DC Bukoba aamuru walimu wachapwe mboko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DC Bukoba aamuru walimu wachapwe mboko!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Baba Mkubwa, Feb 12, 2009.

 1. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimesoma kwenye gazeti la mwananchi. Kuna walimu 32 wamechapwa. Mkuu wa wilaya aamuru polisi kucharaza bakora walimu 32. Ni kutokana na matokeo mabaya ya mtihani darasa la saba. MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali aliamuru polisi mmoja kuwachapa viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizo Bukoba, kutokana na wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba.

  Jamani tumefika huko?
   
 2. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu wa wilaya aamuru polisi kucharaza bakora walimu 32
  * Ni kutokana na matokeo mabaya ya mtihani darasa la saba

  Lilian Lugakingira, Bukoba na Saa Mohammed, Tanga

  MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali aliamuru polisi mmoja kuwachapa viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizo Bukoba, kutokana na wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba.

  Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi wakati mkuu huyo wa wilaya akiwa ameambatana na koplo huyo wa polisi alipowalaza chini walimu hao na kumuamuru askari huyo wa usalama, kuwachapa walimu hao viboko viwili kila mmoja makalioni na mikononi.

  Walimu waliocharazwa viboko, tisa wanatoka Shule ya Msingi Katerero, 11 wa Shule ya Msingi Kanazi ambao walichapwa viboko viwiwili kila mmoja na walimu 12 kutoka Shule ya Msingi Kansenene walichapwa viboko vinne vinne kila mmoja.

  Akizungumza jana na waandishi wa habari juu ya tukio hilo, mkuu huyo wa wilaya alisema alilazimika kuwatandika viboko walimu hao baada ya kugundua kuwepo uzembe kazini, ikiwemo kuchelewa kufika kazini na kutofundisha kama mikataba yao ya ajira inavyoeleza.

  Alisema uzembe huo umesababisha wilaya ya Bukoba kuwa ya mwisho kimkoa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana na kuwa uamuzi huo utasaidia kuwakumbusha walimu wajibu wao.

  “Nikweli nimewachapa, mara hii nimewachapwa wakiwa wamefungiwa, wakati mwingine watachapwa hadharani,” alisema mkuu.

  Kitendo hicho cha ubabe kimevuta hisia za wadau wa elimu, kikiwemo Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ambacho kimeitaka serikali kumchukulia hatua kali za kisheria mkuu huyo wa wilaya kwa kosa la kuvunja sheria na kuwadhalilisha walimu 32 wa shule mbalimbali za wilaya ya Bukoba Vijijini kwa kuwachapa viboko.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema suala hilo si jepesi na kwamba mkuu huyo wa wilaya ametonesa kidonda kibichi kwa kukitia chumvi hivyo aliyemweka serikalini mkuu huyo ndio atakayemtoa na kumchukulia hatua.

  “Hivyo akaona ni bora kuwaadhibu kwani walimu hao wanadai fidia zao serikalini na yeye akaona hakuna wanachokifanya... kwamba hawafanyi kitu ndio maana kiwango cha elimu kimeshuka,’’ alisema Mukoba

  Alisema kitendo hicho ni cha kibabe ambacho kinatumiwa na watu wanaofuja madaraka yao.

  Aliongeza kuwa CWT itatoa tamko rasmi kwa ajili ya kumpeleka mahakamani mkuu wa wilaya huyo wa Bukoba, kutokana na kukiuka haki za binaadamu.

  Alisema taarifa hiyo waliipata saa 5:00 asubuhi juzi ofisi yake walipokea barua pepe kutoka katika chama cha walimu, tawi la Kagera iliyoeleza kuwa mkuu wa wilaya anatembelea shule za msingi wilayani kwake na kutoa adhabu ya viboko kwa walimu.

