BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,097
1668954094944.png

Kamati ya kufuatilia mwenendo wa matokeo ya mitihani ya mafunzo ya uansheria kwa vitendo (LST), imeanisha changamoto nane ikisema ni miongoni mwa vikwazo katika kupata wanafunzi bora wanaosomea fani ya sheria.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Harrison Mwakyembe amesema changamoto hizo pia zimelalamikiwa na LST pamoja na wadau mbalimbali wa sheria.

Dk Mwakyembe ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 20, 2022 wakati akisoma muhtsari wa taarifa ya kamati hiyo kufuatilia chanzo cha wanafunzi wengi kufeli katika mitihani ya mafunzo katika taasisi ya LST.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro, katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo, wajumbe wa kamati hiyo pamoja viongozi waandamizi wa wizara hiyo.

Kamati hiyo yenye wajumbe saba iliteuliwa Oktoba 12, mwaka huu na Dk Ndumbaro na kufanya kazi kwa siku 30 kufuatilia sakata la kufeli kwa wanafunzi wengi wa taasisi hiyo.

Sakata hilo lililoibuliwa na Mwananchi, lilitokana na matokeo ya awamu (Cohort) ya 35 ya wanafunzi wa taasisi hiyo, kuonyesha kati ya wanafunzi 633 waliofanya mtihani huo, ni 26 ndio waliofaulu kwa awamu ya kwanza.

Katika matokeo hayo, wanafunzi 265 walifeli (discontinue) na wengine 242 walitakiwa kurudia mtihani (supplementary).

Akitoa taarifa hiyo leo, Dk Mwakyembe amesema udahili wa wanafunzi wengi kupita uwezo katika vyuo vinavyofundisha sheria na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo unasababisha uwiano mbaya kati walimu na wanafunzi na kuathiri ufundishaji na usimamizi.

Pia Dk Mwakyembe ambaye ni waziri wa zamani wa Katiba na Sheria amesema kumekuwa na uhuria usio kuwa na tija kwa kila chuo kuwa na uhuru wa kupanga muda wa kukamilisha shahada ya sheria kati ya miaka mitatu au minne.

"Pia uwezo mdogo wa wanafunzi wengi wanaoruhusiwa kusoma sheria na baadaye kujiunga na LST katika kumudu lugha ya kufundishia ya kiingereza.Tatizo hili lina athari kubwa katika uelewa wa masomo ya kujieleza," amesema Dk Mwakyembe.

Mbali na hilo, amesema uamuzi wa Tume ya Vyuo Vikuu kushusha vigezo vya ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita kutoka alama nane (B mbili kwa masomo mawili hadi alama nne ( D mbili kwa masomo mawili kulikowezessha vijana wasiokuwa na uwezo kusoma masomo ya sheria.

Dk Mwakyembe mbunge wa zamani wa Kyela mkoani Mbeya amesema utatuzi wa changamoto hizo upo kisera na kimfumo. Amesema mfumo wa bora wa elimuT ya sheria unasimamamiwa na ule uanasheria kwa vitendo unasimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria nchini (CLE).

Amesema kamati inashauri kufufuliwa kwa CLE na kuliwezesha kutekeleza majukumu yake ikiwemo kukaa chini na TCU kupandisha vigezo vya ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na nne kwa wanaotaka kusomea sheria vyuo vikuu.

"Kuanzisha mtihani maalumu wa kuingia LST kama ilivyo kwa wenzetu wa Afrika Mashariki ambao utasimamiwa na CLE, " amesema Dk Mwakyembe.

Dk Ndumbaro amesema, “leo tumepokea taarifa tunakwenda msituni, tutapitia changamoto kwa changamoto zilizoanishwa katika taarifa ya kamati hii” Dk Ndumbaro

MWANANCHI
 
uamuzi wa Tume ya Vyuo Vikuu kushusha vigezo vya ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita kutoka alama nane (B mbili kwa masomo mawili hadi alama nne ( D mbili kwa masomo mawili kulikowezessha vijana wasiokuwa na uwezo kusoma masomo ya sheria.
Hapa ndipo serikali ya CCM ilipofanikiwa kucheza na akili za watanzania kwa kufyatua mavilaza na mambumbu wasioweza kuhoji kitu. Ama kweli ukitaka kuliua taifa lolote lile, ua elimu!
 
