Dar: Kukosekana huduma ya maji kwa wateja Kimara Stop Over hadi Kibanda cha Mkaa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
TANGAZO LA DHARURA

22.1.2024

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na wananchi wa eneo la Kimara Stop over hadi Kibanda cha Mkaa kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kutokana na matengenezo ya bomba la inchi 24 eneo la Kibanda cha Mkaa lililoathiriwa na mvua.

Maeneo yanayoathirika ni;
Kimara Stop over, Kimara Suka, Kimara Temboni, Kwa Msuguri, King'ong'o na Kibanda cha Mkaa

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza na Mamlaka itaendelea kutoa taarifa za uimarishaji wa huduma mara kwa mara kupitia makundi songosi (whatsap) za wateja na mitandao ya kijamii.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202-121(WhatsApp tu)
0735 451 865 (DAWASA Ubungo)

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano

 
Back
Top Bottom