Manyara: Wakulima Kiteto warejea kwenye mashamba waliyoondolewa, watuma ujumbe kwa Rais Samia wakidai wameporwa Ardhi yenye mashamba yao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Wakulima wa Vijiji vya Mwitikira, Ndaleta, Katikati, Ngabolo na Olboloti Wilayani Kiteto Mkoani Manyara waliodai kuporwa maeneo yao ya mashamba wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati changamoto yao inayowakabili kuhusu kuporwa ardhi ya Wafugaji wakidai kuwa wanapewa nguvu na baadhi ya maafisa wa Serikali.

Mgogoro wa ardhi baina ya Wakulima hao na Wafugaji umekuwepo muda mrefu ambapo Wakulima wanadai kigezo cha wao kuondolewa katika maeneo yao kwa madai kuwa mashamba hayo yapo ndani ya Hifadhi ya Jamii ya Makame (WMA), Kiteto ni kweli wakidai kuwa wanaodolewa wao kwa kuwa kuna watu wanaotumia maeneo hayo kulisha mifugo yao.

Wanadai kuwa wameshafikisha malalamiko yao kuanzia ngazi ya Wilaya hadi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara (Queen Sendiga) lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Mbali na kupeleka ujumbe kwa Rais Samia pia wametuma ujumbe kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wakiomba waingilie changamoto yao hiyo.

Baadhi ya Wakulima wamekusanyika na kuandika ujumbe kadhaa kwenye makaratasi kwa ajili ya kusambaza katika jamii ili ujumbe umfikie Rais Samia na viongozi wa juu Serikalini wakidai kuwa kuna mazingira ya rushwa katika mchakato wa wao kuondolewa maeneo hayo.


7.JPG

6.JPG

5.JPG

4.JPG

1.JPG

2.JPG

20231120_100845.jpg

Tamko la Serikali
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga alipoulizwa kuhusu changamoto hiyo amesema:

Ni kweli kuna aadhi ya maeneo kuna migogoro ya ardhi sugu kwa maana ya miaka mingi, kama Mkoa tumejipa muda kuwa hadi kufikia Januari 15, 2024 tuwe tumemaliza migogoro na ile sugu tuweitengenezea mikakati maalum.

Nimeanza ziara maalum ya kushughulikia changamoto ya migogoro hiyo, kampeni ilianza siku chache zilizopita na inaendelea.

Eneo lolote migogoro inawezekana kutatuliwa, migogoro mingi wanaanzisha wenyewe kwa kutofuata Sheria, tunachohitaji ni kufuata Sheria, kila upande utapata haki kulingana na Sheria.

Wananchi wanarejea kwenye maeneo kinyume cha Sheria hapo watakuwa wanavunja utaratibu, nimewaomba wawe na Subira kwa kuw akuna migogoro ambayo imedumu kwa miaka 25 inamaanisha kunahitajika utulivu zaidi.

Pamoja na hivyo, Wataalam wetu wa Kilimo wanafanya kazi kutoa elimu ya Kilimo.

Naomba wanipe muda, wawe na subiria, uongozi huwa unabadilika hivyo kuna mambo yanatakiwa kufanyiwa kazi, kuendeleza migogoro ni kutengeneza mazinira ya kudumaa na kutokuwa na maendeleo.
=========

Oktoba 7, 2022 hali ilivyokuwa
311168643_8496599470357884_7705347946460672443_n.jpg
 
Back
Top Bottom