Dawasco Yamwomba Radhi Dr. Mwakyembe

LazaroSMtindi

Senior Member
May 6, 2008
100
5
Katika kipindi cha Bunge leo jioni mjini Dodoma, DAWASCO kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, imemwomba radhi Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe kwa kumtangaza kuwa alijiunganishia maji kinyume cha sheria, kitu ambacho hakikuwa cha kweli. Tamko hilo la Wizara lilikuja baada ya Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo, kuishutumu vikali DAWASCO kwenye kikao cha ahsubuhi cha Bunge kwa kujiingiza katika siasa na kuwazulia watu kashfa. Shellukindo, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki pamoja na Dk.Mwakyembe, aliishutumu DAWASCO kwa kutumiwa na kuchafua jina la Dk. Mwakyembe aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Richmond iliyofanya maamuzi ya kihistoria Tanzania na kusababisha Lowassa kujiuzulu. Lazaros
 
Katika kipindi cha Bunge leo jioni mjini Dodoma, DAWASCO kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, imemwomba radhi Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe kwa kumtangaza kuwa alijiunganishia maji kinyume cha sheria, kitu ambacho hakikuwa cha kweli.

Hawa mafisadi wasipokemewa na kuchukuliwa hatua za kisheria, watatusumbua sana hili taifa, yaani sasa wameingia hata kwenye maji tena?

Je next wataibukia wapi hawa? Shujaaa wa taifa Mwakyembe akaibe maji? Yaani hawa mafisadi wameishiwa hoja kama kina flani humu ndani?
 
..na wengine humu humu wakakurupuka kumwita Dr Mwakyembe fisadi. Sijasahau!
 
Kwa mtaji huu CCM sasa ni sawa na kichaka, kilicho stawi kwa ukijani mbichi, karibu na stand isiyo na Choo.

Kila ajisikiaye haja aenda huko. Uoza, Harufu kali, Mainzi na kila aina ya kinyaa ndo kwao.

Wote ndani ya CCM wanaupenda ukijani, lakini hawakipendi kabisa kiupacho ukijani kichaka chao, yaani mashonde yanukayo.
Dawa ni kufunga pua na midomo na kujitoma na majembe surululu na nyengo na kuusafisha uchafu wote, zaidi kung'olea mbali kichaka kile na mahali pake kuchimba choo na kisha kujenga tabia ya kukitumia.

Haya, shauri yenu wenyewe, Mbolea ikizidi sana kichaka kitaungua.
 
Ha ha haa!! Lakini una hakika gani na hayo maneno in bold. Nijuavyo mimi ni hiyo harufu ya uvundo ndio inaowavuta makada kwani bila kufanya hivyo watagangaje njaa yao.
 
Pole Dr Mwakyembe kwa kudhalilishwa....mimi kwangu wewe bado ni shujaa sana tu tena sana
 
Aisee MDELA-WA MADILU UMERUDI kamanda, aisee karibu sana Kamanda, kijiwe kiliukumiss sana hapa, ilikuwaje mzee ukapotea?. naona sasa kijiwe kinazidi kukamilika maana kumbe makamanda hawakutekwa kumbe walikuwa chimbo wanatafakari stratergy za kuumaliza uadui
 
Katika kipindi cha Bunge leo jioni mjini Dodoma, DAWASCO kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, imemwomba radhi Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe kwa kumtangaza kuwa alijiunganishia maji kinyume cha sheria, kitu ambacho hakikuwa cha kweli. Tamko hilo la Wizara lilikuja baada ya Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo, kuishutumu vikali DAWASCO kwenye kikao cha ahsubuhi cha Bunge kwa kujiingiza katika siasa na kuwazulia watu kashfa. Shellukindo, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki pamoja na Dk.Mwakyembe, aliishutumu DAWASCO kwa kutumiwa na kuchafua jina la Dk. Mwakyembe aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Richmond iliyofanya maamuzi ya kihistoria Tanzania na kusababisha Lowassa kujiuzulu. Lazaros

Namna waliyoitumia kuomba radhi bado haijaniridhisha, inamaana bila Mhe.Beatrice Shellukindo, Mbunge wa Kilindi, kuwawakia wasinge omba radhi. Pia inaonyesha kwamba Wizara ilikuwa inatambua kitendo hiki kibaya ambacho DAWASCO ilikifanya ndiyo maana Mhe. waziri/Naibu waziri hata hakuhitaji muda wa kuwasiliana na wahusika bali alikuwa na jibu kwenye incha za vidole vyake. Ni mbaya sana.
 
Halafu nilisema yule Badra anatumiwa..........watu wakasema oooh unamuonea dada wa watu.................sasa kapata ajira mpya Tanesco baada ya kukamilisha kazi yake ya kuchafua watu akiwa DAWASCO...........

....I know Badra......haikuwa fair kwake kuingia ktk mchezo ule........ile tabia inamtafsiri vibaya sana....................anyway ndivyo waandishi wetu walivyo
 
Mimi nadhani rekodi zimewekwa wazi... waongo watakaangwa tu hata kama sio leo lakini siku yao ipo...

Yupo mchangiaji makini amekuwa anatupeleka anavyotaka lakini sasa hivi mambo yanamwakia kwenye thread nyingine...

