DC mpya wa Ikungi, Singida atumbuliwa ndani ya masaa 24

Vetting process iliyo nayo serikali yetu ni mbovu kwa sababu imejaa "yes men". Raisi hawezi kufanya kila kitu na hawezi kuwa right saa zote. Washauri wake wanatakiwa kutambua hilo na kumshauri accordingly. Wale wanaohusika kwenye issue kama hizi nao wanaogopa kupoteza kibarua na hii ni problem kubwa kwa Raisi. It has to be changed, la sivyo pamoja na effort kubwa anayofanya Raisi, matunda ya kazi yake hayataonekana over a long term.
 
Mbona hii ni kawaida na ilikuwa inatokea sana enzi ya Nyerere. Mtu unapata taarifa kuwa umeteuliwa cheo fulani, unaitisha party ya kusheherekea na kuropoka maneno ya ajabu ajabu. Mara eti 'Oh nimeukata, umasikini sasa bye bye, mademu sasa watanikoma nk'. TISS huanza kufuatilia mwendo na tabia ya mteuliwa kwa karibi sana mara tu baada ya uteuzi na uki misbehave wanatoa taarifa mteuaji ambaye atatengua mara moja.

Nadhani hiki ndicho alichokipata mteuliwa huyu.
 
M
Taarifa ya kwamba Mkuu wa wilaya Ikungi aliyeteuliwa jana Bw.Fikiri Avias, uteuzi wake umetenguliwa leo, (ndani ya saa 24) kabla hata hajaapishwa imeniacha na maswali mengi sana. Pamoja na kwamba tunaheshimu mamlaka ya uteuzi lakini nadhani ipo shida mahali fulani. Kama ndugu Fikiri hakupaswa kuwa kwenye nafasi hiyo ilikuaje haikujulikana mapema hadi akatangazwa? Nadhani hii si habari njema sana kwa mamlaka husika. Rais wetu mwema Magufuli anapaswa kuchukua hatua zaidi ili kujiridhisha na wateule wake kabla haja"publisize". Anyway namtakia majukumu mema DC mpya wa Ikungi Bw.Miraji Mtaturu ambae alikuwa Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza.!

Malisa G.J
MPWa kapewa jina hewa kashtukaa
 
What if file lake limekuwa wazi baada ya kutangazwa.. nikimaanisha baadhi ya taarifa zilikuwa hazijulikani lakini baada ya watu kuona jina lake wakazitoa..
Kama ni hivyo kuna uwezekana.marehemu akatangazwa kuwa mkuu wa wilaya siku moja. Inawezekanaje mtu ambaye taarifa zake hazijulikani ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya?? Kwani rais hana watu wa kufuatilia taarifa za watu anaowateua?
 
Taarifa ya kwamba Mkuu wa wilaya Ikungi aliyeteuliwa jana Bw.Fikiri Avias, uteuzi wake umetenguliwa leo, (ndani ya saa 24) kabla hata hajaapishwa imeniacha na maswali mengi sana. Pamoja na kwamba tunaheshimu mamlaka ya uteuzi lakini nadhani ipo shida mahali fulani. Kama ndugu Fikiri hakupaswa kuwa kwenye nafasi hiyo ilikuaje haikujulikana mapema hadi akatangazwa? Nadhani hii si habari njema sana kwa mamlaka husika. Rais wetu mwema Magufuli anapaswa kuchukua hatua zaidi ili kujiridhisha na wateule wake kabla haja"publisize". Anyway namtakia majukumu mema DC mpya wa Ikungi Bw.Miraji Mtaturu ambae alikuwa Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza.!

Malisa G.J
We, the people, must join hands to stop this madness that has engulfed our nation today...I feel that we have the worst President(kwa mujibu wa Lubuva) ever!
 
Back
Top Bottom