA kupitia wrong infos Ili kumkinga Ames asishtukiwe na mamlaka za marekani kutokana na kuwa double agent. Hizo informations zilikuwa fake kiasi kwamba zisingeweza kuvuta attention kuelekea kwa Ames kushtukiwa ,pale CIA walipoanza kumsaka msaliti anayewachoma agents wake kwa KGB. Na hata baada ya Ames kukamatwa mwanzoni hakuwahi kukutwa na ushahidi wa Moja kwa Moja kwamba alikuwa ni double agent anayetumikia Russia. KGB waliwaweza kwa kiasi fulani CIA.

Ripoti za kiuchunguzi baadaye zilionyesha maafisa wengi waliokuwa double agents wakitumikia CIA au mashirika mengine ya kijasusi nchi za magharibi waliochomeshwa na Ames walikuwa ni kama ifuatavyo:
Sergei bokhan, Adolf tolkachev, olte Gordievsky, Leonid poleschuk, Gennady varenik, Gennady poleschuk, Sergei vorontosov, Valery martynov, Sergei motorin, Vladimir potashev, Boris yuzhin, Vladimir piguzov, Dmitri polyakov na Vladimir vasyilev. Na wengine kadhaa ambao majina yao hayakutambulika kwa urahisi.

Maafisa Hawa baada ya Russia kuwashtukia wengine walipotezwa,wengine wakatoroka kabla ya kutiwa hatiani uchunguzi ukiendelea mfano Oleg alitoroka Hadi uingereza. Wengine walifungwa na pia baadhi ya wengine walisamehewa kutokana na unyeti wa vyeo walivyokuwa navyo............ Tuachane na hili kidogo.

Mashirika mengi ya kijasusi hususan kwenye nchi zilizokuwa mpinzani wa marekani kwenye vita baridi kama East German, Russia na Cuba zilikuwa zinajua udhahifu wa CIA na wakaamua ku take advantage na point of weakness ya wamarekani. CIA walikuwa na kiu ya kupata taarifa nyeti kwenye nchi hizo ambazo zingewasaidia marekani katika ku win vita baridi iliyokuwa ikiendelea, hivyo CIA wakaamua kupandikiza double agents lakini kumbe hata taarifa walizokuwa wanapata kwenye nchi hizi zilikuwa fake na hawakuweza kupata zile info sensitive kutoka kwa Hawa double agents kwa wakati au wakati mwingine Kwa kuchelewa.

CIA hawakuweza kupenyeza double agents kwa baadhi ya nchi kiurahisi kiasi kwamba wale waliokuwa wakijitokeza kwa kujifanya kuifanyia kazi CIA walitaka tu Dola Kisha wapotee. Hawa ndio waliokuja kuisabishia CIA matatizo kutokana na info zao kutokuwa na credibility za uhakika au tayari zimekuwa compromised tayari. Wengi wa Hawa double agent walikuwa wanafanyia CIA kama part time job Kisha wanasepa. Kwa kifupi walibaki kuwa loyal kwenye vitengo vya nchi zao na sio kwa CIA.

Kwa mfano marekani iliwatumia watu kadhaa ndani ya nchi ya Cuba kwa ajili ya kuuza Siri za serikali ya Castro ikiwemo za kijeshi. Wengi wa Hawa wa Cuba baada ya kujulikana wanatumiwa na CIA , shirika la kijasusi la nchi hiyo likaamua kutoa info fakes kwa watu hawa kwa ajili ya kuwapa CIA kiasi kwamba Sasa wakawa wapo kwenye payroll zaidi ya Moja . Mistake waliyofanya CIA hawakutaka kujishughulisha kutaka kujua background za Hawa double agents. Sasa baadhi Yao wakawa wanapata kiasi Cha Dola 500 Hadi 1700 kwa mwezi. Zilikuwa ni pesa nyingi sana kwa kipindi hicho ukilinganisha na uchumi wa Cuba uliokuwa haupo stable kutokana na sanctions za marekani. Watu wakaamua kucheza na fursa.

Mwisho wa siku baada ya haya yote kutoka hadharani CIA wakaamua kujifunza Somo in hard way kiasi kwamba wakaanza kufumua upya taratibu na kanuni za kuwatumia double agents kwenye ujasusi.

NB: DON'T TRUST ANYONE EASILY , WHEN MONEY STARTS TALKING .
 
Back
Top Bottom