DC wa Bariadi, Simon Simalenga anakaidi maagizo ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
34
82
-5931294413974257150_121.jpg


Machi 13, 2023 Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, iliendesha Mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa Wilaya wote nchi nzima, hii ni kutoka na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kufanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya.

Mgeni rasmi katika ufunguzi alikuwa Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango akimwakilisha Rais na siku ya kufunga Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndiye aliyekuwa mgeni rasmi

Viongozi hao wakuu wa Nchi waliwaonya wakuu hao wa Wilaya kuepuka matumizi ya wasaidizi binafsi kama walinzi, waandishi wa habari, wapiga picha au na watu wengine ambao siyo watumishi wa Serikali.

Ujumbe kama huo pia ulitolewa na Rais Samia wakati anafungua Mafunzo ya Uongozi kwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu wakuu Mkoani Arusha.

Baada ya utambulisho huo kuna huyu bwana anaitwa Simon Simalenga ambaye baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi akaona isiwe tabu, yeye kaamua kuendelea kuwa na msimamo wake tofauti kwa kuwa na Wasaidizi binafsi ambao si watumishi wa Serikali.

Wasaidizi hao ni Mpiga picha pamoja na Mwandishi wa Habari wa kike wa chombo kimoja cha kitaifa ambaye alitoka naye Songwe ambako alikuwa Mkuu wa Wilaya hiyo.

Mpiga Picha ni kijana wa Bariadi, hana taaluma hata ya uandishi wa habari bali alimchukua kwa kuwa alikuwa na ujuzi wa fani ya kupiga picha.

Huyo Mwandishi anatoka Cloud TV, yeye ana taaluma ya kazi yake lakini si Mwandishi wa Simiyu bali alikuja na DC kutokea Songwe.

DC Simalenga amekuwa akiongozana na wasaidizi hao binafsi popote napoenda huku wasaidizi wanaotakiwa kuchukua nafasi hizo Serikalini wakiwekwa kando.

Anapokuwa katika ziara zake za kikazi wasaidizi hao wanapanda gari la DC nafasi ambayo hata wasaidizi wa Serikalini hawawezi kuipata na pia anawatambulisha rasmi kuwa ni wasaidizi wake.

Kibaya zaidi amekuwa akitengeneza mazingira ya kuwalazimisha Wadau wanaokuwa wanaandaa shughuli mbalimbali za Kiserikali kuwa wawalipe posho au malipo yoyote pindi anapokwenda sehemu kufanya kazi.

Mfano inaweza kutokea amepata mwaliko sehemu kama mgeni rasmi, yeye cha kwanza anachofanya akifika ni kuwaambia waratibu wa hiyo event kuwa anachotaka watu wake kwanza walipwe kabla hata waandishi wa Habari waliolikwa na wenye event.

Wilaya yake ina Halmashauri 2, Bariadi Vijijini na Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Wakurugenzi wa hizo Halmashauri wanalalamika kila siku, wanalazimishwa kila kazi anayoifanya kwenye Halmashauri zao lazima hao wasaidizi walipwe.

Hata kazi ambayo haina malipo, ni lazima wasaidizi hao walipwe kwanza ndiyo kazi iweze kuendelea.

Hivi karibuni, alimwakilisha Mkuu wa Mkoa kwenye kazi moja, kitu cha kwanza baada ya kufika aliuliza Mhasibu yuko wapi? Alipofika huyo mtunza fedha akamwambia “Hakikisha hawa wasaidizi wangu, mpiga picha na mwandishi wa Clouds wanalipwa.”

Alifanya ziara ya kukagua miradi ya maji, akatoa maagizo hayohayo.

Alimwakilisha Mkuu wa Mkoa kwenye hafla ya Wadau wa Kilimo Kampuni ya PASS, baada ya kufungua aliwataka wahusika kuwalipa wasaidizi wake, tena alisema hawa ni wasaidizi wangu, wakalipwa Posho kama ya kwake Mkuu Wilaya.

Wahusika licha ya kulalamika lakini wakatekeleza kile walichoagizwa.

Akiwa katika ziara ya siku nne kwenye Wilaya yake, alifanya hivyo tena, wasaidizi wake hao wakalipwa kama kawaida licha ya kuwepo waandishi wengine kutoka Simiyu na wengine kutoka Songwe.

Gharama za kutunza wasaidizi binafsi wa DC Simalenga zimekuwa juu ya Halmashauri zake mbili.

Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ina Ofisa Habari wake lakini DC Simalenga hataki kumtumia hata kidogo kwenye kazi na hajawahi kumtumia.

Ukiwauliza waandishi wa Habari wenyewe wanabaki kushangaa, ambapo mmoja wa waandishi wa Habari Mkoa wa Simiyu, aliniambia kuwa yule ni kiongozi, na ana maamuzi yake.

“ Mimi sijawahi kufanya kazi yake, ingawa alikuja pale kwenye ofisi zetu waandishi wa habari ila mimi sikuwepo…na alisema atafanya kazi na waandishi wote wa Simiyu, sasa kama ameamua kutafuta wa Songwe ni uhamuzi wake, siku labda akipata shida atafute hao hao waandishi wa Songwe”

Hivyo, ni wazi kinachofanywa na DC Simalenga ni kama amedharau Mamlaka ya Uteuzi na viongozi wote wa juu waliotajwa mwanzoni mwa andiko hilo.
 
Back
Top Bottom