..Huyu mzee inasemekana hakuwa muumini wa dini yoyote wakati wa uhai wake (pagan) hata wakati wa kuapishwa enzi za JK Nyerere yeye hakushika bible wala msahafu na mwenzie Kingunge.......RIP M/kawago!!
According to michuzi blog Balozi Mwakawago hatunaye tena
Marehemu daudi mwakawago
Habari zimetufikia sasa hivi zinasema balozi daudi mwakawago (71 amefariki dunia ajfajiri leo katika hospitali ya aga khan jijini dar alikokuwa amelazwa kwa takriban siku tisa akisumbuliwa na malaria na baadae nimonia.
Msemaji wa familia, yasini mwakawago, amethibitisha habari hizo na amesema msiba uko msasani maduka mawili jijini dar, na mazishi yanatarajiwa kufanyika jumamosi.
Balozi mwakawago atakumbukwa kama mwanasiasa na mwanadiplomasia mwandamizi aliyeshika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na waziri wa habari na utamaduni, waziri wa kazi na maendeleo, waziri wa viwanda na biashara.
Balozi mwakawago pia alikuwa balozi wetu huko italia na baadae umoja wa mataifa, kabla ya kusataafu. Aliwahi pia kuchaguliwa na katibu mkuu wa umoja wa mataifa wakati huo, koffi annan kuwa msuluhishi wa mgogoro nchini sierra leone.
Kuna taarifa kwamba ndugu yetu mkongwe, Comrade Daudi Mwakawago alifariki leo asubuhi katika Hospital ya Aga Khan jijini Dar es Salaam. Mazishi ni siku ya Jumamosi katika makaburi ya Kisutu
RIP Mzee Mwakawago, kwa wale tuliokuwa Freetown enzi hizo akiwa USG-UNAMSIL, tutamkumbuka kwa kuitisha vikao vya watanzania nyumbani kwake maeneo ya Aberdeen, kwa kweli alituunganisha vizuri sana, ni majonzi makubwa
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.