  Alisema kuwa baada ya taarifa hiyo uongozi wake ulitembelea shule ambazo mkuu huyo alipita na kukuta walimu hao kwenye vituo vyao vya kazi na walimu hao walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

  Alisema kitendo hicho kimewafanya walimu hao kutokuwa na amani darasani na kufanya hata wanafunzi kuwadharau walimu hao na hata kuwacheka wanapoingia madarasani kwa ajili ya kufundisha.

  “Kutokana na hatua hii walimu wanaona kuwa hatua iliyochukuliwa ya kuchapwa viboko ni kitendo cha udhalilishaji na uvunjaji wa heshima ya mwalimu mbele ya mwanafunzi na jamii anayoishi ambayo haijapata kuona tangu waanze kazi,’’ alisema Mukoba.

  Alisema kuwa baadhi ya walimu walioadhibiwa wanafanya kazi bila ya kulipwa kwa zaidi ya miezi sita, lakini madai hayo yanaonekana ni usumbufu na wanalipwa viboko, badala ya kupewa haki zao.

  Mwenyekiti wa CWT mkoa, Dauda Bilikesi alisema wanachama wake wanaitaka serikali kuchukua hatua ili kurudisha heshima zao. Alizitaja hatua hizo kuwa ni kulipwa fidia ya kudhalilishwa na kuvunjiwa heshima kwa kuwa walimu wa kike walipigwa makalioni huku nguo zao zikibaki wazi wakati wamelaala wakiadhibiwa, tena na mwanaume mbele ya kadamnasi.

  Pia serikali iwaombe masamaha walimu hadharani na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo awajibishwe kwa kutumia madaraka yake vibaya, kutenda kosa la jinai kwa kuwachapa walimu kwa kutumia nguvu kubwa ya dola wakiwa kwenye vituo vyao kazi na kwenye majengo ya serikali na pia kuwakashifu walimu kuwa ni mafisadi kinyume na sheria kwa kuwa wanaidai serikali haki zao.

  Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Magembe alikiri kuwa na taarifa hyo na kusema kwamba kamwe hawawezi kulivumilia.

  "Ni kweli kuna tukio la aina hiyo na nimeshamwagiza mkuu wa mkoa kufanya uchunguzi na endapo ukweli utapatikana, serikali itachukuwa hatua kali dhidi ya wahusika," alisema Profesa Magembe na kuongeza:

  "Nchi yetu haiwezi kuongozwa na watu wa aina hiyo na kamwe serikali haiwezi kukaa kimya... mara tu baada ya mkuu wa mkoa kumaliza kazi yake, atatuletea taarifa na sisi tutalifikisha kwa waziri mkuu kwa hatua zaidi kwani hao wote wako chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu".

  "Hilo ni tukio la aina yake na lakusikitisha sana kwa sababu binadamu hawezi kuongozwa njia kwa kuswagwa kama ng'ombe... ni lazima serkali ichukue hatua kali dhidi ya wahusika".
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,231
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hayo yametokea. Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya TBC, Naibu Waziri, Shamsa Mwangunga, ameshauri Mkuu huyo wa Wilaya apimwe akili!.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wana JF,
  Hivi hawa wakuu wa wilaya huchaguliwa na Rais? Kama ni hivyo basi Muungwana ana viongozi MABOMU ya kutupwa. Nampa hongera mkulu huyu kwa kuthibitisha zaidi UIMARA wa Serikali ya awamu ya nne. Huyu angelifaa hata awe Rais wetu naamini tungelifika mbali maana Mafisadi wote wangelichapwa viboko.

  Sijui hata yule aliyeko Kigoma na yeye anafanya kazi vipi hasa ukichukuliwa alinyang'anywa mke na kigogo wa CCM na kupewa kifutia machozi akafanywa kuwa Mkuuwa Wilaya. Nategemea hata kuwa Mbovu/imara kama huyo.
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tungepata rais dizain ya huyu mkuu wa wilaya, pengine mambo yangekuwa tofauti. Kusingekuwa na deals za kifisadi huko serikali kwa vile ukigundulika ni habari nyingine kubwa (kama mwalimu anapewa adhabu ya viboko, nadhani fisadis kama BWM, EL, RA, AC hawa wangepata adhabu ya kifo).

