Samia: Vijana wanamezeshwa sumu kuchukia Serikali

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
7,600
Reaction score
15,522

Samia amesema kuwa baadhi ya Mataifa makubwa duniani hayafurahishwi na kasi ya maendeleo ya Nchi zinazoendelea, huku wakiwalaghai Vijana kuhujumu Mataifa yao.

Samia ameyasema hayo leo Julai 13, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali pamoja na Wakuu wa Sheria uliofanyika Jijini Arusha.

Amesema katika mazingira ya sasa ya ushindani wa Kimataifa, baadhi ya Vijana wamekuwa wakishawishiwa na kulaghaiwa ‘Kumezeshwa Sumu’ kuichukia Nchi yao pamoja na kuhujumu juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali zao.

“Nimemsikia mmoja wa Viongozi wakubwa duniani akisema kuwa yeyote anayewazidi kwa kasi ya maendeleo ni adui yao, Nchi zetu zinapopiga hatua mbele, wengine wanatafuta njia na mbinu za kuzivuta nyuma,” amesema Samia.

Ameongeza kuwa dunia inaendelea kushuhudia Mataifa yakihujumiana kwa njia mbalimbali, huku baadhi ya Vijana wakipewa taarifa na mitazamo inayowafanya kuhujumu Mataifa yao wenyewe.

“Tunashuhudia Vijana wakilaghaiwa, wengine wakimezeshwa sumu dhidi ya Mataifa yao na kushawishiwa kuhujumu uchumi unaojengwa kwa nguvu kubwa,” amesema.
 
Kuamini kuna kumezeshwa sumu katika dunia ya sasa ni ujuha.

The world is full of information sources ktk dunia ya sasa.

No one can fool the society ktk dunia ya sasa.

Ni wao viongozi wa sasa ndiyo wamegoma kubadilika ili waendane na nyakati za sasa.
 
View attachment 3628340

Samia amesema kuwa baadhi ya Mataifa makubwa duniani hayafurahishwi na kasi ya maendeleo ya Nchi zinazoendelea, huku wakiwalaghai Vijana kuhujumu Mataifa yao.

Samia ameyasema hayo leo Julai 13, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali pamoja na Wakuu wa Sheria uliofanyika Jijini Arusha.

Amesema katika mazingira ya sasa ya ushindani wa Kimataifa, baadhi ya Vijana wamekuwa wakishawishiwa na kulaghaiwa ‘Kumezeshwa Sumu’ kuichukia Nchi yao pamoja na kuhujumu juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali zao.

“Nimemsikia mmoja wa Viongozi wakubwa duniani akisema kuwa yeyote anayewazidi kwa kasi ya maendeleo ni adui yao, Nchi zetu zinapopiga hatua mbele, wengine wanatafuta njia na mbinu za kuzivuta nyuma,” amesema Samia.

Ameongeza kuwa dunia inaendelea kushuhudia Mataifa yakihujumiana kwa njia mbalimbali, huku baadhi ya Vijana wakipewa taarifa na mitazamo inayowafanya kuhujumu Mataifa yao wenyewe.

“Tunashuhudia Vijana wakilaghaiwa, wengine wakimezeshwa sumu dhidi ya Mataifa yao na kushawishiwa kuhujumu uchumi unaojengwa kwa nguvu kubwa,” amesema.
Kwa huyu bibi Aibu utaona wewe
 
Swali la kawaida tu, tena halihitaji akili kubwa, mpaka leo bado Tanzania tunateseka na maji na mgao wa umeme toka uhuru???
Akuna mtu anamezeshwa sumu, kasi ya maendeleo ni ndogo…watu wanalalamika haki hakuna, hatua gani imechukuliwa?
 
Tunashuhudia Vijana wakilaghaiwa, wengine wakimezeshwa sumu dhidi ya Mataifa yao na kushawishiwa kuhujumu uchumi unaojengwa kwa nguvu kubwa,” amesema.
Mkulu sijui huwa anapewa hizi taarifa na nani? Au ndio ile unasifiwa kukimbia hadi unapitiliza kwenu.