View attachment 2422326
Kamati ya kufuatilia mwenendo wa matokeo ya mitihani ya mafunzo ya uansheria kwa vitendo (LST), imeanisha changamoto nane ikisema ni miongoni mwa vikwazo katika kupata wanafunzi bora wanaosomea fani ya sheria.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Harrison Mwakyembe amesema changamoto hizo pia zimelalamikiwa na LST pamoja na wadau mbalimbali wa sheria.

Dk Mwakyembe ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 20, 2022 wakati akisoma muhtsari wa taarifa ya kamati hiyo kufuatilia chanzo cha wanafunzi wengi kufeli katika mitihani ya mafunzo katika taasisi ya LST.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro, katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo, wajumbe wa kamati hiyo pamoja viongozi waandamizi wa wizara hiyo.

Kamati hiyo yenye wajumbe saba iliteuliwa Oktoba 12, mwaka huu na Dk Ndumbaro na kufanya kazi kwa siku 30 kufuatilia sakata la kufeli kwa wanafunzi wengi wa taasisi hiyo.

Sakata hilo lililoibuliwa na Mwananchi, lilitokana na matokeo ya awamu (Cohort) ya 35 ya wanafunzi wa taasisi hiyo, kuonyesha kati ya wanafunzi 633 waliofanya mtihani huo, ni 26 ndio waliofaulu kwa awamu ya kwanza.

Katika matokeo hayo, wanafunzi 265 walifeli (discontinue) na wengine 242 walitakiwa kurudia mtihani (supplementary).

Akitoa taarifa hiyo leo, Dk Mwakyembe amesema udahili wa wanafunzi wengi kupita uwezo katika vyuo vinavyofundisha sheria na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo unasababisha uwiano mbaya kati walimu na wanafunzi na kuathiri ufundishaji na usimamizi.

Pia Dk Mwakyembe ambaye ni waziri wa zamani wa Katiba na Sheria amesema kumekuwa na uhuria usio kuwa na tija kwa kila chuo kuwa na uhuru wa kupanga muda wa kukamilisha shahada ya sheria kati ya miaka mitatu au minne.

"Pia uwezo mdogo wa wanafunzi wengi wanaoruhusiwa kusoma sheria na baadaye kujiunga na LST katika kumudu lugha ya kufundishia ya kiingereza.Tatizo hili lina athari kubwa katika uelewa wa masomo ya kujieleza," amesema Dk Mwakyembe.

Mbali na hilo, amesema uamuzi wa Tume ya Vyuo Vikuu kushusha vigezo vya ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita kutoka alama nane (B mbili kwa masomo mawili hadi alama nne ( D mbili kwa masomo mawili kulikowezessha vijana wasiokuwa na uwezo kusoma masomo ya sheria.

Dk Mwakyembe mbunge wa zamani wa Kyela mkoani Mbeya amesema utatuzi wa changamoto hizo upo kisera na kimfumo. Amesema mfumo wa bora wa elimuT ya sheria unasimamamiwa na ule uanasheria kwa vitendo unasimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria nchini (CLE).

Amesema kamati inashauri kufufuliwa kwa CLE na kuliwezesha kutekeleza majukumu yake ikiwemo kukaa chini na TCU kupandisha vigezo vya ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na nne kwa wanaotaka kusomea sheria vyuo vikuu.

"Kuanzisha mtihani maalumu wa kuingia LST kama ilivyo kwa wenzetu wa Afrika Mashariki ambao utasimamiwa na CLE, " amesema Dk Mwakyembe.

Dk Ndumbaro amesema, “leo tumepokea taarifa tunakwenda msituni, tutapitia changamoto kwa changamoto zilizoanishwa katika taarifa ya kamati hii” Dk Ndumbaro

MWANANCHI
Mwakyembe has been too local, primitive, and conservative the parameters that they have had as a team were too predicative for the results. Ametumia vigezo vyetu vya lately 2001-2002 which was the case wenye one za 7 ndio tulikuwa na uhakika wa kupata hio admission ya Sheria enzi za Kalembo kama admission officer.
 
