Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,934
- 16,573
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeunga mkono na kufungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Kanda Kuu Dodoma) kupinga uhalali wa matumizi ya adhabu ya viboko shuleni. Kesi hii imewasilishwa kwa niaba ya Samwel Maduhu Mangu, mlezi wa marehemu Mhoja Wilson Maduhu, mwanafunzi wa Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari Mwasamba mkoani Simiyu. LHRC inamwakilisha mlalamikaji kama sehemu ya jitihada zake endelevu za kulinda haki za watoto na kuhakikisha mazingira ya kujifunzia yanakuwa salama na yenye heshima.
Kesi hii inapinga Kanuni ya 2, 3 na 6 za Kanuni za Elimu (Adhabu ya Viboko), GN. Na. 294 ya 2002, kwa hoja kwamba zinakiuka Katiba hususan haki ya heshima na utu, haki ya kusikilizwa, na haki ya kuwa huru dhidi ya mateso au adhabu au matendo ya kikatili au ya kudhalilisha. Shauri hili linatokana na tukio la kusikitisha ambapo Mhoja na wenzake waliadhibiwa kwa kutokamilisha kazi ya somo la Jiografia kinyume na maelekezo ya walimu. Mhoja alipigwa mara kadhaa kwa fimbo, zikiwemo viboko viwili kichwani alipokuwa akijaribu kujikinga. Alianguka chini, hali yake ikazidi kuwa mbaya, na licha ya kulia kwa maumivu, mwalimu aliendelea kumsukuma kichwani ili amnyamazishe. Alikimbizwa hospitalini lakini alifariki dunia. Ripoti ya uchunguzi wa mwili ilionyesha kuwa alikufa kutokana na kutokwa na damu ndani ya fuvu la kichwa baada ya kupigwa na kitu butu.
Mwalimu aliyempiga marehemu alifikishwa Mahakamani kwa kosa la kuua bila kukusudia katika Shauri la Jinai Na. 16680 la mwaka 2025 (Mahakama Kuu - Kanda Ndogo ya Shinyanga), ambapo alikiri kosa na kuhukumiwa adhabu ya kutotenda kosa lolote ndani ya kipindi cha miezi 12.
Kesi ya kikatiba imepewa namba Shauri Na. 32373 la 2025, na imepangiwa kusikilizwa na Majaji Mruma, Hassan na Musokwa. Kesi imepangwa kutajwa tarehe 16 Machi 2026 saa 3:00 asubuhi. LHRC itaendelea kufuatilia shauri hili kwa karibu, kuhakikisha haki inapatikana kwa Mhoja na kuendeleza msukumo wa mageuzi ya kisheria yanayolinda watoto dhidi ya adhabu za kikatili na za kudhalilisha shuleni.
Soma

- Simiyu: Mwanafunzi adaiwa kufariki kwa kuchapwa viboko na kukanyagwa kichwani na mwalimu shuleni
- Mtandao wa Elimu Tanzania: Adhabu ya viboko iondolewe shuleni