Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Sikonge, nimeshawahi kusema kuwa sioni mantiki ya kuwa na Wakuu wa Mikoa (RCs) na Wakuu wa Wilaya (DCs), hivyo vilikuwa vyeo vya kikoloni na vilitumiwa na wakoloni na si ajabu huyo DC kuamuru Waalimu wachapwe viboko! Vyeo vya RCs na DCs huwa ni vyeo vya kuwasaidia 'wenzetu' ambao hawana pa kwenda na ndo maana utakuta sehemu kubwa ya RCs na DCs ni Wabunge waliopoteza Ubunge, walioondolewa kazini bila sababu za msingi na ili kuficha ukweli au kuepusha kesi anateuliwa kuwa RC au DC (Mfano Col. Simbakalia-RC wa Kigoma alikuwa DG wa NDC, akaondolewa baada ya kukataa matakwa ya Wakubwa kuhusu Mgodi wa Mchuchuma au Liganga).
Kuna DC wa Wilaya ya Hai- Husna Mwilima, huyu alikuwa Katibu wa Tawi moja la CCM Arusha Mjini, baada ya Muungwana na kundi lake kushika hatamu sasa ni Dc wa Hai tena ni bomu kweli! Mkuu wa Wilaya ya Tabora-Moshi Chang'a ulizia elimu yake, utachoka. Lakini alikuwa ni Mkereketwa huko Iringa na Mshereshaji kwenye matukio ya CCM! wako wengi na ni vituko vitupu na wote wamekabidhiwa Mashangingi!
Ingekuwa vema vyeo vya RC na DC vikafutwa wakabaki Maafisa Tawala (RAS na DAS) ambao ndio professionals na si hawa wanasihasa.
Na kweli kazi ya hawa jamaa sasa hivi ni ubangaizaji tu. Wanakimibizana na Wakurugenzi na Mameya kwa kuonyeshana ubabe. Wengine mhhh, mambo yao yanatisha. Ila namuhusudu mrembo wangu mmoja hapo Korogwe (Betty), yeye mambo yakiwa magumu analia tu na kuomba wananchi wamuonee huruma kwa kutekeleza anachokitaka