KERO Mamlaka ya Maji Kibaha kuna urasimu mkubwa sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ukiomba kupata huduma ya kuunganishiwa maji DAWASCO Kibaha, uwe umejiandaa kifedha.

Zoezi linaanza kumpata surveyor, bila elfu hamsini hatafika site. Ukishatoa hiyo hela na surveyor akapima zoezi. linalofuata ni kuingizwa kwenye mifumo yao hatimae upate Control Number kwa ajili ya kulipia huduma ya kuunganishiwa maji.

Zoezi la kuingizwa kwenye mfumo bila Sh. 20,000/= faili lako litakaa mezani miezi nenda rudi.

Ukishatoka hapo faili linapelekwa kwa injinia wa maji ili kupatiwa control Number, bila 30,000/, utasubiri mpaka uchakae na ukipata kupewa vifaa na fundi hapo bila 50,000/ utasubiri mpaka uchakae.

Kwa sasa wameanzisha utaratibu wa kuandika barua kuomba control Number kwa muongozo wanaotaka wao ili kujifunga kimaelezo hii wanatengeneza mazingira ya rushes.
 
Yuko fundi mmoja supervisor hapo Kibaha, maeneo yake ya kazi Ni kuanzia kongowe Hadi Vikuge na Soga.

Kabila mhaya, anatembelea Bajaj ya dawasco. Huyo Ni kinara wa rushwa, Kuna kipindi alipigwa na raia kwa sababu ya urasimu na kulazimishwa rushwa.
 
Kwakua mpokeaji na mtoaji rushwa wote wanamakosa, ngoja nikae kimya
 
Kwa sasa wameanzisha utaratibu wa kuandika barua kuomba control namba kwa muongozo wanaotaka wao ili kujifunga kimaelezo hii wanatengeneza mazingira ya rushes
 
Back
Top Bottom