DC Hapi aagiza baa maarufu Jijini Dar, Corner bar ifungwe!

DC Hapi aagiza baa maarufu Jijini Dar, Corner bar ifungwe!

Ifungwe tu zipo na nyingine nyingi,zifuatiliwe bila ya kuangalia sura za wanaozimiliki.
 
Mheshimiwa Taylor9119 tafauti na watalii wa ndani vilvile uchumi wa kinondoni utaporomoka kutokana na maneneo yanayotinga twenty four seven ndani ya jiji ni pamoja na pale pale.

Ni kweli kabsa Mhe. Okyoma, naunga mkono hoja yako, haitaji akili za ziada..
 
Dar es Salaam. Baada ya malalamiko kuzidi kutokana na kuwapo biashara zisizo rasmi katika baa maarufu ya Corner, sasa baa hiyo imeamriwa kufungwa.

Akiwa katika ziara ya kawaida leo (Jumamosi) mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Ofisa Biashara wa Kinondoni, Mohamed Nyasama kuifunga baa hiyo.“Hatuwezi kuvumilia vitendo hivivikaendelea kufanyika huku tukiwa kimya...

Natoa agizo kesho nendeni kaifungieni hiyo baa kwa kuwa inakiuka maadili,”amesema Hapi.

Hata hivyo Nyasama amesema walishaitoza baa hiyo faini ya Sh 300,000 kwa kosa hilo.“ Mkuu hii baa ni sugu, nimeahawahi hata kuipiga faini na bado imeendelea na utaratibu huo huo wa kuruhusu kina dada kujiuza.

Kwa amri yako mkuu naanza taratibu za kuifungia leo, hadi kufikia keshoitakuwa tayari,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

img_20170225_203946-jpg.474544
hivi bar inahusikaje na biashara za ngono? kwani mmiliki wa bar ndiye anayewauza hao akina dada? amri za kipuuzi kama hizi zisifumbiwe macho hata kidogo. yeye mwenye bar anauza bia na sio uchi. pesa zinazotokana na uuzaji nyuchi zinachukuliwa na wauza nyuchi wenyewe. sasa hapa mmiliki wa bar anahusikaje? akina bashite kumbe wapo kila kona katika nchi hii.
 
MAHOJIANO MAHAKAMANI YATAKUWA HIVI:

WAKILI: Unaweza kuiambia mahakama umri na elimu yako?
DC: Nina umri wa miaka 29. Nimesoma hadi darasa la saba na kisha nikajiendeleza hadi ngazi ya cheti katika chuo cha chama Kivukoni.

WAKILI: Je, kuna sheria yoyote inayoharamisha biashara ya kuuza uchi katika nchi hii?
DC: Hapana

WAKILI: Kama ndivyo, je wauza uchi wakikamatwa na polisi hufunguliwa kesi gani?
DC: Hufunguliwa kesi ya uzururaji.

WAKILI: Je, mliwahi kumkamata mmiliki wa bar hii ndugu (anamtaja jina) akizurura na mlimchukulia hatua gani?
DC: Hapana. Hatujawahi kumkamata akizurura, hivyo hatuwezi kumfungulia mashtaka.

WAKILI: Unaweza kuiambia mahakama huyu mteja wangu mmefikisha hapa kwa kosa gani la jinai alilotenda?
DC: Tumemfikisha mahakamani kwa kuwa tulikuta watu wakizurura kwenye bar yake.

WAKILI: Kwanini hamkuwakamata wao badala ya kumkamata mmiliki wa bar?
DC: (huku akikuna kichwa) KIMYA!!!!!!!!!!

WAKILI: Je, ni nani mwenye jukumu la kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wazururaji?
DC: Ni polisi na kisha kuwafikisha mahakamani.

WAKILI: Nikikuambia kwamba elimu yako ni ya kutiliwa mashaka sawa na ya ndugu Bashite nitakuwa nimekosea?
DC: Utakuwa sahihi kabisa mheshimiwa. Unachosema ni........

....INTERUPTION....wakili wa serikali anasimama na kumzuia DC asiendelee kujibu swali hilo lakini wakili wa utetezi anapinga na mahojiano yanaendelea.....

WAKILI: Je, kuna kifungu chochote kinachotamka kwamba mtu anaweza kushtakiwa na kufungwa kwa kosa au makosa yaliyotenwa na mtu au watu wengine?
DC: Hapana.

Maswali kutoka upande wa utetezi yanafungwa na baada ya siku tano hakimu anasoma hukumu.

*********************************************
HAKIMU: Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili nimejiridhisha kwamba mtuhumiwa hana kosa lolote kisheria hivyo upande wa mashtaka (DC na wapambe wake) wanaamriwa kulipa gharama za kesi, pamoja na fidia ya Tsh 1.2 bilioni kwa kuvuruga biashara ya ndugu (anamtaja jina).

Koooooooooooooooooti!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Umeongea usichokijua ndugu.

Mwenye bar kama hataki Malaya kwenye bar yake huwakuti. Wenye bar ndio huwaruhusu Malaya wawepo ili Malaya wakiume wajazane pale
Unawezaje kuthibitisha hili kisheria? Je, mwenye bar ndiye anayewalazimisha kujiuza? Hata kama ndiye, je mimi nikikushawishi wewe uende kuiba siku ukikamatwa mimi ndiye nitakayeenda jela badala yako wewe MWIZI? Unapobishania haya mambo ya kisheria ni vizuri ukajirudishia akili kwanza.
 
