Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Aisee hivi vidude vinanitesa nimekunywa kila aina ya matakataka ya dawa za hospitalini na tiba mbadala lakini bado vinanisumbua, angalau kidogo dawa zinaitwa legal kit zinisaidia lakini zingine ni kama natupa hela na kutesa tumbo kwa madawa

Na ni bora vingekuwa vinasumbua tumboni lakini mimi vinanitesa zaidi kwa maumivu ya vichomi mgongoni na kifuani upande wa moyo yaani hata kukohoa kucheka au kutikisa mkono wa kushoto ni maumivu makali sana
Ukividekeza imekula kwako kisaikoljia
 
Kwa upande wangu nilitumia sana dawa za hospitali lakini kiukweli ilikuwa nikama zinatuliza kwa muda..
Jambo lililofanya ni kuepuka kitu chochote ambacho ni kila .. kinafanya kuamsha vidonda tumbo...
Kwa mfano dagaa..ni mwaka wa nne sasa situmii.. na vinginevyo..
 
Aisee hivi vidude vinanitesa nimekunywa kila aina ya matakataka ya dawa za hospitalini na tiba mbadala lakini bado vinanisumbua, angalau kidogo dawa zinaitwa legal kit zinisaidia lakini zingine ni kama natupa hela na kutesa tumbo kwa madawa

Na ni bora vingekuwa vinasumbua tumboni lakini mimi vinanitesa zaidi kwa maumivu ya vichomi mgongoni na kifuani upande wa moyo yaani hata kukohoa kucheka au kutikisa mkono wa kushoto ni maumivu makali sana
Unga wa Mlonge, Uwatu na Mafuta ya Black Seed! Tumia kwa mwezi unapona jumla
 
Tafuta Omeprazone 20mg imeandikwa gold fish viko kwenye box ya Pink na nyeupe.Mimi nimetumia miezi 6 kila baada ya siku moja na nimepona kabisa.
Nimefanyiwa checking ya kuingiza mipira kupitia puani hadi tumboni. Na ikathibitishwa nimepona kabisa.Huu ni mwaka wa 10 sasa sina tatizo hilo kabisa.
 
Kupona vidonda vya tumbo sio rahisi kwa sababu vipo ndani ya tumbo na tumboni kuna chemical na pia asilimia kubwa ya vyakula vina kemikal , ili upone lazima utafute namna ya kuepuka Vyakula vyenye kemikal na kula vyakula vyenye uwezo wa kukabiliana na acid ili vidondo vipate mda wa kupona.
Tatizo Ni kwamba almost vyakula vyote ambavyo vinasababisha gesi ndo ambavyo viko common na affordable Kwa watu wa level zote,. Tofauti na hapo Ni kuviongeza tu vidonda Kwa kutokula mlo kamili
 
Kuna mtu wangu wa karibu ambaye ana ulcers zile chronic, siku zikiamka huwa anachukua majani ya mlonge na mstafeli, anayatwanga na kuyachemsha pamoja, baada ya hapo huwa anakunywa na vinapoa faster

Hii ndio nimethibitisha 100%
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom