DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Utaratbu wenu wa kudai bili kwa vitisho katikati ya mwezi ni mbovu sana.
 
Naomba kujua gharama za kuunganishiwa Maji mana nimeenda kila Mara naambiwa mpaka nifanyiwe servey..then ndo ntatajiwa bei kulingana na umbali wa bomba na mm nilipo...ila mm napatikana ndani kama ya mita Mbili tu kutoka kwa bomba la Maji ma nyumbani kwangu.....wananizungushaaa mpaka nakosa Amani
 
Habari za asubuhi DAWASCO. Mimi ni mkazi wa Kinondoni Kata ya Wazo, siku za karibuni tumepata Neema ya maji katika maeneo ya Salasala. Hata hivyo waunganishaji wa mabomba ya maji hawakuunganisha vizuri kiasi cha kufanya maji kuvuja na kusambaa barabara na kuisababishia serikali hasara. Nilijaribu tarehe 23/2/2019 kupiga namba za simu za Tegeta (0743451881) mara kadhaa ili kuwajulisha zilikuwa hazipokelewi. Naomba sasa baada ya kupata taarifa hii mpite maeneo mliyosambaza maji na kukagua hali ilivyo ili mfanye marekebisho.
 
Jamani ninyi DAWASCO kule Mbezi Maeneo ya Malamba Mawili ni lini mtatuletea mabomba ya maji na maji yatoke ?? Tuna shida sana ya maji sana jamani maana tunasikia tu sasa hv mnazalisha maji mengi sana lakini wenzenu tunateseka tunanunua maji ya kwenye Magari Zaidi ya miaka mi nne sasa, maji hayo hayana uhakika siku nyingine wanakuletea ya chumvi mara hatujui hata vyanzo vyake, tunawaomba jamani muongeze kasi ya kutusambazia maji, uwezo wa kulipa tunao maana kama kwa sasa naweza kununua maji kwa mwezi mmoja natumia Tzs 150,000/ ntashindwaje kulipia maji yanayotoka katika bomba ambayo bili zake huwa sio kubwa kiasi hicho. Tunawaomba sana kaeni chini DAWASA Kimara mtufikilie
 
.. you Kirk you can see the statue is no a p this mail but Problems with hukurudi dar huu I have .. Re u.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I used to be

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu wa dawasa hii meseji inatoka kwenu au ni matapeli wapo .
 

Attachments

  • dawasa.docx
    36.8 KB · Views: 28
ENG.CYPRIAN TUNAKUHOJI NI LINI MAENEO YA MBEZI MSHIKAMANO,KIBAONI,KANISAN KATOLIKI MBEZI MSHIKAMNO,FABIANI ROAD MPKA KWA ASENGA YATAPATA MAJI YA DAWASA ....MABOMBA MMEYALAZA 2017MWISHONI SASA 2019 TONE LA MAJI HAKUNA KWENYE MAKAZI.
 
Mimi nawapongeza sana DAWASA kwa jitihada mlizofanya za kuhakikisha yale maeneo yaliyokuwa sugu kwa upatikanaji wa maji sasa yanapata maji mfano hapa Mbezi kwa Muguri. Hata hivyo kuna changamoto kadhaa ambazo itabidi mzifanyie kazi. Kuna watu wanamita zile za mwanzo walizowekewa na wachina lakini hazijawahi kusomwa isipokuwa wanatumiwa bill kwa kukadiria. Ni vizuri mngefanya scouting kila nyumba kujiridhisha kama mita zipo na zina somwa kwakuwa wengine wanatumia maji lakini hawajawahi kupewa bili. Mfano mimi nililetewa bili ya 868,348/= nikasoma mita yangu nikaenda Dawasa wakarekebisha nikajikuta nadaiwa 12,586
Jambo la msingi ni kuwa mtoe elimu kwa wateja wawe na uwezo wa kusoma mita zao na kuleta units Dawasa pale wanapokuja kulalamika kuzidishiwa bili kitu ambacho kinatokana na kutosomwa kwa mita au wanapoona mita haisomwi ili wasije kudaiwa deni kubwa. Kuna jirani yangu hapa alikuwa anatumia maji mita haisomwi walipokuja kusoma akajikuta anadaiwa 608,538 maana uniti zilikwenda zaidi kwa kuachia maji watu wachote kama ya kijiji na kutoka kwenda Dawasa. Kwakuwa hana uwezo wa kulipa hizo amekatiwa maji.

