Mkuu
Nguruvi3, it's very unfortunately tangu tumeungana, hakuna any civic education or public information program to educate the public about the union, hivyo kuna wengi hawaujui muungano wetu ukiwemo wewe, hivyo najitolea kukuelimisha ili pia kuwaelimisha na wengine.
1. Muungano wetu ni very unique muungano duniani, miungano yote ni ama ni muungano wa union, ama ni muungano wa federation lakini muungano wetu ni both union and federation at the same time.
2. Kimataifa muungano wetu ni muungano wa union wa nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT ambayo ndio dola yenye sovereignty, yenye rais mmoja wa JMT, yenye serikali moja ya JMT, yenye Bunge moja la JMT, Mahakama moja ya Rufani ya JMT, sarafu moja ya JMT, Benki Kuu moja ya JMT, na uraia mmoja wa JMT.
3. Kwa vile tuna uraia mmoja wa JMT, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari bali kuna mtu mmoja tuu, Mtanzania mwenye haki zote za Utanzania. Hivyo Kila Mzanzibari ni Mtanzania ana haki zote za Utanzania ikiwemo kumiliki ardhi, ajira, elimu, kuishi popote, kufanya kazi popote na kuteuliwa kushika madaraka kwenye wadhifa wowote!.
4. Kimataifa Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT hivyo JMT ndio nchi inawajibika kuhudumia Zanzibar kwa kila kitu.
5. Muungano wetu ni kama ndoa kuna mume amechumbia, amelipa mahari, ameoa, amekabidhiwa mke, hivyo ni wajibu wa mume kumtunza mkewe kwa kila kitu, hivyo serikali ya JMT inaihudumia Zanzibar kwa kila kitu!.
6. Kitaifa muungano wetu ni federation ya nchi mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar yenye utawala wake wa ndani.
7. Hivyo ndani ya Tanzania, muungano wetu ni wa nchi mbili za Tanzania na Zanzibar, zenye serikali mbili, ya JMT na SMZ , zenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar, zenye mabunge mawili, Bunge la JMT na BLW, lenye Mahakama mbili, Mahakama Kuu ya JMT na Mahakama Kuu ya Zanzibar, yenye ardhi mbili, ardhi ya JMT na ardhi ya Zanzibar, yenye mipaka miwili, mipaka ya Tanzania Bara na mipaka ya Zanzibar, yenye uraia wa aina mbili, uraia wa JMT na Ukaazi wa Zanzibar.
8. Wenye haki Tanzania ni Watanzania wote, ila wenye haki Zanzibar ni Watanzania ambao ni Wakaazi wa Zanzibar pekee!.
9. Hivyo kila Mtanzania ana haki zote za Utanzania wakiwemo Watanzania wote ambao ni Wakaazi wa Zanzibar
10. Wenye haki Zanzibar ni Wazanzibari Wakaazi pekee.
Sii kweli kuwa wanapata 4.5% ya GDP ya Tanzania, Zanzibar are entitled 4.5% ya fedha zote za mikopo na misaada ya kimataifa only. Fedha hizi ni entitled!.
Mimi nilimuoa sweetheart wangu wa chuo, mimi nikaajiriwa RTD yeye Guardian. 1995 nikaacha kazi RTD na kujiunga DTV, nikamuachisha kazi wife na kukubali kumlipa mshahara wake wote aliokuwa analipwa as her entitlement. Muungano wetu ni kama ndoa, kwenye wanandoa wawili hawa kuna mmoja ambaye ni mume ana sovereignty na ni dola na kuna mwingine ni mke hana sovereignty, hada dola hivyo ni jukumu la mume kuhudumia mkewe. Huduma za mke kutoka kwa mumewe sio favours ni stahiki ni haki yake kwasababu Zanzibar imepoteza sovereignty haiwezi kukopa kimataifa na sio nchi, hivyo JMT ina wajibu kuhudumia!.
Refer No. 3 ya uraia, Mbarawa ni Mtanzania ana haki zote za Utanzania kama Mtanzania mwingine yeyote, na KM wake the same.
Shaka ni kama Mbarawa ana haki zote za Utanzania kama Mtanzania mwingine yeyote ikiwemo kuteuliwa kwenye nafasi yoyote.
Wazanzibari hawapewi ardhi bali wanamiliki ardhi kwa haki ya Utanzania wao kama Mtanzania mwingine yeyote, ila Mtanzania hawezi kumiliki ardhi Zanzibar bali ni Wanzanzibari wakaazi pekee!. Watanzania wote wakiruhusiwa kumiliki ardhi, Watanzania watavamia vile visiwa vitazama!.
Referring to No. 3 again, wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT wana haki zote za Utanzania na wanajadili chochote!.
Sio sababu za kipuuzi, wana sababu za msingi sana.
Naamini wewe una wazazi, una ndugu na una mke, how much do you spend kwa wazazi na ndugu zako compared to mkeo?. Muungano wetu ni kama ndoa, Zanzibar ni mwanandoa, Simiyu ni mwana ndugu!.
Zanzibar ndio wana sheria ya kura ya maoni, sisi Tanzania Bara, hatuna ila pia hoja kama hii niliwahi kushauri humu
Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja
Kwa vile nimeandika sana humu kuhusu muungano, bandiko hili nitalisambaza kwenye baadhi ya post hizo ili uzitumie kama post darasa ujifunze zaidi kuhusu muungano, tena tumshukuru sana Samia, ndie aliyetoa uhuru huu
"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Natumaini nimekusaidia sana kukuelimisha kuhusu huu muungano wetu adhimu.
Pasco.
Karibu katika baadhi ya Rejea Zangu kuhusu huu Muungano wetu adhimu.
-
Wanabodi, Wakati tunaelekea kusherehekea miaka 51 ya Muungano wetu adhimu, kuna taarifa za kushitusha kutoka Zanzibar!. TAARIFA MUHIMU: Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Magharibi Unguja kupitia kikao chake kilichomalizika muda huu Kimemvua Uanachama wa C.C.M Mzee HASSAN...
www.jamiiforums.com
-
Wanabodi, Wakati tukijiandaa rasmi kuingia kwenye serikali 3, tutake tusitake, lazima tutarudi nyuma kuungazia muungano wetu, na kabla hatujaingia katika serikali tatu, lazima kwanza tuwe na Mkataba rasmi wa Muungano, ndipo zifuate hizo serikali 3. Hiki kilichopo, kinachoitwa Mkataba wa...
www.jamiiforums.com
-
Wanabodi, Kufuatia chokochoko ya kuuchokoa Muungano ilioanzishwa na kikundi cha Uamsho huko Zanzibar, na kuungwa mkono na Wazanzibari wasioutakia mema huu Muungano wetu adhimu, zimeanza kutolewa hoja mbalimbali za kuhatarisha huu Muungano wetu ikiwemo hoja ya Watanzania tupewe fursa kuujadili...
www.jamiiforums.com
-
Wanabodi, Sisi wengine wenu humu, japo tuna vyama toka ndani ya mioyo yetu, CCM kimeoza kwa rushwa na ufisadi, from top to bottom, left, right and center hadi kwenye shina lake!, huku hakuna upinzani wowote wa maana!, watu wanacheza makida makida na wengine hadi kuchezea shilingi chooni...
www.jamiiforums.com
-