David Djumbe (Msaidizi wa Lissu) atekwa

David Djumbe (Msaidizi wa Lissu) atekwa

Hili ni onyo la awali kwa mamlaka za Tanzania.

Kwa ilipofikia Chadema Kwa sasa kitendo chochote cha kuua viongozi wake hakitanyamaziwa na haraka sana kisasi kitalipwa pakubwa

Jumbe, Mtu Mwema na Mtulivu, ambaye ni msaidizi wa Lissu ametekwa n.a. maofisa usalama Kwa lengo la kumuua, baada ya kutoa siri ya Lissu kulishwa sumu gerezani, hili jambo litavuruga Armani ya Nchi

Soma Pia: Tetesi: - David Djumbe Msaidizi Wa Tundu Lissu Ametekwa
Haifai kufyatuka namna hii.

Kwa nini wamuue; "lengo la kumuua" limetangazwa wapi?

Hakuna asiyejuwa uovu wa watu hawa, lakini haimsaidii yeyote kufyatuka tu namna hii jukwaani humu.

Inamsaidia nani hasa kwa maneno kama haya yaliyotumika; kama siyo hao hao waovu.

Huu siyo wakati wa kubwatuka tu hovyo hovyo na maneno ambayo waovu wanayachukulia kutokuwa na uzito wowote!

Samia yupo kwenye hali mbovu sana, ndiyo maana ya haya yote yanayofanyika. Anatafuta kila aina ya njia kupenya kikombe kinachomkabili; haitulazimu na sisi tuanze kuonyesha dalili za kutojiamini juu ya kinachosubiri kumwandama mwovu huyu.
 
Diaspora niliandika hapa kuwa waombe audience na Trump aingilie Kati ikiwezekana kama alivyofanya Venezuela! Lazimamkujaribu kila linalowezekana
Tusikwepe; hii kazi ni yetu, waTanzania. Siyo kazi ya Trump.

Ukisema hao hao 'diaspora' unaowawekea matumaini washughulikie kupaza sauti huko walipo, na hasa kukazia zaidi kwenye msaada wa kuzuia waTanzania kuuliwa wakati wa kutimiza jukumu la kumwadabisha mwovu huyu; hapo nitaungana nawe tupate msaada huo wa ulinzi dhidi ya mitutu anayoitumia Samia dhidi yetu.

tukihakikishiwa hilo, Samia na Genge lake hawadumu wiki moja.
 
Mganga akae na kichwa na maini wiki 2 na visioze na wewe kwa upumbavu wako ukaamini!
Nilikukataza matusi! Silaha ya mtu ambaye hajaelimika ni matusi. Ukiona mtu anatukana jua ameishiwa hoja.

Kujua mtu ana elimu ya kuunga unga ni kuangalia mawasilisho yake, hawezi kukosa hoja za mabavu na matusi.
 
Hii nchi watawala wametugeuza raia kuwa kama ng'ombe wao waliopo zizini, kwamba once wakikuhitaji kwa matumizi yao, basi is just a matter of picking and taking you to whatever place where they can brutally torture, kill and no one will ever see your body.

Tusipoamua kupambana nao katika namna ambayo itawaumiza watawala, hakuna raia wa taifa jingine atajitokeza kuja kupambana kwajili yetu.

Ukombozi thabiti huja kwa ujasiri na kumwaga damu.
Dalili na ushahidi wa kwamba CCM hawapo tayari kuachia madaraka kwa njia ya haki na amani, wamesha uonesha 29/10/2025 na bado wanaendelea kutuonesha mabavu yao kwa kuteka na kuua raia wenzetu kama hivi.

Amka Mtanganyika.
Twendeni tukaipiganie Nchi yetu kwa kumng'oa mkoloni mweusi CCM.
 
Msaidizi wa Tundu Lissu, David Djumbe inadaiwa ametekwa usiku huu na wanaodhaniwa kuwa Maafisa wa Usalama wa Taifa ambao walikuwa na silaha za moto.

Djumbe ametekwa akiwa nje ya geti la nyumbani kwake, maeneo ya Bunju Dar es Salaam.

Wananchi waliokuwa wanalikimbiza gari hilo lililomteka, wamesema wameliona likiingia kwenye nyumba za Usalama wa Taifa zilizo maeneo ya Mbweni.

=====

View attachment 3592007


View: https://www.instagram.com/p/DYkyDomueV1/?igsh=cTBocm1sa2g1M2Z0

======================

View: https://x.com/i/status/2057218064194637829

sema chadema imemficha ili kupata tension, nonsense public sympathy na kutafuta kiki useless 🐒
 
Huyu Mama na genge lake la mauaji na utekaji, ipo siku atakipata anachokitafuta. Anafikiri ataweza kuwaua, kuwafunga na kuwateka wote wanaomkosoa na kumpinga! Kuhusu hilo, asahau.