Hata hivyo, naibu mkuu wa Taasisi anayeshughulikia mafunzo kwa vitendo, machapisho, utafiti na utaalamu elekezi wa LST, Profesa Zakayo Lukumay akizungumzia madai ya rushwa ya ngono, alisema ni vigumu hilo kutokea kwa kuwa mtihani wa mwanafunzi wa taasisi hiyo hausahihishwi na mtu mmoja.
“Kila swali linasahihishwa na mhadhiri wake, unakuta yapo maswali matatu yanasahihishwa na wahadhiri watatu sasa rushwa utawapa wote?” alihoji.
Kuhusu madai ya wanafunzi kufeli, Profesa Lukumay alisema, “tuzungumze kwa lugha nyepesi, tatizo tunacholetewa hakijaiva (hawajaiva kutokea vyuo vikuu).”
 
Katibu mtendaji mMwanzilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Anthony Ngaiza alisema, “tatizo halitokani na wahitimu wa vyuo vikuu kutokaa kwenye ‘law firms’ kwa muda mrefu.”
Ngaiza alisema tatizo ni ubora wa wahitimu, “hawana uelewa unaotakiwa kwa wanasheria. Hawana viwango stahiki vya lugha ya Kiingereza kuweza kumudu. Hata walimu wao wakiwa wazuri namna gani (ingawa naamini asilimia zaidi ya 50 ya walimu wao nao hawana ubora unaotakiwa.”
 
Mwakyembe has been too local, primitive, and conservative the parameters that they have had as a team were too predicative for the results. Ametumia vigezo vyetu vya lately 2001-2002 which was the case wenye one za 7 ndio tulikuwa na uhakika wa kupata hio admission ya Sheria enzi za Kalembo kama admission officer.
CCM walishusha vigezo ili vilaza wengi zaidi wasomee hata kama watashindwa kupenya LST. Hapa ndipo matatizo yalipoanzia.
 
Tatizo ni lugha.Hata Sheria ikifundishwa kwa kiswahili watafeli.
Aidha elimu duni Tz ni nyanja zote
Watu wengi wanategemea kukopi kwenye mitandao wakipelekwa field wanapepesa macho.
Mfano zamani mhasibu kupata CPA ilikuwa mbinde au kupata diploma au digrii ya uhandisi kulikuwa hakuna kulala lkn kwa sasa ni walkover ni kama wasoma VETA
 
Kwanini unaita rubbish? Je umeisoma yote au unategemea hiyo summary ya mtoa mada?
Swali zuri sana! Sijaisoma na sina haja ya kuisoma kwa vile huyu is not an independent thinker, ana maagizo ya party caucus as has been a tradition in Tanzania ya CCM! Huyu ni CCM hawezi kuwa mkweli!
And for your information it will never be public for public consumption!
 
Mwenyekiti wa kamati ya kufuatilia tathmini ya mafunzo yanayotolewa na taasisi ya uanasheria kwa vitendo nchini (LST), Dkt Harrison Mwakyembe amekabidhi ripoti na kuanisha changamoto ambazo ni miongoni mwa vikwazo katika kupata wanafunzi bora wanaosomea fani ya sheria.

Kamati hiyo yenye wajumbe saba iliteuliwa Oktoba 12, 2022 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro na kufanya kazi kwa siku 30 kufuatilia sakata la kufeli kwa wanafunzi wengi wa taasisi hiyo ya sheria.

"Uwezo mdogo wa wanafunzi wengi wanaoruhusiwa kusoma sheria na baadae kujiunga na Taasisi katika kumudu lugha ya kufundishia ya Kingereza, tatizo hili lina athari kubwa sana katika uelewa wa masomo na kujieleza," imeeleza taarifa ya kamati.

Aidha, changamoto nyingine ni, "Vyuo vingi vya sheria nchini, kutozingatia masharti ya uwiano kati ya walimu na wanafunzi, sifa za waalimu na idadi yao na piramidi ya elimu.”

Kamati hiyo iliyoongozwa na Dkt Mwakyembe ilibaini changamoto nane ni za kimfumo na kisera na hivyo utatuzi wake hauna budi kuwa wa kimfumo na kisera.

Chanzo: EA Radio
 
... kati ya kozi zinazo-admit wanafunzi wenye highest grades ni sheria. Tatizo litakuwa huko huko vyuoni hususan kweye ufundishaji. Kwamba itake nzima ya LST ilifeli ni indicator tatizo ni ufundishaji vyuoni - lecturers wanawaingiza wanafunzi chaka.
 
