DC Makame: Vijana tambueni sababu ya uwepo wenu duniani

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,754
Reaction score
2,859
Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Jabiri Makame, amewataka vijana nchini kujiuliza na kutambua sababu ya uwepo wao duniani, akisisitiza umuhimu wa kila kijana kujiwekea malengo ya maana na kujiendeleza kwa bidii katika maisha.

Akizungumza katika Kongamano la Uwezeshaji Vijana lililoandaliwa na Global Youth Empowerment Institute (GYEI) lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam siku ya Jumapili, Aprili 27, 2025, Makame amesema:

“Jambo la msingi ni kutambua wewe ni nani, umeletwa duniani kuja kufanya nini. Haujaletwa hapa duniani kuja kuzurura. Kwenye dini zetu tunaamini kwamba lengo la kwanza la mwanadamu ni kumuabudu Mwenyezimungu, lakini ukiachana na lengo hilo kuna malengo mahususi ambayo Mwenyezimungu kila mmoja amewekewa ndani yetu."

Makame amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kuishi ndoto zao kwa kuweka juhudi kwenye kile wanachokifanya, huku wakijitambulisha kama watu wa kuaminika katika jamii. Amesema kuwa mafanikio hayatokani tu na ndoto pekee bali na juhudi, maadili, na uaminifu ambao vijana wanajijengea miongoni mwa watu wanaowazunguka.

Ametoa wito kwa vijana wa kizazi hiki kuwa na mwamko wa kuwekeza katika misingi thabiti ya maisha, ikiwemo kuonekana kuwa watu wa kuaminika, wanaotegemewa, na wanaochangia ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
 
Awe wazi, aseme tyuu vijana wawe machawa, maana wakiwa upinzani wana wa sativa, Lok
 
1745826244753.jpeg
 
Back
Top Bottom