  Haya ndugu viongozi, mfano wa kuigwa huo katika kuwawajibisha watumishi legelege.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahah Jamani kuna mambo huyo mkuu wa wilaya sidhani kama yuko vizuri kichwani.....
   
 7. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Yupo timamu kabisa, inaonekana hiki kitendo kimemsikitisha sana na dawa ya karibu aliyoiona ni kuwatandika tu viboko badala ya kuunda tume kama watanzania tulivyozoea.

  Manake uundaji wa tume na utekelezaji wa majukumu yake aliona yangemchukulia muda mrefu pengine bila majibu ambayo angeyapenda yeye.
   
 8. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bora tuswagane tu kama ng'ombe labda tutafika.nampa heko huyo mkuu wa wilaya na ningekuwa waziri mkuu ningempandisha cheo!!
  ningekwenda kufuatilia mienendo ya hao walimu,ningewauliza wanafunzi hata wazazi kama wanafuata schedule ya kazi inavyotakiwa,nikithibitisha ni wazugaji basi nampandisha cheo mkuu wa wilaya.
  tanzania sasa inabidi tuwe na viongozi kama hawa,hakuna kubembelezana wala kuoneana haya.tumeshachelewa sana.kama huwezi kazi basi kataa mapema kuwa siwezi tena jiondoe mwenyewe kwa hiyari yako vinginevyo tutakusurubu hadharani.tungepata dikteta mzalendo flani basi nchi ingesogea vizuri tu.
   
 9. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hao walimu au wanafunzi, Hivi hakuna sheria yoyote inayoweza kufanya huyu bwana kushtakiwa? Maana ninachoamini ni Unyanyasaji huu. Hivi ina maana kama watoto hawaelewi lawama lazima zije kwa mwalimu? Na hivi je walimu wakikataa kwenda kufundisha wilayani hapo lawama zitakwenda kwa nani Wizara ama Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Nathubutu kusema kwamba Mijitu kama hii ipimwe akili kwanza kabla ya kupewa madaraka.
   
 10. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ndio miafrika tulivyo
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Walambwe tu mboko!

  sasa kama hawafundishi na kila saa wanalalamilkia tu maslahi iweje?

  na wakati watoto wamefeli?????????l

  Mimi hizi sheria za wazungu za human rights na kubembelezana ktk nchi maskini siziamini!

  Eti mtu hana choo..... choo chake ili asipate kipindupindu...bado wanambeleza na kumsihi ajenge choo...na anakataa..eti mimi sitajenga choo..na analia eti serikali inamwonea ajenge choo chake!

  sasa mtu kama huyu afanyweje?
   
 12. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sioni uhusiano wa wajibu wa kujenga choo na uhalali wa mkuu wa wilaya kuamuru walimu wachapwe viboko. Kumbe kuna wengi tu humu JF wangekuwa ma-DC wangefanya hivyo! Tena mkuu Mzalendohalisi una signature nzuri tu, lakini inapingana na comments yako kuhusu DC.

   
 13. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #13
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuduatana na taarifa za Televissheni ya Taifa (TVT) mkuu wa wilaya ya Bukoba Albert Mnali aliamuru koplo wa Polisi awatandike viboko walimu wa shule ya Katerero,Kasenene na Kanazi kwa alichodai kuchelewa kazini.

  Koplo huyo alitekeleza amri hiyo na kuwacharaza viboko barabara.

  Naibu waziri wa Elimu Mwantumu Mahiza alipoulizwa maoni yake alisema kuwa ni Vizuri mkuu huyo wa wilaya apimwe akili yake na mabingwa kama iko timamu.

  Swali ni je na huyo Koplo wa polisi naye akili yake ni mbovu? Au yeye ni roboti la kichaa mkuu wa wilaya.Naamini kama mpiganaji Koplo ni mtu aliyefunzwa barabara kuhusu usalama wa raia na haki zake.