VILAZA wataenda wapi kama Huko kwenye Sheria wamechemka? Maana sikuhizi kilamtu anajiita msomi ILIMRADI amevaa shati, tai na suruali ya kitambaa
 
View attachment 2422326
Kamati ya kufuatilia mwenendo wa matokeo ya mitihani ya mafunzo ya uansheria kwa vitendo (LST), imeanisha changamoto nane ikisema ni miongoni mwa vikwazo katika kupata wanafunzi bora wanaosomea fani ya sheria.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Harrison Mwakyembe amesema changamoto hizo pia zimelalamikiwa na LST pamoja na wadau mbalimbali wa sheria.

Dk Mwakyembe ameeleza hayo leo Jumapili Novemba 20, 2022 wakati akisoma muhtsari wa taarifa ya kamati hiyo kufuatilia chanzo cha wanafunzi wengi kufeli katika mitihani ya mafunzo katika taasisi ya LST.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro, katibu mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mary Makondo, wajumbe wa kamati hiyo pamoja viongozi waandamizi wa wizara hiyo.

Kamati hiyo yenye wajumbe saba iliteuliwa Oktoba 12, mwaka huu na Dk Ndumbaro na kufanya kazi kwa siku 30 kufuatilia sakata la kufeli kwa wanafunzi wengi wa taasisi hiyo.

Sakata hilo lililoibuliwa na Mwananchi, lilitokana na matokeo ya awamu (Cohort) ya 35 ya wanafunzi wa taasisi hiyo, kuonyesha kati ya wanafunzi 633 waliofanya mtihani huo, ni 26 ndio waliofaulu kwa awamu ya kwanza.

Katika matokeo hayo, wanafunzi 265 walifeli (discontinue) na wengine 242 walitakiwa kurudia mtihani (supplementary).

Akitoa taarifa hiyo leo, Dk Mwakyembe amesema udahili wa wanafunzi wengi kupita uwezo katika vyuo vinavyofundisha sheria na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo unasababisha uwiano mbaya kati walimu na wanafunzi na kuathiri ufundishaji na usimamizi.

Pia Dk Mwakyembe ambaye ni waziri wa zamani wa Katiba na Sheria amesema kumekuwa na uhuria usio kuwa na tija kwa kila chuo kuwa na uhuru wa kupanga muda wa kukamilisha shahada ya sheria kati ya miaka mitatu au minne.

"Pia uwezo mdogo wa wanafunzi wengi wanaoruhusiwa kusoma sheria na baadaye kujiunga na LST katika kumudu lugha ya kufundishia ya kiingereza.Tatizo hili lina athari kubwa katika uelewa wa masomo ya kujieleza," amesema Dk Mwakyembe.

Mbali na hilo, amesema uamuzi wa Tume ya Vyuo Vikuu kushusha vigezo vya ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita kutoka alama nane (B mbili kwa masomo mawili hadi alama nne ( D mbili kwa masomo mawili kulikowezessha vijana wasiokuwa na uwezo kusoma masomo ya sheria.

Dk Mwakyembe mbunge wa zamani wa Kyela mkoani Mbeya amesema utatuzi wa changamoto hizo upo kisera na kimfumo. Amesema mfumo wa bora wa elimuT ya sheria unasimamamiwa na ule uanasheria kwa vitendo unasimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria nchini (CLE).

Amesema kamati inashauri kufufuliwa kwa CLE na kuliwezesha kutekeleza majukumu yake ikiwemo kukaa chini na TCU kupandisha vigezo vya ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na nne kwa wanaotaka kusomea sheria vyuo vikuu.

"Kuanzisha mtihani maalumu wa kuingia LST kama ilivyo kwa wenzetu wa Afrika Mashariki ambao utasimamiwa na CLE, " amesema Dk Mwakyembe.

Dk Ndumbaro amesema, “leo tumepokea taarifa tunakwenda msituni, tutapitia changamoto kwa changamoto zilizoanishwa katika taarifa ya kamati hii” Dk Ndumbaro

MWANANCHI
D mbili form 6 🤯🤯 siku hizi unasoma sheria!!!!!Zamani ukiona mtu anasoma sheria au medicine au engineering au economics au accounts au computer science, ujue alikuwa kichwa kweli kweli shuleni.
 
Back
Top Bottom