Watanganyika walio wengi wanamtaka Lissu na nchi yao! Wameshagundua wapo kwenye muungano wa kijinga. Hata afanye nini, haitabadilisha kitu.
 
Msaidizi wa Tundu Lissu, David Djumbe amedaiwa kutekwa usiku wa kuamkia leo Mei 21 na watu waliokuwa na silaha za moto.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alipoulizwa kuhusu tukio hilo, amesema; “Mimi nimefika Moshi sasa hizi, kwa hiyo ngoja nifuatilie kwanza.”

Taarifa zilizopatikana mitandaoni, zimedai kuwa Djumbe alitekwa akiwa nje ya geti la nyumbani kwake, maeneo ya Bunju Dar es Salaam, wakati akiingia nyumbani kwake ndipo watu hao waliokuwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser walimkamata na kumwingiza kwenye gari hilo na kuondoka naye kwa kasi.

Taarifa hizo zinasema wananchi walioshuhudia tukio hilo walilikimbiza gari hilo na wakadai kuwa waliona likiingia kwenye nyumba za Usalama wa Taifa zilizo maeneo ya Mbweni.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika alipoulizwa, alisema wameitisha mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia tukio hilo. Katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Mikocheni Dar es Salaam.
 
Tanzania si sehemu salama kabisa. Usalama wa Taifa si usalama wa taifa tena bali ni wa ccm. Mimi sina chama na sihitaji chama chochote cha siasa, lakini yanayofanyika yanatia hofu mno. Pia si kwa CHADEMA tu na hata kwa watu ambao si wanachama wa CDM nao wanauwawa.
 
Ninakubaliana na wewe, Tanzania kamwe hatuwezi kuwa na vita kati yetu kwa sababu ya mtu duni, mwovu kabisa kama Samia Suluhu Hassan.

Lililowazi ni kuwa mwovu huyu wakati wake wa kuwajibishwa sasa umetimia.

Hakuna tena sababu ya damu ya waTanzania kumwagika kwa sababu ya mtu wa hovyo kama huyu.
Mzee wa ngonjera, unaandika utadhani uko serious. Unasubiri nini sasa kuingia barabarani? Au unataka waingie wengine??
 
Diaspora niliandika hapa kuwa waombe audience na Trump aingilie Kati ikiwezekana kama alivyofanya Venezuela! Lazimamkujaribu kila linalowezekana
Trump huyu huyu anayesadiana na Israel kuua watoto wa Gaza na Iran? Ndiyo aje atetee wachoma miundombinu wa Kimara?
 
Dalili na ushahidi wa kwamba CCM hawapo tayari kuachia madaraka kwa njia ya haki na amani, wamesha uonesha 29/10/2025 na bado wanaendelea kutuonesha mabavu yao kwa kuteka na kuua raia wenzetu kama hivi.
Dalili zipo tangu 1995 chini ya utawala wa Komandoo Zanzibar mpaka 2001 kwa mauaji ya waandamanaji Pemba.

Sasa hivi upinzani umeimarika Tanganyika na kusababisha watawala kubabaika. Hata CCM Zanzibar wanaishi na hofu kwa yanayoendelea Bara.

Anguko la CCM bara moja kwa moja litasababisha anguko la CCM Zanzibar.
 
Msaidizi wa Tundu Lissu, David Djumbe inadaiwa ametekwa usiku huu na wanaodhaniwa kuwa Maafisa wa Usalama wa Taifa ambao walikuwa na silaha za moto.

Djumbe ametekwa akiwa nje ya geti la nyumbani kwake, maeneo ya Bunju Dar es Salaam.

Wananchi waliokuwa wanalikimbiza gari hilo lililomteka, wamesema wameliona likiingia kwenye nyumba za Usalama wa Taifa zilizo maeneo ya Mbweni.

=====



======================


Polisi wetu hayanaga akili kbs, yatakuwa yamemuua jamaa halafu yanatengeneza story ku justfy kifo chake kwamba kilitokana na majeraha makubwa kichwani baada ya kuanguka kutoka kwenye gari akijaribu kutoroka!.

Yaani mtuhumiwa mwenye pingu mikononi akiwa chini ya ulinzi wa polisi anawezaje kuruka kutoka kwenye gari na kukimbia bila kukamatwa??
Hizi mimi naziita ni drama za polisi!, niliwahi kumshauri IGP Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This
P
 
Back
Top Bottom