Hata kama wakiifunga hio bar, commercial sex workers are there to stand and we shall continue getting their services as usual. Ni ubashite tu unamsumbua huyo DC, akielimika ataacha.
 
hamna bar maarufu na kubwa utakayoenda hapa mjini haina machangu kama vipi zifungiwe zote tu
 
Hivi machangudoa wapo coner bar tu? Tukiesabu sehemu changudoa wanakopatikana mbona bar zote maarufu zitafungwa? Pia hivi mmiliki wa bar atajuaje mteja fulani anajiuza? Maana ya jiji ni nini?
 
Lissu kuna hela huku corner bar. Zungukia utengrneze mazingira.
Hi serikali ya .....italipa fidia miaka mingi sana,samaki,vivuko,madawa ya kulevya,ee mungu nusuru watu wako maana taifa linaangamia
 
Huu ndo uteja wa madaraka.Hivi mtaani kwako kukiwa na vibaka utafunga nyumba za wakazi au ni kuwaondoa wakosaji.Ptuu miviongozi ya aibu namna hii sijui yanapatikana wapi.Mwenye biashara ya baa analipa leseni,ajira na kodi.Mi namshauri atinge mahakamani kudai hiyo amri ipigwe stop.Mbona wasifunge pia kituo cha polisi mabatini kilichopo jirani na eneo hilo kwa kushindwa kudhibiti hao wakosaji?Tena zaidi ya hapo hao kina dada wanajipanga barabarani,kama mtindo ndo huo basi nayo ifungwe.Chizi uyu anashindwa kujua ukiifunga baa hao wakina dada watahamia sehemu nyingine badala ya kumaliza tatizo unakuwa umelihamishia kwingine.
 
Huyu naye CV yake ikuye huku wasije kuwa ndugu, manake yule mwingine kapitia hapohapo, yan DC anajazwa maneno na washindan wa kibiashara Naye anakurupuka kufangia bar, ivi amewah Fanya hats biashara ya kuuza kalamu shuleni huyu?
 
Hii sio amri halali. Unawafungiaje kisa kuna machangu? Hawa vijana sijui Dr. JPM aliwaokota wapi?

Yaani hapa ni kweli hii biashara ya kujiuza haifai.

Lakini turudi upande wa pili ni kwamba sidhani kama huyo mwenye bar ndiye amewaajiri hao madadapoa kujiuza hapo. Inatakiwa itafutwe njia ya kuwadhibiti na siyo kufunga biashara.

Biashara yoyote kama hakuna wateja lazima mwenye biashara ataifunga na kutafuta biashara nyingine, sasa kwa suala hili inabidi wadhibitiwe wateja wa madada poa ndipo suluhisho litapatikana lakini siyo kumzuia au kumtoza faini mwenye biashara ya vinywaji.

HII SIYO HAKI KABISA NA YEYE HAWEZI KUJUA NI NANI MTEJA WA KINYWAJI NA NANI MTEJA WA NGONO.

TUCHUKUE TAHADHARI UKIMWI BADO UPO.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Je mtu anaweza ifunga Serena sababu machangu hukaa Ohio street?
 
Ukahaba ni biashara kongwe zaidi duniani,Hapa anajitekenya mwenyewe hawezi ishinda
 
Waliokuwa wanajiuza huko Sina wametawanyika ktk machimbo mengine.

Sugar ray bar kibao sana. Chang'ombe

Kimboka Buguruni wamejaa Buguruni

Sewa bar kibao usiseme Buguruni

Buriaga bar kibao Temeke

Keezy pub kimara ndiyo usiseme

N.k
 
Yule Mzee wa "suti ya kaptula nyeupe na shati jeupe" atakuwa ameonewa kwa hakika. .....

Kutoka Corner Bar mpaka Kituo cha Polisi - Mabatini ni kama mita 500 tu .....

Sijui kama kuna Baa itanusurika kwa mwendo huu. ....

Kusoma UDSM kutumike kuimarisha siyo kubomoa hata kama ulichukia wale waliokuwa wanaenda Corner Bar those days....
 
Waliokuwa wanajiuza huko Sina wametawanyika ktk machimbo mengine.

Keezy pub kimara ndiyo usiseme

N.k

Mkuu nlikua sijui kama 'kez pub' pale baruti/kona wapo pia. Nna mda mrefu kidogo sijaenda, ngoja niende kesho nkajionee mwenyewe. Ila kez pub weekend huwa ina amsha amsha ya hatari
 
Mkuu nlikua sijui kama 'kez pub' pale baruti/kona wapo pia. Nna mda mrefu kidogo sijaenda, ngoja niende kesho nkajionee mwenyewe. Ila kez pub weekend huwa ina amsha amsha ya hatari
Sio kila siku wapo, wenyewe wanajua kutegesha mingle zao.

Wapo sana pale! Mimi issue ni namna DC anavyotaka kufunga Bar kwasababu ya uwepo wa wanawake wanaodhaniwa kuwa wanajiuza Mimi ndiyo shida yangu.

Je mwenye Bar afanye nini wakati hao wanaodhaniwa ni wauza miili ndiyo wanaonunua vinywaji?? Na ndiyo biashara ya bar kuuza vinywaji?
 
Back
Top Bottom