Dawa gani ilikusaidia kwenye ugonjwa wa vidonda vya tumbo?

Sijawahi mkuu.. Naomba nisaidie kwanza mlonge ndio mnini?
Ni mti na itwa mti wa mlonge, google hapo youtube utauona. matumizi asubuhi mchana jioni kijiko 1 kidogo cha chai weka kwenye maji ya moto, uchemshe hiyo dawa, chemsha maji tuu kikombe kimoja alafu weka hiyo dawa kwenye hicho kikombe chenye maji ya moto koroga,ikipoa kunywa
 
Kwa upande wangu nilitumia sana dawa za hospitali lakini kiukweli ilikuwa nikama zinatuliza kwa muda..
Jambo lililofanya ni kuepuka kitu chochote ambacho ni kila .. kinafanya kuamsha vidonda tumbo...
Kwa mfano dagaa..ni mwaka wa nne sasa situmii.. na vinginevyo..
Mimi dagaa maharage njegere mwaka wa 2 sijala nikaambiwa nile bamia matango mapapai haya madude sikuyapenda lakini nilikula sana lakini wapi
 
Ni mti na itwa mti wa mlonge, google hapo youtube utauona. matumizi asubuhi mchana jioni kijiko 1 kidogo cha chai weka kwenye maji ya moto, uchemshe hiyo dawa, chemsha maji tuu kikombe kimoja alafu weka hiyo dawa kwenye hicho kikombe chenye maji ya moto koroga,ikipoa kunywa
Asante mkuu nimeona.. sasa Si Niko na nyingine naendelea nayo au hata Kwa pamoja hazina shida?
 
Aisee hivi vidude vinanitesa nimekunywa kila aina ya matakataka ya dawa za hospitalini na tiba mbadala lakini bado vinanisumbua, angalau kidogo dawa zinaitwa legal kit zinisaidia lakini zingine ni kama natupa hela na kutesa tumbo kwa madawa.

Na ni bora vingekuwa vinasumbua tumboni lakini mimi vinanitesa zaidi kwa maumivu ya vichomi mgongoni na kifuani upande wa moyo, yaani hata kukohoa kucheka au kutikisa mkono wa kushoto ni maumivu makali sana.
Uko wapi tukusaidie
 
Huu ugonjwa ni balaa sana nilitoka nao congo drc paka Leo sijapona mwaka wa pili huu nimezunguka hospital nyingi duniani naishia kupewa dawa za kupona miezi 7 alafu baadae ugonjwa unarudi 😭😭😭 ila mwaka huu nilichekiwa na docta mswedish na kipimo cha tumboni akaniambia vimebakia kidogo muhimu niache stress nitapona
 
Aisee hivi vidude vinanitesa nimekunywa kila aina ya matakataka ya dawa za hospitalini na tiba mbadala lakini bado vinanisumbua, angalau kidogo dawa zinaitwa legal kit zinisaidia lakini zingine ni kama natupa hela na kutesa tumbo kwa madawa.

Na ni bora vingekuwa vinasumbua tumboni lakini mimi vinanitesa zaidi kwa maumivu ya vichomi mgongoni na kifuani upande wa moyo, yaani hata kukohoa kucheka au kutikisa mkono wa kushoto ni maumivu makali sana.
Ukuje PM
 
Chukua cabbage, likate kama wanavyolikaya wakipika mboga
1705665100288.png

Ukishakata chemasha maji lita tano kwenye sufuria. Yakichemka tu epua kisha weka vipande ulivyokata.
1705665281240.png

Unaacha mchanganyiko wako wa cabbage na maji upoe

Saga carrot na kidude cha kusagia. Kisha changanya na cabbage inayopoa. Inches ipoe kabisa

Ukinaliza weka kwenye brenda saga mchanganyiko wako. Sasa kwenye kusaga haitakiwi iwe uji. Unasaga sekunde 5 hivi

Ukimakiza tafuta ndoo ndogo au chombo chochote hata dumu. Kisha weka mchanganyiko wako uliosaga na 🥕 with cabbage.

Hakikisha unaweka kwenye chombo ambacho ukiweka kina space ndani. Maana yake ukiweka kwenye ndoo ya lita kumi. Mchanganyioko wako utakuwa lita tano, na ndoo haijai. Ukiacha na nafasi inajitengeneza vizuri fermentation

Hapo unakuwa kama unatengeneza pombe. Maana inakuwa kama pombe, lazima ndoo iwe na nafasi.

Unafunika ndoo kwa siku tatu 72 hours. Hakikisha hewa haiingii unabana mfuniko vizuri.

Baada ya saa 72 toka ubane ndoo unafungua ile ndoo. Unachuja maji. Kifupi yana harufu kali, ila utazoea. Cabbage ukiliosha kawaida tu linatoa harufu, hapo kitakuwa na harufu kali kidogo

Ukichuja unatupa matakataka hayo maji unaweka kwenye chombo then kwenye fridge. Utakuwa unakunywa nusu saa kabla ya kula. Ukitumia miezi miwili unapumzika mwezi kisha unatumia tena miezi miwili then unapumzika hata miezi mitatu kisha unatumia mwezi mmoja

Nilitumia miezi 2 nikaka miezi sita nikatumia tena. Kama hujaelewa nitakupigia simu nikueleweshe

Matumizi: Wife ananikamulia machungwa mawili, kisha nachanganya na maji ya cabbage yaliyo kwenye fridge kutoa harufu. Huwa naweka na kitunguu swaumu siku moja moja.....

Any questions?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom