SoC03 Azimio la Vijana haliepukiki kama tunahitaji Katiba Mpya

Stories of Change - 2023 Competition

Smartkahn

JF-Expert Member
Jun 22, 2020
293
565
KATIBA
Ni sheria kuu au sheria mama ya nchi, kutokea humo zinazaliwa kanuni zote sheria zote na taratibu zote. kwa msingi huo katiba ni msingi mkuu na muongozo wa nchi unaotoa muongozo wa namna gani nchi inapaswa kuongozwa. (Ni mkataba unaotoa muafaka baina ya mtawala na mtawaliwa). katiba ya Tanzania ina misingi mikuu minne ambayo ni uhuru, haki, undugu na amani hivyo umuhimu mkubwa wa katiba unategemea misingi hii. Kwa mujibu wa Paskali Mayala,.[Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?].

AZIMIO
Ni tamko kuu linalotangazwa kwa umma husika na kwapamoja wanakua wameazimia kwa dhati kuanzisha au kukomesha jambo au mambo flani flani kutokana na malengo wliojiwekea. Mfano Azimio la Arusha la mwaka 1967 lilikua ni tamko rasmi la kisiasa lililokusudiwa kuiongoza Tanzania katika misingi ya ujamaa na kujitegemea nakadharika. Pia soma zaidi; na FM WOLLE,. [Thread 'Kwa vyovyote vile Azimio la Arusha lisingependwa na halitapendwa na viongozi wa kimichongo michongo' Kwa vyovyote vile Azimio la Arusha lisingependwa na halitapendwa na viongozi wa kimichongo michongo].

Dhima kuu ya kuhusianisha katiba mpya na azimio jipya (Mseto) ni kuiongezea nguvu katiba mpya yaani kusisitiza au kutilia mkazo katika utekelezaji wake katika nchi yetu ya Tanzania (kuamsha hari/molali kwa vijana na watu wote kwaajili ya nchi yetu (uzalendo)).

katika kuelekea kuzindua katiba mpya maandalizi yake ni lazima yaambatane na azimio dhabiti mpaka siku ya kilele cha tukio la uzinduzi wa katiba mpya. Chukulia mfano chakula kinapoandaliwa iwe ugari ama wali ni lazima mboga nzuri pia pembeni itakayomuongezea ladha na hamu mlaji wa chakula hicho na hatimae atapata nguvu na afya pia itamuongezea ufanisi katika umeng'enyaji wa chakula na ifahamike kua kwenye mbogamboga Kuna virutubisho (vitamini) ambavyo kimsingi sio lazima sana lakini vinaumuhimu katika mwili wa binadamu.

================================
KABLA YA KATIBA MPYA IMARA NA THABITI LINATAKIWA AZIMIO IMARA NA DHABITI ZAIDI.
Sina maana kwamba linatakiwa azimio jipya la hasha! Bali azimio ni lilelile la Arusha ila linahitaji maboresho kidogo (kusashisha) ili kuendana na mabadiliko hasa katika zama hizi za ukuaji wa kasi wa sayansi na teknolojia hususani ulimwengu wa kidijitali mapinduzi yanne ya viwanda, (teknolojia habari na teknolojia hai).

Sasa basi licha ya kua na katiba nzuri sheria nzuri kanuni na taratibu nzuri lakini bado hizi changamoto zinaendelea kuikabili nchi hii inamaana kwamba hata tukiwa na katiba mpya bado itakosa nguvu, kwasababu changamoto zinazoikabili nchi hii zinaendelea kuwepo licha ya kwamba katiba na sheria zilizopo kwa asilimia kubwa zaidi ya 85% zinaweza kutatuliwa, yaani inakadiliwa asilimia 85% ya changamoto za nchi ziko ndani ya uwezo wa katiba hii tunayoitumia.

