Polisi Kiteto wamekamata Wakulima, wanawatesa na kuwanyima dhamana

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
4 (2).JPG
Kutokana na mgogoro wa ardhi unaoendelea Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, baadhi ya Wakulima wa Vijiji vya Mwitikira, Ndaleta, Katikati na Ngabolo inadaiwa wamekamatwa na Polisi na wamewekwa ndani.

Hakuna taarifa yoyote inayoendelea, Jeshi la Polisi mbona mnafanya maamuzi ambayo ni ya kidikteta, juzi hapa si Mkuu wa Mkoa kasema wanashughulikia tatizo hilo na hadi kufikia Januari 15, 2024 kila kitu kitakaa sawa

Sasa mbona mnakamata Wakulima na kuwaacha wafugaji ambao wanaendelea kupelekea mifuo yao kwenye mashamba hayo wakati Mamlaka nyingine zinasema maeneo hayo ni ya hifadhi, inakuwaje hifadhi kisha kunakuwa na mifugo tena ikiwemo mifugo ya Wanasiasa?

Majibu ya Jeshi la Polisi haya hapa - Wakulima 27 Wilayani Kiteto washikiliwa na Polisi kutokana na mgogoro wa Ardhi

Pia soma = Manyara: Wakulima Kiteto warejea kwenye mashamba waliyoondolewa, watuma ujumbe kwa Rais Samia wakidai wameporwa Ardhi yenye mashamba yao
 
Hii Nchi inahitaji Peasants Revolt dhidi ya utawala wa kimabavu wa Serikali ya CCM.
 
Kutokana na mgogoro wa ardhi unaoendelea Wilayani Kiteto Mkoani Mara, baadhi ya Wakulima wa Vijiji vya Mwitikira, Ndaleta, Katikati na Ngabolo inadaiwa wamekamatwa na Polisi na wamewekwa ndani.

Hakuna taarifa yoyote inayoendelea, Jeshi la Polisi mbona mnafanya maamuzi ambayo ni ya kidikteta, juzi hapa si Mkuu wa Mkoa kasema wanashughulikia tatizo hilo na hadi kufikia Januari 15, 2024 kila kitu kitakaa sawa

Sasa mbona mnakamata Wakulima na kuwaacha wafugaji ambao wanaendelea kupelekea mifuo yao kwenye mashamba hayo wakati Mamlaka nyingine zinasema maeneo hayo ni ya hifadhi, inakuwaje hifadhi kisha kunakuwa na mifugo tena ikiwemo mifugo ya Wanasiasa?
Mifugo ya mwanasiasa yupi mkuu
 
Kutokana na mgogoro wa ardhi unaoendelea Wilayani Kiteto Mkoani Mara, baadhi ya Wakulima wa Vijiji vya Mwitikira, Ndaleta, Katikati na Ngabolo inadaiwa wamekamatwa na Polisi na wamewekwa ndani.
Au naota
 
Back
Top Bottom