Wtz wengi ni waoga wa kujaribu vitu. Deci mwanzoni ilikuwa ni organisation ambayo ilikuwa ni special kwa walokole tu. walioianzisha ni walokole, na wanaoiendesha hadi sasa ni walokole, yaani watu kama mimi hapa ninayeandika, mlokole. ninaifahamu kiundani sana. the main purpose of this Deci, ilikuwa kama kuwainua walokole, waumini wa kanisa. lakini, kwasababu ulokole/wokovu unahitaji upendo, na watu walipolalamika(wasiokuwa walokole), Deci ikaamua kupokea hata wasio walokole. hadi sasa hivi inaendeshwa na watu wa Mungu, ninao wafahamu. wachungaji kibwena wameweka pesa zao kule na wanakula faida kila wakati. kuna waislam pia wengi sana, wengi wao wanawake, wameweka pesa hapo na wanapokea pesa kibao. wengine wamejenga kwa njia hii. kuna wakati mwingine huwa wanakatishwa tamaa halafu wanajaribu kuirudisha kwa walokole(kwasababu watu wengine wanawaletea fujo...sina uhakika na hilo ila) lakini huwa wanajirudi na kuendelea kuwapenda. in short, hii ilikuwa ni njia ya kusaidia walokole lakini kwa upendo, wamewapokea hata wasio walokole. walokole wanafaidika sana na hii, na wasio kuwa walokole pia. kila mtu anakaribishwa, lakini halazimishwi.
hii ni challenge kubwa kwa watu wa dini zingine, hasa zinazojifanya zina pesa. walokole wanasapotiana sana wao kwa wao, lakini wengine wamelala fofofo. hii nchi kwa kifupi, inaenda kuendeshwa na walokole, na ndio walioishika hii nchi kwa sasa. Mungu wao anawasaidia. angalia makanisa makubwa yanayojaa kila siku, na wachungaji wao wana influence kubwa sana, wanaweza wakafanya hivyo hata kisiasa mtu asipigiwe kura, na ikawa hivyo. kwasababu waumini wana imani sana na mchungaji. walokole wamejenga mashule mengi(pamoja na kwamba roman catholic na lutheran ndio vinara kwa hili). hii ni muhimu pia kwasababu, ulokole sasa haujawa wa dini moja, kuna walokole lutheran,roman na dini zingine, hivyo nawezakusema ukristo sasa umekuwa ulokole kwasababu movement ya waumini kwa sasa si kitu cha kushangaza toka dini moja kwenda ingine, zote zina feel one. kwa kifupi, kila kanisa kubwa hapa bongo, hata mikoani, yanajenga shule za kilokole, na watoto wanakuzwa kimazingira ya kilokole. wanapata sapoti hata kama hawana hela. wanasaidiana sana, na tunajivunia kwa hilo. Deci imesaidia walokole lukuki, mimi na my wife wangu pia, tuliweka hela ya mboga, na huwa tunachuma kila baada ya miezi mitatu zaidi ya million. hiyo ya mboga tu na mafuta ya gari. inatupa faida infact.