  Kama koplo yuko hivyo private police sijui itakuwaje.

  Kama kauli ya Naibu waziri Mwantumu iko sahihi kuwa mkuu wa wilaya naye kama ni kichaa basi nchi hii ina kazi ina maana aliyemchagua hakujua kama ni kichaa au naye ni kichaa haelewi tofauti ya mwenye akili timamu na asiyekuwa nazo anapoteua,au akiwateua hafuatilii kujua kama wamepata maradhi ya ukichaa wa madaraka unaopitiliza?

  Kwa maoni yangu Nadhani iko haja ya viongozi wote ikiwemo maraisi wetu wapimwe afya ya akili badala ya kuulizwa tu kwenye fomu zao kusema una akili timamu na mtu anajaza nina akili bila kuthibitishwa na mwingine .Ni vizuri pia kuwe na kupimwa IQ TEST.
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Mkuu, huu ni ushuhuda wa kuwa na watawala badala ya viongozi! Hana tofauti yoyote na wakoloni. Mimi natumai hawataishia kumpima akili tu, bali pia tafikishwa kwa pilato ayaone yanayomkuta Zombe. Utawala wa sheria unatakiwa kutekelezwa kwa vitendo na si maneno maneno na ngonjera. Hata hivyo, nashindwa kuelewa kitu kimoja, hivi walimu hao wote (16 kama sijakosea) ni wajinga kiasi cha kushindwa kujitetea na kukataa adhabu za kipuuzi zinazodhalilisha utu wao? Kwani angesema wote anataka kufanya nao ngono bila kujali jinsia zao wangekubali? Nadhani tatizo ni kubwa kuliko linavyoonekana. Sidhani kama kuwa na kosa kunahalalisha mtu mwingine akutendea isivyo haki.:confused:

  Siku hizi hao jamaa wanaitwa TBC1:rolleyes:
   
 15. Piemu Esquire

  Piemu Esquire Member

  #15
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona basi hata Naibu Waziri naye anaropoka tu juu ya kiongozi mwenzie sasa tuelewe yupi ni kichaa zaidi ya mwingine?

  Nadhani swala la maadili ya uongozi linafika hadi kiongozi aseme nini na atende lipi,Acha kuwa atoe maamuzi gani!!Haya , hayo ni malumbano tayari.......Tusikilize nani zaidi??? Yale yale Spika na Jaji Mkuu,Waziri na Mfanyabiashara,Mkuu wa Mkoa na Mbunge nk.School of though is important here.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Naibu waziri, Mwantumu Mahiza kweli ameenda bali. Labda naye apimwe akili pia. Vinginevyo atatufanya tuamini kuwa amezidisha staili ya mipasho!!
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huu au hizi ni dalili za udikteta ,kaeni vizuri sana na mtafakari ,ingawa kuna habari imetundikwa kule kwenye jukwaa la siasa ,kuwa wengine wamechapwa kwa kuchelewa kazini ,sasa sijui uhakika wa habari hii kwa sisi tunaoishi mikoa ya pwani.

  Sawa kama hatua hiyo imefikia ya kuwacharaza viboko wafanya kazi wa serikali kwa kuwa tu matokeo si mazuri, na serikali haijasema lolote kuhusiana na hilo au kumchukulia hatua kiongozi alieamuru kufanya hayo naona serikali sasa inaingia katika sura ya ufashisti au udikteta ,aidha Chama cha walimu kilitakiwa kusimamisha walimu wake wote wa mikoa husika kuhudhuria katika kazi zao mpaka kiongozi aliyetibuka akili ashitakiwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ,maana amewahukumu watu kupigwa viboko bila ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria,au viwache walimu wanendelee lakini vinahakikisha mkuu huyo anaondolewa katika safu za uongozi wa serikali na kushitakiwa kwa haraka sana,kwa ufupi vimfikishe kwenye vyombo vya sheria ili sheria asiyoijua yeye ifuate mkondo wake.

