LazaroSMtindi
Senior Member
- May 6, 2008
- 100
- 5
Katika kipindi cha Bunge leo jioni mjini Dodoma, DAWASCO kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, imemwomba radhi Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe kwa kumtangaza kuwa alijiunganishia maji kinyume cha sheria, kitu ambacho hakikuwa cha kweli. Tamko hilo la Wizara lilikuja baada ya Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo, kuishutumu vikali DAWASCO kwenye kikao cha ahsubuhi cha Bunge kwa kujiingiza katika siasa na kuwazulia watu kashfa. Shellukindo, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki pamoja na Dk.Mwakyembe, aliishutumu DAWASCO kwa kutumiwa na kuchafua jina la Dk. Mwakyembe aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Richmond iliyofanya maamuzi ya kihistoria Tanzania na kusababisha Lowassa kujiuzulu. Lazaros