Originally Posted by Eeka Mangi
Hii imetulia sanaaa. Walimu wetu nao wamebweteka sana. Anyway hata Julius Nyerere aliwahi kumchapa waziri wake sembuse mwalimu? Mzee Mkuu Wa Wilaya wakirudia tena kutufanya tuwe wa mwisho tunawapa mboko mbele ya wanafunzi wao. BIG UP DC
I did not expect this disappointing comment from Eeka Mangi!
"Ni kweli kuna tukio la aina hiyo na nimeshamwagiza mkuu wa mkoa kufanya uchunguzi na endapo ukweli utapatikana, serikali itachukuwa hatua kali dhidi ya wahusika," alisema Profesa Magembe na kuongeza:
"Nchi yetu haiwezi kuongozwa na watu wa aina hiyo na kamwe serikali haiwezi kukaa kimya... mara tu baada ya mkuu wa mkoa kumaliza kazi yake, atatuletea taarifa na sisi tutalifikisha kwa waziri mkuu kwa hatua zaidi kwani hao wote wako chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu".
Nampongeza sana huyo mkuu wa wilaya waache watandikwe....si majuzi 2 wametoka kugoma hapa oooh hawajalipwa pesa zao,wakalipwa, sasa kwanini wasitekeleze wajibu wao.Hongera sana mkuu wa wilaya endelea hivyohivyo watandike tena ikibidi mbele ya wanafunzi!!!!!!!
hakuna kabisa uchunguzi ni lazima ,huwezi kupokea na kuamrisha lazima ufanywe uchunguzi wa kina na ukishatimia ndio hapo hata wale walimu wanaweza wakajikusanya na kumfungulia mashtaka huyo DC Mapepe ili aonje joto la mahakama kama akina Yona na isitoshe wadai fidia ka Bilioni saba tu zinatosha ,nasikia DC hajulikani alipo.
hakuna kabisa uchunguzi ni lazima ,huwezi kupokea na kuamrisha lazima ufanywe uchunguzi wa kina na ukishatimia ndio hapo hata wale walimu wanaweza wakajikusanya na kumfungulia mashtaka huyo DC Mapepe ili aonje joto la mahakama kama akina Yona na isitoshe wadai fidia ka Bilioni saba tu zinatosha ,nasikia DC hajulikani alipo.
Hii imetulia sanaaa. Walimu wetu nao wamebweteka sana. Anyway hata Julius Nyerere aliwahi kumchapa waziri wake sembuse mwalimu? Mzee Mkuu Wa Wilaya wakirudia tena kutufanya tuwe wa mwisho tunawapa mboko mbele ya wanafunzi wao. BIG UP DC
Mkuu Mwiba,
Mi hata nashindwa kukuelewa. Unataka UCHUNGUZE NINI ZAIDI????
Jamaa kesha kiri ni kweli amewachapa viboko... na akatoa sababu so wewe unataka uchunguzi wa aina ya fimbo iliyotumika, kiwango cha maumivu AU ni nini hasa unachotaka kichunguzwe?? It is wastage of TIME, MONEY na KUFANYA WA TZ WAJINGA.
Kila mmoja apate uhakika wa kimaandishi,sio ushahidi wa kusema ,huo peke yake bado haujakuwa ni ushahidi,maana unaweza baadae akakataa na akasema haukuwachapa viboko isipokuwa wanamsingizia tu na kumpikia majungu kwa sababu anapendeza kwa wananchi, so far inabidi ushahidi uandaliwe kimaandishi ,polisi alietimiza wajibu wake nae ahojiwe mkuu wa kituo cha polisi nae ahojiwe kama alimruhusu kijana wake kwenda uraiani kucharaza mikwaju ndugu hii ni kesi kubwa maana mbali ya kumhusisha DC kuna na wengine nao pia hawatoki ukifuatilia utendaji wa kazi za kipolisi hivyo kinachotakiwa kufundishwa si kwa DC peke yake,bali hata kwa polisi waliotimiza wajibu wakiwa kazini ni nani alimpa polisi amri hiyo nae ahojiwe na akikutwa kwenda kinyume na sheria zao basi hapa Saidi Mwema itabidi amuwajibishe kiranja wake kwa kuliharibia jina Jeshi la polisi ,upo ,haya ni mambo ambayo yanataka yashonwe na yashoneke ili liwe fundisho kwa wengine ndio maana yake ,sio DC peke yake bali na wale waliokuwa nyuma yake ,sidhani kama Dc peke yake na polisi mmoja wangeweza kuwachapa viboko watu 50 lazima kutakuwepo na washiriki wengine na sheria inapochukua mkondo hata dereva nae anaweza kukaa jela wiki moja.
Ndipo sheria na utawala wakisheria utakapoanza kushika kasi.
Kwa Kuwa huyu kawacharaza waalimu Bakora kwa kuwa shule zao zimekuwa za mwisho , na yeye yafaa achapwe na Mkuu wa Mkoa kwa sababu Wilaya yake imekuwa ya Mwisho , na huu ndio utawala wa sheria.
Wana JF,
Hivi hawa wakuu wa wilaya huchaguliwa na Rais? Kama ni hivyo basi Muungwana ana viongozi MABOMU ya kutupwa. Nampa hongera mkulu huyu kwa kuthibitisha zaidi UIMARA wa Serikali ya awamu ya nne. Huyu angelifaa hata awe Rais wetu naamini tungelifika mbali maana Mafisadi wote wangelichapwa viboko.
Sijui hata yule aliyeko Kigoma na yeye anafanya kazi vipi hasa ukichukuliwa alinyang'anywa mke na kigogo wa CCM na kupewa kifutia machozi akafanywa kuwa Mkuuwa Wilaya. Nategemea hata kuwa Mbovu/imara kama huyo.
Sasa kwa kuchapwa hao walimu ndiyo watoto watafaulu?
Kwa kauli hizi bwa' mkubwa hiyo analysis yako ni very rich naona haushindani na hoja bali unamshambulia mtu binafsi. By analysing your arguments tunahitaji watu kama mkuu wa wilaya huyu wengi tu maana hata wewe unastahili viboko.