LazaroSMtindi
Senior Member
- May 6, 2008
- 100
- 5
Katika kipindi cha Bunge leo jioni mjini Dodoma, DAWASCO kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, imemwomba radhi Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe kwa kumtangaza kuwa alijiunganishia maji kinyume cha sheria, kitu ambacho hakikuwa cha kweli.
na wengine humu humu wakakurupuka kumwita Dr Mwakyembe fisadi. Sijasahau!
Kwa mtaji huu CCM sasa ni sawa na kichaka, kilicho stawi kwa ukijani mbichi, karibu na stand isiyo na Choo.
Kila ajisikiaye haja aenda huko. Uoza, Harufu kali, Mainzi na kila aina ya kinyaa ndo kwao.
Wote ndani ya CCM wanaupenda ukijani, lakini hawakipendi kabisa kiupacho ukijani kichaka chao, yaani mashonde yanukayo.
Dawa ni kufunga pua na midomo na kujitoma na majembe surululu na nyengo na kuusafisha uchafu wote, zaidi kung'olea mbali kichaka kile na mahali pake kuchimba choo na kisha kujenga tabia ya kukitumia.
Haya, shauri yenu wenyewe, Mbolea ikizidi sana kichaka kitaungua.
Katika kipindi cha Bunge leo jioni mjini Dodoma, DAWASCO kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, imemwomba radhi Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe kwa kumtangaza kuwa alijiunganishia maji kinyume cha sheria, kitu ambacho hakikuwa cha kweli. Tamko hilo la Wizara lilikuja baada ya Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo, kuishutumu vikali DAWASCO kwenye kikao cha ahsubuhi cha Bunge kwa kujiingiza katika siasa na kuwazulia watu kashfa. Shellukindo, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki pamoja na Dk.Mwakyembe, aliishutumu DAWASCO kwa kutumiwa na kuchafua jina la Dk. Mwakyembe aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Richmond iliyofanya maamuzi ya kihistoria Tanzania na kusababisha Lowassa kujiuzulu. Lazaros
Jana nimemtafuta sana kwa simu sikumpata, lakini nikawapata wabunge wenziwe walo karibu sana naye including Beatrice mwenyewe, wakaniambia this is big joke kwa sababu kwanza hiyo nyumba wala sio yake, amepewa tu hivi karibuni na serikali,
Mimi sikuiona topic yake hapa nasikia ilitolewa haraka sana, lakini nasikia kuna waliojkaanga sana kwenye hiyo topic kwa kumuhukumu bila facts zote, tena nasikia kuna hata wakulu flani hapa walihusika na hizo hukumu, lo! aibuuu!
Mimi pia nilimhukumu Dr. Mwakyembe kwa kufuata facts ambazo zilikuwepo. Hivyo ndivyo ambavyo tumekuwa tukifanya safari zote, kutumia facts zilizopo mpaka ukweli mwingine ukijulikana.
Mkuu Mtanzania,
Heshima mbele mkuu, mimi skuiona hiyo topic, lakini ninashukuru kuwa umejitokeza kuwa ulikuwa ni mmoja wa waliokurupuka, sasa the right thing ni kuomba radhi kwa kukurupuka,
Hiyo excuse hapo juu, ni dhaifu sana kwa sababu tunapaswa kuwa na standards za kuwangalia viongozi wetu, kuna wasiostaili utafiti kabla ta kutoa hukumu na kuna ambao ni lazima kwanza tufanye utafiti kabla ya kurusha hukumu wanapotajwa,
Mimi kwa haraka haraka, viongozi kama Mwakyembe, Zitto, Dr. Slaaa, Mama Kilango, Seleli, Sendeka, Beatrice, Kaduma, hata siku moja siwezi kudandia treni bila kuwa na facts kwanza on them, mkuu hapa ulichemsha sasa dawa ni kuomba radhi tu kwa wana-forum wengine, lakini ninaheshimu kitendo chako cha kujitokeza mwenyewe!