Jingine ni kupita kila kwenye mtandano wa bomba ili kuzuia maji yanayovuja kutokana na bomba kupasuka au shughuli za kibinadamu ambazo husababisha mabomba kupasuka na kuziba.

Asanteni!
 
Tabata kifuru lini maji tutapata?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu wa Dawasco. Sisi wakazi wa Mbezi MWISHO maeneo ya Peter Selasini tunapata tabu sana ya kukatiwa mabomba yetu na walima mchicha. It's a big problem. Kwa nini hamuwafuatilii hawa Watu? Idara yenu ya usalama inafanya kazi gani? Wananchi tumewapiga bit LA nguvu sasa maji wanakata usiku saa nne halafu wanaunga. Mnafanya kazi gani lakini? Lita za maji kibao zinapotea mmekaa ofisini tu. CEO act on it!
Tabata kifuru lini maji tutapata?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kujua ni lini mtaanza kuwaunganishia maji wakazi wa Saranga Mwisho? Kwani tokea mmeweka mabomba na kuwajazisha form wananchi hakuna kinanchoiendelea mpaka sasa.
 
DAWASCO tunapenda kujua lini mtaunganisha maji..wakazi wa BUNJU A MAENEO mkabala na nyumba za TBA...TUMESHAJAZA FORM NA TUMELIPIA MAMITA YAMESHAFUNGWA NJE..LAKINI MAJI HAKUNA..HII IKOJE..TOKA MWAKA 2018
 
Mkuu umeniwahi nilishakuja hapa kuwauliza hawa DAWASA maana mimi nipo hapo jirani na kwa Moshiro 'mjeda' mtaa wa Senzele kwa mjumbe Swai right uelekeo wa mradi wa TBA ...kweli kabisa tumelipa maji hakuna DAWASA njooni mtupe jibu hapa hii ishakuwa kero kabisa
DAWASCO tunapenda kujua lini mtaunganisha maji..wakazi wa BUNJU A MAENEO mkabala na nyumba za TBA...TUMESHAJAZA FORM NA TUMELIPIA MAMITA YAMESHAFUNGWA NJE..LAKINI MAJI HAKUNA..HII IKOJE..TOKA MWAKA 2018

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hii kampuni jina lake hasa ni lipi kati ya haya; DAWASA au DAWASCO? which is which?
 
NILILIPA SHS.462,000 KWA AJILI YA KUUNGANISHIWA MAJI KIMARA BARUTI BAADA YA SURVEYOR KUFANYA SURVEY. IMEFUNGWA METER KWENYE LILE ENEO LAKINI TANGU ILIPOFUNGWA HALIJATOKA HATA TONE MOJA LA MAJI. MAJIRANI WOTE WANAPATA MAJI LAKINI KWANGU HAKUNA. NIMEAMBIWA ILE METER ILIFUNGWA KWENYE BOMBA LA MAJI LA ZAMANI AMBALO HALINA MAJI. NIMETUMA MALALAMIKO DAWASA NA HADI WIZARANI LAKINI HAKUNA ANAECHUKUA HATUA.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIVI DAWASCO MTATUTATULIA LINI TATIZO LA MITA.TUNAKUWA WA WAPANGAJI WENGI NA TUNAHITAJI METER KWENYE ENEO MOJA.MFANO UNA JENGO LINA APARTMENT 3 KILA MTU ALIPE KADRI YA MATUMIZI YAKE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…