DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Naomba kujua mteja mpya anatakiwa kulipa shilingi ngap afungiwe maji,eneo ni Kimara mwisho karibu na lukundo lodge
 
Tatizo kulipa bill ya maji kwa kutumia simu. Transactions unavailable, kuna tatizo gani?? Account yangu 90086494 nipo Kerege ccm Bagamoyo. Jina ni Joseph Abdala Lebai
 
Dawasco watoe vyeo kufuatia elimu za wafanyakazi wake,inaleta shida eti mtu ana diploma ndio anakuwa meneja wa kituo au wilaya halafu mtu ana digrii yake anakuwa msoma mita tu,hii inawavunja moyo wa kufanya kazi
 
Dawasco watoe vyeo kufuatia elimu za wafanyakazi wake,inaleta shida eti mtu ana diploma ndio anakuwa meneja wa kituo au wilaya halafu mtu ana digrii yake anakuwa msoma mita tu,hii inawavunja moyo wa kufanya kazi
....majungu !
 
Mbona hamjibu wengine? Nlituma ujumbe humu nataka nipatiwe huduma ya maji gharama yake ni tsh ngap?majibu tafadhali,
 
DAWASCO, kwa sasa tunatumia njia gani kulipia bili za maji? Nimejaribu kupitia simu ila huduma haipatikani, pesa inarudi. Nimeenda kwa wakala kaniambia mmejitoa!
 
Dawasda
Mbona haujibu au unakunywa kahawa

 
Dawasco mimi nina shida bomba la mtaa wa feza nyuki road huwa linakatika ni kutokana na lipo barabarani na magari hukanyaga kwahiyo maji yanamwagikaga mengi mno mpk panafurika sasa dawasco wenyewe wanapita hapo hapo na wanaona mimi nimesha litengeneza mwenyewe maana ukiita mtu wenu hatokei.sasa last week hatimaye wakatokea mafundi mara wakasema tuwalipe 30000 kwa ufundi hivyi kwanini mnakuwa hivyo toka lini mnaomba mlipwe kwa kazi yenu na ni bomba lipo barabarani sasa tutaanza wapiga picha na kuwaanika
 
Kama ndio nifikiriavyo basi huu ni Mfumo mbovu sana. Kila mwezi mnanitumia kumbukumbu namba nyingine?? Nikiipoteza hiyo kumbukumbu namba ndio nianze tena kulimbikiza madeni au nianze kuja kuja ofisini kwenu kufuatilia??
Itapendeza kila mteja awe na kumbukumbu namba ya pekee na ya kudumu. Mfumo huu wa malipo ya bili UNATAKIWA UWE USER FRIENDLY KWETU SISI, sio nyie, kama ukiwa kwa wote basi vizuri ila kipaumbele ni sisi! Nyie mjipange, sasa nashangaa mnakuwa na mfumo ambao ni user friendly kwenu badala ya kuwa user friendly kwetu sisi. Nimejaribu kulipa bili nimekwama kisa sijatumiwa bado kumbukumbu namba, mfumo mbovu sana huu.
Labda kama sijaelewa huu mfumo mpya wa malipo, ebu nielewesheni.
DAWASCO
 
Naomba kujua taratibu za kubadili jina, kiwanja nilipewa na mtu(sikununua) na bomba lilikuwepo sasa nataka lisome kwa jina langu maana nakereka napolipia jina lisilo langu. Nipo Mlandizi kibaha
 
Nakuunga mkono mfumo mbovu kuwahi kutokea yani kulipa bili ni kazi balaa. Tatizo huwezi lipia kidogo ukilipa no inakua haitumiki mpaka upate no ingine nimechukia sn
 
habari ya Leo naomba kuuliza swali.. endapo bomba la maji la nchi 4 likipita katikati ya kiwanja cha makazi ya mtu utaratibu wa kuliamisha unakuwaje ?
 
Kuna tatizo kuhusu mfumo MPYA wa kulipia bili kwa kutumia reference number yenye tarakimu 12. Mfumo haukubali kulipia kwa Simu kama tunavyoambiwa. Nilijaribu Mara NNE kulipia kwa tigo pesa! Unafuata hatua zote mpaka kuweka mamba ya siri lakini bado malipo hayafanyiki. Mpaka nikalazimika kwenda kulipia CRDB kwa kupoteza pesa kwa kulipa nauli na kupoteza muda kwenye foleni!! Huu mfumo haufai!!!
Pili reference number ingekuwa ni moja tu kwa kila MTEJA kwa muda wote kuliko hii ya kupewa reference number MPYA kila mwezi.
Tatu, pamoja na kuwa wana namba Yangu nilisubiri reference number kwa miezi miwili bila mafanikio mpaka nikalazimika kwenda ofisini kwao!!!!
Warudishe mfumo wa mwanzo uliokuwa rafiki zaidi wa kutumia akaunti namba ambapo tulikuwa tunalipia kwa Simu bila matatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawasco ntapataje kumbukumbu namba kwa ajili ya malipo nwezi huu? Message mlotuma imefutika ...
 
Dawasco mnatumia akili zipi kukata maji eneo flani kwa miezi 2? Madale ni wahanga wakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…