Dawa ya kuondoa tatizo la mtoto kupata degedege

bulabo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
620
759
Mtoto wangu miaka(4) alipatwa na homa mwaka Juzi 2021 mwez wa 11. Joto ilikuwa juu sana mpaka ikamsababishia dalili za degedege kutokwa na povu mdogo.

Tulimpa Panadol kushusha homa na kumkimbiza hospitali ikaonekana ana infection kwenye damu akapatiwa dawa akapona. Mwezi ulioisha tena alipata kihoma fulani joto likapanda ikamtokea tena hii kitu. Je shida nini

Tatizo limejirudia mwez ulioisha Jan 2022 ni kama mwaka umeisha sasa hajapatwa na tatizo kama hilo tena.

Dawa gani nitumie asipatwe na hili tatizo...
 
Hospital ikigonga mwamba unaenda mbadala Mkuu!

SIO KILA ugonjwa hospital wanatibu ndio maana kuna kitengo cha tiba asili hospital!!
 
Kutoka na povu, pole Ila ukweli kifafa ndio wanatoa povu, tegedege, anageuza macho na kukakamaa au kuzubaa.
 
Mtoto wangu miaka(4) alipatwa na homa mwaka Juzi 2021 mwez wa 11. Joto ilikuwa juu sana mpaka ikamsababishia dalili za degedege kutokwa na povu mdogo.

Tulimpa Panadol kushusha homa na kumkimbiza hospitali ikaonekana ana infection kwenye damu akapatiwa dawa akapona. Mwezi ulioisha tena alipata kihoma fulani joto likapanda ikamtokea tena hii kitu. Je shida nini

Tatizo limejirudia mwez ulioisha Jan 2022 ni kama mwaka umeisha sasa hajapatwa na tatizo kama hilo tena.

Dawa gani nitumie asipatwe na hili tatizo...
Kama ni mtoto wa kike, boresha usafi wake na epuka kumvalisha pampers. Most likely anasumbuliwa na UTI za mara kwa mara.

Kama ni kidume, mfanyie tohara haraka. Inasaidia kupunguza maambukizi ya UTI kwa watoto.
 
Kumbe hizi pampers zinasababisha uti mkuu, nilikuwa sijui hili, binti yangu kila siku ni lazima alale na hayo makitu
 
Back
Top Bottom