DC Kiteto anafumbia macho suala la wafugaji kulisha mashamba ya wakulima wilayani

Sep 14, 2023
82
66
Ugomvi wa wakulima na wafugaji wilayani Kiteto unachangiwa kwa kiasi kikubwa na Viongozi wa Wilaya kuwasadia jamii ya wafugaji kulisha Mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima.

Na wanapata nguvu kubwa kwa DC Wa Kiteto ameweka wazee upande anauoupendelea kwenye sakata hili.

Mwaka huu wakulima wa maeneo ya Pori number Moja, London, Mbiri, Ngabolo, Mererani, Lekumaishi, Kwa mwarabu, Ndaleta, Kambi ya mkaa, Kisima, Kilima mbogo, Dunya, Lengatei, mashamba yao yameharibiwa Kwa kiasi kikubwa na wameshindwa kuvuna mbazi.

Mamia ya ng'ombe yamechungwa mashambani. Ukiacha janga la tembo kuwa wengi mitaani na kuharibu mali mashambani yeye akiwatuma maliasili wapambane na mkaa badala ya kuwatumia maliasili kurudisha tembo nyuma.
 
Pole sana Mkuu. Unaweza ukapoza kidogo hasira uandike kwa utaratibu wa 5Ws+H ili nasi wasomaji tujue hasa unazungumzia nini, nani, wapi, lini,kwa nini na ni kwa namna gani ugomvi wa wakulima na wafugaji wilayani Kiteto unachangiwa na huyo mtajwa hapo juu.
 
Back
Top Bottom