  Suala hili kama ni kweli sio dogo, ukilihusisha na serikali iliyopo madarakani ,na vile vile Chama kilichopo madarakani kwani ni serikali yake ,sasa pa kujiuliza hizi ndio sera za CCM ,najua watasema kisihukumiwe Chama ahukumiwe mtu mmoja mmoja. Kunahitajika tamko la serikali vilevile tamko la Chama Tawala kuhusiana na kitendo hiki cha kufikia kwa walimu kuchapwa viboko ,kama huu uongozi si wa mkoloni mweusi ni wa mkoloni gani ?

  Mambo ya kuchapwa viboko hadharani ni mambo ya kikoloni na kwa jamii yetu ya leo ni udhalilishaji,ikiwa adhabu ya viboko kwa wanafunzi inapigwa vita huko majuu na haipo na wala haitumiki tena,ni kosa kwa Mwalim kumpiga viboko mwananfunzi ,hapa Tanzania natumai shule za kulipia wanafunzi hawapigwi viboko. Lakini leo serikali inakwenda kumpiga viboko Mwalimu au walimu ,kama wametenda kosa kwa nini serikali haikuwashitaki walimu hao na kuacha mahakama ifanye jukumu lake au iamue kesi hiyo.
  Je serikali inawatisha walimu ambao wana madai ya kutolipwa kwa miezi kibao kama si udikiteta ni kitu gani ?
   
 18. J

  James J Member

  #18
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 13, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nampongeza sana huyo mkuu wa wilaya waache watandikwe....si majuzi 2 wametoka kugoma hapa oooh hawajalipwa pesa zao,wakalipwa, sasa kwanini wasitekeleze wajibu wao.Hongera sana mkuu wa wilaya endelea hivyohivyo watandike tena ikibidi mbele ya wanafunzi!!!!!!!
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hizi ni sera za kidikteta lazima tuzikemee ,na ikikubalika serikali itoe tamko kwa kitendo hiki ,hizi ni sura za kiutawala ambazo zinajitokeza ,waziri mkuu alisema uweni mtu papo hapo uraiani hakuna haja ya mahakama,na huyu nae amefuata kauli waziri mkuu kuwa hakuna kuwapeleka mahakama ni kuwaadhibu huko huko,ila Waziri mkuu alifuta kauli yake hiyo,hivyo kuifuata ni kosa.

  Kama walimu walitenda kosa ,ilibidi washitakiwe na sheria kuachiwa kufuata mkondo wake.
  Hayo ndio yameanza kesho utasikia amewachapa watu wa manispaa kwa kuwa mji ni mchafu ,na siku ingine akawambia watu wavamie maduka kwa sababu wenye maduka wanauza vitu ghali na mwananchi hana fedha ya kununua sasa afanye nini kama asiende kuchukua vitu bure.

  Huyo jamaa ajiuzulu tu na kisha apelekwe mahakamani japo mahakama itamwachia kwa kuwa hana kesi ya kujibu ,ndio maana yake kwa utawala wa CCM tulionao.
   
 20. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wahuni kama DC Albert Mnali ni wengi tu katika nchi hii.Utawala wa sheria na haki za binadamu huko wapi?
  Nashangaa chama cha walimu wanasema hawajawahi kusikia kitendo kama hicho.
  Miaka ya nyuma kuna aliyekuwa RC wa Mkoa wa Mara na pia akawa mshauri wa Rais mambo ya siasa aliwahi kuwadhalisha kwa matusi na vibao waratibu kata wa elimu kule Kinesi na Bunda kwa kuchelewa katika vikao na kutosimamia vizuri shughuli zao.
  Ni kwamba watu sasa wanaelimika na wanajua haki zao kikatiba siyo kama enzi zile za ..................
  Poor Albert Mnali
   
Loading...