Ndugu watanzania kwa ufafanuzi huo hapo juu inatosha kutufungua fikra na kufikiri kwamba!? tunaweza kuunda katiba bora duniani pengine yenye kurasa nyingi zaidi duniani lakini isituletee matokeo chanya kama wengi wetu tunavyotarajia, hapo ndipo linapokuja wazo na kuna umuhimu kwamba linahitajika tamko kuu kutoka kwa kiongozi au viongozi mwenye maono na malengo mwenye nguvu na mamlaka dhabiti asiyeteteleka kwa namna yeyote ile na ikiwezekana awe mwenye hekima mithili ya Mw J. K. Nyerere na mwenye uzalendo na uthubutu anaeamini katika vitendo na matokeo chanya zaidi ya Hayati Dr. John Joseph Magufuli. atakae tuongoza watanzania kuazimia vikali na kwa viapo thabiti.

Changamoto ni sehemu ya maisha, kwanza ni muhimu tutambue kwamba jamii yoyote ile iwe Tanzania, Afrika na duniani kote lazima ikumbane na matatizo (changamoto) hili halikwepeki, Lakini ukubwa (ukubwa na uzito) wa changamoto au matatizo hayo utatofautiana kutoka jamii moja na nyingine kwa sababu mbalimbali lakini kwa kua kila jamii ina uongozi wake, sina budi kusema kwamba serikali ndio inayo ratibu na kudhibiti mambo haya. Je serikali inawajibika ipasavyo!? Nini kifanyike, vijana wa kitanzania tuzinduke!!! tujiwinde mpaka tujikamate.

================================
ZIFUATAZO NI CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TANZANIA KWA SASA.
Changamoto hizi zimefikia hatua ya nyufanyufa ambazo zisipo angaliwa kwa jicho la tatu na kuthibitiwa kwa wakati na serikali kwa uratibu maalumu (MSETO) baina ya katiba mpya na azimio dhabiti) zinaweza kuligawa taifa na nchi ya Tanzania.

Changamoto hizo ni;
1. Udhaifu mkubwa wa Tanzania ni Tanzania yenyewe; nikiwa na maana kwamba muungano baina ya Tanganyika na Nzanzibari unadosari ambazo zinaleta maswali mengi na wasiwasi mkubwa katika jamii... hii nikutokana na kwamba muungano haijakamilika upo katikati/upo katika hari ya uvuguvugu. nanukuu kutoka katka Biblia "ni heri kua moto ama kua baridi kabisa kuliko kua vuguvugu", hili jambo ni nzito inahitajika hekima na utashi bayana kabisa sisi kama jamii ya watu wanaojitambua ni vyema kama tunatengana tutengane tu na kama tumeamua kuungana basi tuungane kuwe na serikali moja na kusiwe na serikali mbili wala serikali tatu huo ni unafiki wa wazi wazi na moja kwa moja, hii ndio changamoto ya kiufundi inayotumika kimkakati na maadui, kama tisipo chagua moja kati ya umoja/serikali moja na kutengana basi tunashuhuli pevu na endelavu.

2. Kuzorota/ kufifia kwa uhuru haki na utawara bora wa sheria; Katika vyombo vya dola ulinzi na usalama wa taifa, imekua kawaida na ishazoeleka kuripotiwa kwa taarafa za unyanyasaji, upolaji, ukatili,rushwa, kubambikia kesi dhidi ya polisi kitu cha kuhuzunisha zaidi haya matukio ya hovyo yanafanywa na polisi ambayo kimsingi ndio chombo husika kinacho husika na kudhibiti matukio hayo sasa raia uhakika wa usalama na ulinzi wao na mali zao wanautoa wapi?

Ifahamike tu hii ni rekodi ya matukio yaliyovuma baada ya raia kupaza sauti je? ni matukio nimangapi yamefichwa ukizingatia wao ndio wazoefu wanamtandao na nguvu ya kufunika maovu hayo.

images.jpeg

Chanzo: mitandaoni,. (Facebook). Polisi wakitumia nguvu kubwa badala ya weledi.

3. Kufifia kwa umoja na mshikamano katika taifa; tofauti za kimtizamo katika vyama, kiimani katika dini, kitamaduni na mila katika makabila, kimaslahi katika kanda, hoja na kauli tata zinazotolewe na viongozi pasipo kutafakari madhara yake kwa taifa, hari hii imekua ikichanua ndani ya taifa. na serikali haioneshi hata dalili za kushughulikia changamoto hii badala yake wanajibu hoja kimhemuko pasipo kuzingatia weledi katika nafasi zao. mfano; Hamieni burundi, kataa wahuni, genge la sukuma na msoga.
Udini kuna baadhi ya dini mafundisho yake yamejikita kwenye chuki, kujikweza na utengano.

