..hao waalimu nao wajinga. kwanini walikubali kuchapwa viboko? ningekuwa kati ya hao waalimu huyo DC angenitambua.
Walimu sio wajinga lakini umasikini walionao ndio uliowafikisha hapo walipo ,wamewekwa bila ya mishahara kwa muda mrefu na bado hadi wanapigwa hawajapokea mshahara wala malimbikizo.
Wamewaweka na njaa mpaka akili zimewatoka na hawajui mwisho wa kukaa bila ya mishahara itaendelea mpaka lini ,ila kwa kuwasaidia mishahara itakuwa ikifuata wakati utakapowadia msimu wa uchaguzi mkuu wajue kila kitu watalipwa na malimbikizo watalipwa na nyongeza wataongezewa ili wasifu kuwa CCM ndio baba au CCM ndio chama,haya yote wanayofanyiwa wao pamoja na wanafunzi hata wale wa mlimani na kwengineko ,watayasahau yote haya wanayofanyiwa na kuiunga mkono CCM kwa hali ya juu kabisa.
Si ajabu hata wanafunzi waliofukuzwa nao wakarudishwa na kulipwa siku zao zote na kama hazijatosha wakaongezwa watafanyiwa mambo ambayo yatawasahaulisha matatizo kiasi ya kupita uchaguzi CCM wanacharuka na kuanza kuwahenya na kuwaletea polisi kuwapiga marungu na bakora.
Hawa walimu ndio mstari wa mbele kuwahimiza wanafunzi kwenda kumpokea Kikwete akiongozana na DC,Dc ambae amewapiga bakora Kikwete ambae hakumuwajibisha DC mara aliposikia (Si kweli kwamba Mheshimiwa raisi hajasikia jambo hili,si kweli kwamba Waziri Mkuu hajasikia jambo hili si kweli kwamba waziri wa Elimu hajasikia jambo hili). Walimu na wanafunzi sijui kama watayakumbuka haya na kuwanyima kura viongozi wa Chama kilichoko madarakani na badala yake kama kawaida yao nao hutumika kuisimika CCM madarakani kama wanavyotumika polisi na wenginetele.
Walimu na wanafunzi pamoja na mapolisi si watu wanaofaa kuilalamikia serikali iliyopo madarakani serikali ya CCM kuwa haiwatendei haki,kwani wao ndio wasimamizi wakuu kwa kila kitu,iweje leo walalamike kwa mambo waliyoau wanayotendewa na mtawala waliemsimika na kila kukicha au uchaguzi ,hawakumbuki shida na matatizo yanayosababishwa na kile chama wanachokiweka.
CCM haina hati miliki ya nchi hii ni Chama cha siasa kama vilivyo vyama vingine ,hivyo kinapovuruga na kupoteza dira katika kuliongoza Taifa na kufanya mambo ya ajabu ajabu ni vyema wananchi kwa pamoja wakashirikiana kukiondoa madarakani iwe kwa kura na kama hawataki kuondoka kwa kura waondolewe kwa nguvu za wananchi njia ambayo hadi sasa haijaiwacha serikali jeuri madarakani ,ni serikali nyingi tu zilizokuwa zikitegemea vyombo vya dola zimeondolewa madarakani kwa nguvu za wananchi ,watu waliomo serikalini ni wachache sana na ni rahisi kuwaondoa madarakani kwa kutumia nguvu za wananchi ,msisikie ikiwa wananchi wataamua na kuwambia CCM kuwa imetosha kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka 47 sasa muondoke au tutawaondoa kwa nguvu ,basi wataondoka tu kwa Ukubwa wa Tanzania hii,itabidi wasalimu amri maana hata wao wenyewe wanajua kuwa wameshapoteza dira ya uongozi hili sio geni kwao ,CCM wanafahamu fika kuwa kuiongoza Tanzania kwa sasa kunahitaji meno makali ambayo hayana uswahiba ,kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete mara tu alipoapishwa kuwa Uraisi wake hauna ubia ,maana yake ni hiyo kuwa atakuwa hana uswahiba lakini uongozi wa namna hiyo umemshinda kwa kuwa Chama kizima kimeoza hakuna wa kumtegemea hata mmoja kila mmoja anamshinda mwenziwe kwa ubabe,kila mmoja anajifanyia anavyotaka kila mmoja ana amri kuliko mwenziwe utafikiri tupo kwenye kambi ya mafunzo ya jeshi maana jeshini unatakiwa ufuate amri ya mwisho kuipokea na ndipo ulipo utawala wa Serikali ya CCM ,haufuati sheria za nchi haufuati maadilio ya uongozi ni varange varange tu ,sasa kama Chama hiki hakikung'olewa kwenye madaraka kifanywe nini ?
Wakiambiwa ibadilishwe KATIBA hawataki ,wakiambiwa TUME ibadilishwe hawataki kama si udikiteta ni kitu gani ,wakiambiwa mafisadi muwafunge hawataki,wakiambiwa wawafukuze kwenye Chama hawataki bado wanawakumbatia ,wakiulizwa fedha iliyorudishwa na mafisadi ipo wapi hawana jibu zaidi ya ubabaishaji sijui imepekwa kwenye mbolea ili kusaidia wakulima wakati juzi tu waliwahadaa wananchi wa mbea kununua kura zao kwa mfuko wa mbolea?