- Balozi Mwakawago, alikuwa na dini, alikuwa muumini mkubwa sana wa dini ya Islam, ukifika nyumbani kwake hicho kilikuwa ni kitu cha kwanza kuki-notice ndani ya nyumba yake na besides alikuwa ni mtu wa swala tano kwa siku, ninakuomba sana umuombe Mungu wako akusamehe kwa hayo maneno ya hapo juu.
- Marehemu, Balozi Mwakawago alikuwa ni mtu wa watu on a personal level, alikuwa ni mtu wa kujichanganya sana na watu wote bila kujali uwezo wala nafasi zao katika jamii. Alihudhuria sherehe yoyote aliyoalikwa, ninakumbuka siku moja akinilalamikia kwamba kwanini wananchi wa kawaida hawamualiki lakini wanamfahamisha later kwamba walikuwa na sherehe! au kilio.
- On the leadership level alikuwa ni mzalendo, mmoja wa the chosen one wa Mwalimu, he was a very respected leader huko Iringa, lakini ilipotokea ishu ya Mwamwindi wananchi wengi wa huko waliwakaba koo yeye na Chifu Adam Sapi, ambaye Marehemu ameoa dada yake, kwamba wafanye kila wawezalo ili asinyongwe na serikali ya awamu ya kwanza. Kwa vile sheria ni msumeno walishindwa ku-secure his realese na akaishia kunyongwa kama alivyohukumiwa na sheria, wananchi wengi wa Iringa hawakuridhishwa na juhudi zake pamoja na shemeji yake Chifu Sapi za kumuokoa Mwamwindi, na wakaishia kumnyima kura za ubunge mpaka anafariki he was very unpopular na home political base.
- Alikuwa ni mmoja wa viongozi waliomuamini Mwalimu na itikadi zake na kuzitimiza kwa matendo, infact hata nyumba yake aliyoijenga hapa mjini ilikuwa ni baada ya kuingia UN, otherwise aliondoka serikalini akiwa kama alivyo. Na knowing him on a close range he was not very happy na the way he parted ways na taifa letu baada ya kulitumikia kwa karibu nusu ya maisha yake he felt kwamba hakupewa heshima aliyostahili. Na Mtandao made very clear to him kwamba they wanted nothing to do with him na hii ilikuwa ni through Marehemu Kawawa, ambaye alimsaidia sana katika dakika zake za mwisho mwisho na ajira yake kwenye taifa letu.
- Huyu hakuwa fisadi, hakuiba wala hakuwa na kitu ninarudia ametoka serikalini akiwa mtupu sana, thanks to the UN na hasa Mzee Kofi Anan. Ninakumbuka sana baada ya kutoka kwake serikalini, nilikuwa NY nikashiriki kumfanyia sherehe kubwa sana ya kumuaga ambapo binafsi nili-specialize na financial ya ile hafla, pamoja na wananchi wengi sana kujitokeza kushikiri, pia tuliweza kuwashawishi Mabalozi karibu 20 wa nchi zingine za Africa kuja kushirki nasi kwenye kumuaga. It was a suprise party masikini ya Mungu hakujua, he cried alipofika ukumbini, siku moja baada ya sherehe he took a time akanitafuta personally na in a very humble way akaniamibia "....kijana you made my day, hujui how down I was hujui jinsi nilivyokuwa ninajisikia worhtless, kumbe kuna wanaothamini niliyoyafanya hapa duniani...", miezi mitatu later akiwa UN ninakumbuka kumualika tena kwenye sherehe moja iliyokuwa na wakuu wengi wa taifa, he came na again akanishukuru sana kwa kumkumbusha enzi zake, ingawa mwanzoni alisita sana kukubali mwaliko kwa wasi wasi kwamba labda wale wakuu wa taifa wasingependa awepo pale.
- Again this was a good man, ninajua kwamba kama bin-adam alikuwa na mapungufu, lakini ninaamini kwamba hayakuwa makubwa sana kiasi cha kuliltetea hasara taifa, au kulifisadi as opposed na hawa maviongozi magoi goi mengi tulionayo sasa. Kwa jinsi alivyokuwa akinisimulia experience zake na uongozi wa taifa hata Mwalimu alimuheshimu sana, infact hata ndani ya UN alikuwa aki-command heshima kubwa sana na ya juu sana, na he was a family man devoted in a very serious ways to his family, I mean hata watoto wake ni mfano mzuri sana wa who was Marehemu as a person.
- Again nimeandika hiki kipande na roho nzito sana, I am mourning this good man na a good leader, ninawatakia heri familia yake nzima na hasa watoto wake, Mungu awape nguvu na hasa busara za kupita hiki kipindi kigumu sana.
Respect.
FMEs!