Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,734
- 6,292
Naelekeza hili swali kama nilivyotumiwa kwa Mkuu mpya wa wilaya ya Kinondoni, Ndg Godwin Gondwe.
Waumini wa msikiti wa Kisumu, Magomeni mikumi wana mgogoro wa kikatiba kuwa Mkutano mkuu haujafanyika kwa miaka miwili sasa.
Hivi karibuni kupitia michango na jitihada zao wamejenga jengo la ghorofa kadhaa na limekamilika kwa upangishaji. Kuna mwekezaji kutoka Uturuki ameamua kupangisha eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya shule, lakini kuna mashaka kuwa sehemu ya viongozi waliomleta wana maslahi napo.
Katiba ya msikiti wao ambao inatamka kuwa ni lazima mkutano mkuu ujiridhishe na ndipo kupitia baraza la wadhamini upangishwaji huo ufanyike. Hili suala linashangaza kwani mwanzo wakati mkutano unakaribia OCD alifuatwa na kulishwa matango pori na viongozi wachache akauzuia bila kuja kusikiliza waumini wenyewe, Viongozi wa Bakwata walishauri mkutano mkuu ni takwa la kikatiba hivyo unapaswa kufanyika kila mwaka. wakakubaliana na uongozi na waumini kuwa ufanyike tarehe 27/6/2021 siku ya Jpili.
Lakini katika hali ya kushangaza inasemekana sehemu ya viongozi wanaohangaika na hiyo dili walikuja ofisini kwako na kuwalisha matango pori kuwa kutakuwa na uvunjifu wa amani na ofisi yako bila kutafiti ikaamua kuuzuia mkutano huo tena kwa barua baada ya wao kutuma watu au kwenda kusikiliza waumini wana tatizo gani.
Baada ya uchunguzi mwingine imeonekana kuwa hawa viongozi wachache wanahofia mkutano mkuu utawaondoa na baadhi yao kutokana na kashfa za kusigina katiba yao lakini pia wanataka kwanza upangishaji ufanyike wafanye yao then kama mengine yatokee kwani ofa ya mturuki huyo ni Tshs 6 milioni kwa mwezi. Tayari kuna uthibitisho wa hilo kwani imeonekana katibu wa msikiti huo akimshinikiza Mwenyekiti waendelee na dili hilo bila kuhusisha waumini. Swali ni je, kipi kitaleta uvunjifu wa amani hapo?
Nimeleta hii katika jukwaa hili kwani inaonekana Katibu wa msikiti ambaye pia ni M.kiti wa S.Mtaa ulipo msikiti huu na kwa kutumia nafasi yake ya uenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mtaa na uhusiano wake wa karibu na viongozi wa kichama na kisiasa ngazi ya kata na wilaya kuwa ndiye anayemastermind harakati zote hziz pamoja na kulisha viongozi wengine matango pori ikiwemo ofisi yako akiamini pia kuwa mkutano mkuu unaweza kumuondoa kwenye nafasi yake kwa sababu ya tuhuma mbalimbali za kifedha na kikatiba.
Nimeshangaa sana kwani nakujua Mh Gondwe ni mtu wa kwenda Field kujiridhisha, imekuwaje ktk hili umekurupuka na kuminya haki ya waumini kikatiba kwa sababu zisizo sahihi. Kumbuka msikiti si jukwaa la siasa bali ni sehemu ya ibada na mambo kama haya ya kuleta siasa ni kunajisi dini ya wenzetu wahusika.
Imani kwetu ni kuwa kupitia jukwaa hili utaupata ujumbe huu na wewe kwenda field kuwasikiliza waumin au pande zote na kufanya maamuzi yanayozingatia natural justice ktk suala hili.