Dawa Ya Kiranja Mnoko Shuleni

Dawa Ya Kiranja Mnoko Shuleni

Tuliosoma kusini hatukuwa na cha kupasha maana mbaazi ikilala inageuka kuwa "mawe" ukiweka kwenye manati unatungua njiwa. labda tumeotea mafuta kidogo unasubiri wamalize kugawa mnazama jikoni kasufuria cha mbaazi unakaanga mafuta unamiminia hapo ukila unahisi inakula maharage.
 
Hahha mkuu umenikumbusha mbali sana tulikuwa tunachukua jometri na kujaza mchanganyiko wa unga wa mahindi na sukari kisha kuweka chini ya mkaa yaani (kusuvika mofa)hiyo inaitwa mofa rombo kilimanjaro hiyoo si mchezo
 
daaah watu8 kaazi kwelikweli
 
Last edited by a moderator:
Maisha ya boarding raha...huo mzinga umenikumbusha mbali...hahaha
 
Hivi huko boarding mlikuwa na privacy yoyote? Mabafu ya ku-share? Vyoo je? Mlikuwa mnalala kwenye vyumba vyenu wenyewe au li-hall tu lenye mavitanda kibao?

Maisha gani hayo...!!!
 
dah maisha ya boarding raha sana wadau! Kuna jamaa yeye alikuwa hana bakuli la uji wala sahani, anachofanya akitoka likizo anakuja na ma trunker km matatu hivi, moja la ngun jingine kuna mazagazaga ya breakfast kajaza sugar ten kilos, blueband kubwa km nne hivi, jam, roiko mchuzi mix za kumwaga.

Jingine kajaza samaki flani hivi ni tilapia aka perege hawa wa kawaida lkn kwa sababu wanatoka bwawa la Nguruka Kigoma wakihifadhiwa kwa chumvi nyingi baada ya kukaangwa na mafuta ya mawese, kwa ufupi wanaitwa nguruka, mchizi anajaza trunker lote. Anachofanya yeye wakati wa uji saa nne anatoka na blue band yake na sukari kidogo sana, akiingia mesini watu wanamgombeaje! Anapewa bakuri la uji yeye anawapa sugar kidogo na blueband ya kudabia wengine mliomkosa mnaendelea na uji Sumu wenu kimyamkimya.

Mchana wakati wa makana yaani ugali dagaa mchizi anaibuka na nguruka wake mmoja, hana sahani hapo wala hapangi foleni ya msosi watu wakisikia tu harufu ya nguruka, ugomvi wanamgombea jamaa.

Nilienda na ka kikombe ka chai form one jamaa wa form two walipokiona wakaniuliza kakikombe ka nini niliposema chai jamaa alicheka akasema chai ni dawa ya kutolea mimba kwa hiyo hairuhusiwi kunywewa pale shule km nna pakti lake nimpe akatupe kwa uwoga nikampa, usiku saa tatu natoka kuoga nikawafuma jamaa angle moja bwenini wanachemsha chai kwenye ndoo zile za bati kwa kutumia zile heater za coil pembeni lile boksi langu la green label limeshafunguliwa hahaa jamaa kuniona akakauka kimya. Kesho yake akaja kunipa bakuli kubwa km yale wanayonawishia maji kwenye vitimotoz eti ananikopesha wakati ule eti kila siku ntampa shs hamsini dah boarding si lelemamaa
 
wakati nasoma kuna mmoja aliwahi kumwagiwa kinyesi kilichochotwa kwenye chamber tena alikikua kiranja mkuu mnoka kama nyapara
Sidhani kama kulikuwa na head prefect mnoko Tanzania nzima zaidi ya Batanisha Sukume. Huyu alikuwa ni zaidi ya Headmaster.
 
Mpwa umenikumbusha enzi mbaaali sana. Umenifanya niikumbuke shule yangu pendwa, Moshi Technical.
 
Hahaa mi nakumbuka kuna jamaa alikuwa mchoyo wa sikari yake siku moja jamaa wa kauchukua mzinga wake wakaanza kuuroll upside down kwa nguvu jamaa alikujakuta sukari imejaa kwenye nguo zilizokuwa kwenye mzinga
 
Umenikumbusha sisi tulikuwa tunaanika pilau kwa jua (pilau halichachi), uporo wa ndizi na wali ulikuwa unaliwa hivyo hivyo bila kupaswa; ilmradi chai ni ya moto.
am sorrrry wewe uko kidijitali zaidi. Sijawahi kula pilau shule. Ndizi? Duh
 
Mimi nlikuwa nadeki akajipitisha halaf mvua tope sasa jekunduu la moshi nikaroweka dekio vizuurii halaf nikamuwasha la mgongoni mwenyewe ashaulambia aende church yupo form 4 mi nipo form 2 yani aliliaaaa
 
Mpwa umenikumbusha enzi mbaaali sana. Umenifanya niikumbuke shule yangu pendwa, Moshi Technical.

Mpwa unakumbuka hekaheka za Mwl Mpande...sijui kama alikuwepo time unasoma
 
Back
Top Bottom