4. Kushamili kwa rushwa ufisadi tamaa na uchoyo uliokithili miongoni mwa viongozi ndani ya wizara mbalimbali za serikali; hari hii imepelekea kudolola kwa kiasi kikubwa ufanisi na utendaji kazi serikalini na utoaji huduma mbalimbali katika jamii na kuzalisha kero zinazokuja kuingombanisha serikali na wananchi hii kitaalamu tuiiteje, (shida ndani ya tatizo),. Rejea ripoti ya CAG,. 2021/2022, na 2022/2023.

Kanuni za kibiashara zinasema binadamu hutosheka na vitu kama chakura, kiu lakini kamwe hawezi kutosheka ama kuridhika pesa/utajili kadri anapopata zaidi ndia anataka zaidi na zaidi sasa basi viongozi serikalini nao ni binadamu na binadamu wote tuliotimamu tunafanana matamanio pindi kiongozi au mtumishi wa umma anapoona fursa na kunaudhaifu atadokoa zaidi na zaidi na kamwe hatatosheka.

5. Kukosekana/kufifia kwa uwajibikaji madhubuti wa viongozi na watumishi wa umma kwa ujumla; Licha ya kua viongozi kutumia fedha za walipa kodi lakini wengi wao hawanamalengo na uchungu na hii nchi, wanapwaya/hawatoshi kwenye nafasi zao, chakudhangaza zaidi mpaka tatizo litokee katika wizara ndio unamuoma kiongozi anaibuka kuja kutolea maelezo tatizo hilo wakati alipaswa alishugurikie liishe chini kwa chini kabla halijalipuka, mbaya zaidi matatizo yaliyo mengi yeyendio chanzo na hata akikutwa na tuhuma hizo hayupo tayari kuwajibika muda huohuo analindwa na mamlaka badala ya kuwajibishwa wao wanamhamishia sehemu au wizara nyingine akaendelee na tabia yake. Sasa hii ni changamoto kama tujuavyo viongozi nao pia ni watu na watu siokama mashine janja hivyo wanamapungufu yao kama binadamu wengine tu hivyo ni lazima kuwe na muongozo uliopangiliwa na kusisitizwa vikali na kiongozi mwenye sauti/kauli ya mamlaka ili kuweza kuratibu na kudhibiti haya mambo.

6. Kukua kwa Kasi katika nyanja ya sayansi na teknolojia hususani katika nyanja ya kidijitali masuala ya mtandao, teknolojia taarifa na uhandisi katika teknolojia hai; wahenga wanasema "hakuna kizuri kisicho na kasoro" tatizo linakua kubwa kutokana na ukweli kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi za dunia ya tatu elimu bado ni changamoto.

7. Vitishio vya usalama/amani nchini; Maadui wetu wameungana baada ya kuona tupo imara na hatuteteleki, wametumia udhaifu wetu wa nyakati hizi kama fursa madhara ya mlipuko wa UVIKO19, tunapitia kipindi kigumu sana ukiitizama Tanzania kwa jicho la tatu.

20211001_101817.jpg

Chanzo: mitandaoni,. Masoud Kipanya.

RAI YANGU KWA WATANZANIA WOTE HASA VIJANA. Mseto huu haukwepiki kama kweli tunahitaji katiba mpya na yenye meno,

Kijana zinduka kijana pata wasaa tafakari kesho yako kwa kutizama juzi Jana na leo kisha tafakari je? Hali yako itaendelea kua hivyo mpaka lini!

Unafikilia unastahili kua na hali hiyo ukilinganisha na fursa na rasilimali zilizopo katika taifa lako.?
Kwakua kuna mamlaka inayohusika kuratibu mambo haya nchini ambayo ni serikali, kwa ujumla ni siasa ikiongozwa na wanasiasa wenyewe, hawa ndio wakula nao sahani moja. Kwani wao ndio wamebeba mstakabali mzima wa maisha yetu.