Kwa hiyo Tunashukuru Issue ya Dr. Mwakyembe na DAWASCO iko wazi, Issue ya Dr. Slaa na TBC1 iko wazi.

Muda si muda issue ya Dr. Masau na NSSF itakuwa wazi.
 
Walishamchafua Dr Mwakyembe na akachafuka, hiyo radhi wanayoiomba sasa hivi inaombwa wakati wengine walisham-judge Dr Mwakyembe kuwa ni miwizi wa maji, tena baada ya kuamua hivyo, hata huu msamaha ulioombwa hawatauona wala kuusikia, hivyo wataendelea kuamini kuwa mwakyembe ni mwizi wa maji
 
Jana nimemtafuta sana kwa simu sikumpata, lakini nikawapata wabunge wenziwe walo karibu sana naye including Beatrice mwenyewe, wakaniambia this is big joke kwa sababu kwanza hiyo nyumba wala sio yake, amepewa tu hivi karibuni na serikali,

Mimi sikuiona topic yake hapa nasikia ilitolewa haraka sana, lakini nasikia kuna waliojkaanga sana kwenye hiyo topic kwa kumuhukumu bila facts zote, tena nasikia kuna hata wakulu flani hapa walihusika na hizo hukumu, lo! aibuuu!
 
FMES,

Mimi pia nilimhukumu Dr. Mwakyembe kwa kufuata facts ambazo zilikuwepo. Hivyo ndivyo ambavyo tumekuwa tukifanya safari zote, kutumia facts zilizopo mpaka ukweli mwingine ukijulikana.

Wanaotakiwa kumwomba msamaha ni hao DAWASO ambao ndio walimtuhumu.

Mimi namfahamu vizuri huyu mheshimiwa ila pia sikuona shida kulaani hicho kitendo cha
kutumia maji bila kulipa. Hapa tunamlima nyani geledi. Tukianza kuangaliana usoni, tutapoteza mwelekeo.

Ni vizuri DAWASO wamemuomba msamaha ila sidhani kuna haja ya wana JF kumwomba msamaha kwa mambo ambayo watu tuliandika tukidhania ndio ukweli.

Kama ni hivyo basi hapa kila siku tutakuwa tunaomba msamaha maana kuna mambo mengi mno yameandikwa baadaye inakuja kuonekana ukweli hauko hivyo.

Tatizo la Tanzania hasa kwa vyombo vya serikali ni kukurupuka. Uhusiano wa DAWASO na Mwakyembe au Tanesco na mtu mwingine ni wa supplier na client. Inatakiwa kabla hata ya kufikia hatua ya kwenda magazetini au kukata huduma, wawe wamefanya mahojiano na mhusika. Mambo mengi yanaweza kutatulika kwa mazungumzo, sio muhimu wakati wote kutumia nguvu.
 
Mimi pia nilimhukumu Dr. Mwakyembe kwa kufuata facts ambazo zilikuwepo. Hivyo ndivyo ambavyo tumekuwa tukifanya safari zote, kutumia facts zilizopo mpaka ukweli mwingine ukijulikana.

Mkuu Mtanzania,

Heshima mbele mkuu, mimi skuiona hiyo topic, lakini ninashukuru kuwa umejitokeza kuwa ulikuwa ni mmoja wa waliokurupuka, sasa the right thing ni kuomba radhi kwa kukurupuka,

Hiyo excuse hapo juu, ni dhaifu sana kwa sababu tunapaswa kuwa na standards za kuwangalia viongozi wetu, kuna wasiostaili utafiti kabla ta kutoa hukumu na kuna ambao ni lazima kwanza tufanye utafiti kabla ya kurusha hukumu wanapotajwa,

Mimi kwa haraka haraka, viongozi kama Mwakyembe, Zitto, Dr. Slaaa, Mama Kilango, Seleli, Sendeka, Beatrice, Kaduma, hata siku moja siwezi kudandia treni bila kuwa na facts kwanza on them, mkuu hapa ulichemsha sasa dawa ni kuomba radhi tu kwa wana-forum wengine, lakini ninaheshimu kitendo chako cha kujitokeza mwenyewe!
 
Hata kusema watu walikurupuka ni makosa makubwa. Hiyo habari ilitolewa gazetini ikiripoti taarifa ya DAWASO na watu tukachangia. Ni facts zipi zaidi utazitaka hapo kabla ya kutoa comments zako?

Ukisema hivyo basi gazeti litaomba msamaha na watu wote waliochangia wataomba msamaha.

Sidhani kama hilo sahihi wala kwenye hili la Dr. Mwakyembe binafsi sioni sababu wala sina nia ya kumuomba msamaha mtu yeyote.

Hiyo habari ilitoka idara ya serikali wala haikuandikwa kama udaku.

Wanaotakiwa kumwomba msamaha Mwakyembe ni hao waliotoa hiyo taarifa na wala sio watu ambao walitoa comments zao wakijua hiyo habari ni sahihi.

Pia bahati mbaya mimi sina list ya watu ambao naamini ni wasafi mno kiasi kwamba kukitokea kashfa zao naweza kushangaa au kushindwa kuchangia. Wanaweza kuwa wamefanya jambo moja ama lingine la maana na wanapongezwa kwa hilo lakini kama kuna jambo ambalo litaonekana wamefanya tofauti tutawalima pia bila kuangalia majina yao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom