Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,932
- 985
Yupo timamu kabisa, inaonekana hiki kitendo kimemsikitisha sana na dawa ya karibu aliyoiona ni kuwatandika tu viboko badala ya kuunda tume kama watanzania tulivyozoea.
Manake uundaji wa tume na utekelezaji wa majukumu yake aliona yangemchukulia muda mrefu pengine bila majibu ambayo angeyapenda yeye.
Hii ni aibu kubwa si kitu cha kukisifia wala kukishabikia kuwa DC kafanya la maana.Si ujinga tu bali ni upumbavu usiopaswa kuvumiliwa.Anapaswa achishwe kazi.
Walimu waliocharazwa viboko, tisa wanatoka Shule ya Msingi Katerero, 11 wa Shule ya Msingi Kanazi ambao walichapwa viboko viwiwili kila mmoja na walimu 12 kutoka Shule ya Msingi Kansenene walichapwa viboko vinne vinne kila mmoja.
Fikiria kiini cha tatizo la msingi ni kutokana na wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba.
Hivi Lindi ilipokuwa ya mwisho walimu walizomewa?achana nahilo la kupigwa VIBOKO mbele ya kadamnasi.
Ona kiburi cha mawazo yaliyoganda ya DC katika fikra zake, Alisema uzembe huo umesababisha wilaya ya Bukoba kuwa ya mwisho kimkoa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana na kuwa uamuzi huo utasaidia kuwakumbusha walimu wajibu wao.
Kama kweli viboko vinamkumbusha mfanayakazi mwajiriwa nani aliyewahi kumpiga viboko yeye DC ili aweze kukumbuka wajibu wake.Yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, mbona mazeruzeru wanakatwa viungo na kuuliwa wilayani kwake?
Huyu jamaa kwanza si kweli kuwa hajui hapo wilayani kuna ofisi ya elimu ya Wilaya. Tena katika idara ya elimu kuna wakaguzi wa elimu wa kuanzia ngazi ya kanda kushuka chini hadi kata ambako tunawakuta waratibu elimu kata.
Hajaonyesha amefanya jitihada gani kusoma ripoti zao.Matatizo ya shule nyingi za msingi tchanzo si walimu bali ni serikali yenyewe.Walimu wanavunjwa moyo na namna serikali inavyoshughulikia matatizo yao.Soma zile articles za mwanzo mwanzo ambazo Haki Elimu walikuwa wanatoa, wakitazama kwa jicho la pili hali ya ELIMU YA MSINGI Tanzania, utajua ni kwanini serikali ya Mkapa ilizipiga vita.
Mwalimu siyo mhuni wa Katerero wala wa Kansenene.Ni mfanayakazi aliyeajiriwa kwa mujibu wa sheria inayozingatia taaluma yake. Ziko taratibu za kumwadhibu mtumishi/mwajiriwa.Nani kasema DC ni mwajiri wa Walimu katika Wilaya yoyote Tanzania hata awe na haki ya kuwaadhibu, si kihuni kama ivyo bali hata kwa mujibu wa sheria?
DC kawadhalilisha walimu naam si walimu tu bali watanzania wote wanaoiwazia mema tanzania.Niko hapa nilipo kwa sababu ya mwalimu,wako hapo walipo kwasababu ya walimu.
Nasisitiza hii ni fedheha kuu isiyopaswa kuvumiliwa.Ni sawa na mtoto aliyesomeshwa na mam yake kwa kufanya kazi ya kupika na kuuza pombebaada ya kumaliza kidato cha sita akapata kazi shirika la bandari.Kwa kiburi cha pesa akaja nyumbani akamwona mama yake kachafuka na machicha ya pombe akaanza kumpiga kwanini anakuwa mchafu-mchafu na kwanini anaendelea kupika pombe; mbele ya wadogo zake ambao bado wako shule ya msingi.