Always, anapozungumza huwa anakuwa Kinyume kabisa na Uhalisia, utafikiri yeye anaishi Russia na amekuja Tanzania kutembea.

Mtu isipomfaa akili yake, utamdhuru Ujinga wake.
 
View attachment 3628340

“Tunashuhudia Vijana wakilaghaiwa, wengine wakimezeshwa sumu dhidi ya Mataifa yao na kushawishiwa kuhujumu uchumi unaojengwa kwa nguvu kubwa,” amesema
Samia ndio anatoa sumu karibu kila akiongea kwa kauli zake, vitendo vyake, teuzi zake, wizi, ufisadi, utekaji, utesaji, ufiraji, uuaji wake na kuwapoteza Watanganyika wanaodai haki zao.

VIkundi vyake vya utekaji, kigaidi, alivyovitengeneza ndivyo vinatoa sumu kali inaweyoweza
kuliangamiza hili taifa.

Vikundi,magenge yake yanayoratibiwa na kuongozwa na watu kama mtoto wake Abdul, Mwaipopo, Mafwele ni hatari na sumu kali kwa mustakabaribwa hili taifa.
 
Atoke pale huyu na yeye.Kasi gani ya maendeleo bhana.Kusingizia beberu bure.Beberu zenyewe ziko vitani huko na Iran hazina muda na habari zetu.Hata hivyo habari ya kiongozi wa Venezuela si anayo.
 
Washauri wake hawamwambii ukweli hali ilivyo kwa ground? Tunataka maendeleo ya vitu au maendeleo ya watu?
Washauri hata wakimwambia haitasaidia kitu.Huyu bibi ni blank slate.Wewe hotuba anaandikiwa vizuri lakini umeona makosa aliyokuwa anafanya kipindi anasoma hiyo hotuba.

Jina lake mwenyewe kalikosea kama mara tatu sijui anakuwa anakimbizana na nini?Kazi kweli kweli.Siku kakosea kwenye bei za mafuta nilijua ni mbinu ya kutoa watu mchezoni lakini leo kanichosha mazima.
 
View attachment 3628340

Samia amesema kuwa baadhi ya Mataifa makubwa duniani hayafurahishwi na kasi ya maendeleo ya Nchi zinazoendelea, huku wakiwalaghai Vijana kuhujumu Mataifa yao.

Samia ameyasema hayo leo Julai 13, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali pamoja na Wakuu wa Sheria uliofanyika Jijini Arusha.

Amesema katika mazingira ya sasa ya ushindani wa Kimataifa, baadhi ya Vijana wamekuwa wakishawishiwa na kulaghaiwa ‘Kumezeshwa Sumu’ kuichukia Nchi yao pamoja na kuhujumu juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali zao.

“Nimemsikia mmoja wa Viongozi wakubwa duniani akisema kuwa yeyote anayewazidi kwa kasi ya maendeleo ni adui yao, Nchi zetu zinapopiga hatua mbele, wengine wanatafuta njia na mbinu za kuzivuta nyuma,” amesema Samia.

Ameongeza kuwa dunia inaendelea kushuhudia Mataifa yakihujumiana kwa njia mbalimbali, huku baadhi ya Vijana wakipewa taarifa na mitazamo inayowafanya kuhujumu Mataifa yao wenyewe.

“Tunashuhudia Vijana wakilaghaiwa, wengine wakimezeshwa sumu dhidi ya Mataifa yao na kushawishiwa kuhujumu uchumi unaojengwa kwa nguvu kubwa,” amesema.
Serikali yake inaua raia ,inateka watu hovyo ,inawanyonya wananchi kwa makodi yasiyo na kichwa wla miguuu halafu hizo fedha wanaenda kuzitumbua familia tatu tu Kiziga,kizimkazi na msoga.....Na wengine waliosalia wanakula kwa urefu wa kamba huku wananchi tukila VUMBI.

Kwa mwendo huo lazima sirikali ichukiwe.
 
Back
Top Bottom