SABABU ZA UHITAJI WA KATIBA MPYA HUKU IKISINDIKIZWA NA MAONESHO YA AZIMIO LA VIJANA ILI KUPATA KATIBA YENYE MENO:

==>Kwanza kabisa tunahitaji kuboresha utawala bora wa haki na unaozingatia sheria za nchi.
Screenshot_20230619-044203.png

Chanzo: Mitandaoni na @Erythrocytes; utawala bora amani na haki.

==>Pili tunahitaji kudumisha na kuendeleza umoja uhuru na mshikamano. Na kulaani vikali matabaka yanayoibuka baina ya vyama, ukanda na imani.

==>Tatu tunahitaji kwa shauku kubwa uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma katika nafasi zao kwa ufanisi mkubwa, na watumishi hao wapatikane kwa kukidhi vigezo stahiki (weledi/profesheni), wahenga wanasema "Haijalishi paka ni mweusi au mweupe bali yule anaekamata panya ndio anafaa".
images (1).jpeg

Chanzo: Mitandaoni; picha hayati Mwl.J.K Nyerere, ikiwakilisha uwajibikaji kwa viongozi.

==>Nne yahitajika maboresho makubwa sana ya mfumo mzima wa elimu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia. Ulimwengu unaenda kasi sana kiasi kwamba muongo mmoja ujao yatazaliwa mataifa ya ulimwengu wa nne, nyuma ya huu wa tatu na Tanzania tutajikuta miongoni mwao.
images (2).jpeg

Chanzo: Mitandaoni; picha inawakilisha kuto kuendana kwa mifumo ya Elimu na mahitaji ya soko.

•HITIMISHO.
Watanzania wengi tunahitaji mabadiliko/maboresho chanya kwa maslahi makubwa ya taifa letu kwa kizazi cha sasa na cha baadae. KATIBA MPYA ndio imekua tumaini letu kubwa na la mwisho, je tukipata katiba nzuri zaidi itatusaidia kufikia malengo yetu? Fikra zangu zinaniambia sio rahisi kutekelezeka kwa matakwa tutakayokubaliana kwenye katiba mpya, tuchukulie mfano jirani yetu wa kaskazini mambo sio shwari licha ya kua na katiba mpya.

Wito wangu kwa watanzania wote hasa vijana tutumie azimio la arusha (Sio mbaya tukiliboresha kuendana na wakati (japo halina dosari kwa mzalendo wa dhati kabisa)), kama mpango mkakati wa kuhakikisha katiba mpya inakua na nguvu katika kuongoza nchi.

Yaani nataka kuona watawala na watawaliwa wanakua na hofu mioyoni mwao, wanakua na uchungu na rasilimali za nchi, kwa ujumla kuamsha Hali ya uzalendo kama ilivyo kwa waumini mbele ya muumba.
Mwisho kabisa tunatakiwa tuandae tukio maalumu na mahsusi kwaajili ya kuwasilisha hisia zetu juu ya katiba hai mpya tukio hilo tutaliita AZIMIO LA VIJANA litakalochukua siku kadhaa na kilele chake kitaambatana na siku ya uzinduzi wa katiba hai mpya.

Tukio hilo litakua katika mfumo wa maonyesho, kama vile maandamano ya amani nchi mzima, kazi za sanaa mbalimbali (muziki/mashairi, maigizo, na hotuba), kuelekea kilele cha uzinduzi wa katiba mpya.

=========================================
Amani iwe nanyi.
Karibuni.
 

Attachments

  • Screenshot_20230619-044203.png
    Screenshot_20230619-044203.png
    320.6 KB · Views: 3
Hali si shwari katika hii hoja ya tatu, inahitajika moja ya R kati ya zile 4R ifanye kazi yake ili kudumisha umoja na mshikamano wa taifa letu kabla mambo hayajaharibika zaidi.

Nipende kutambua mchango wa vyama vya upinzani katika kuiweka sawa serikali kuu katika mtari hasa katika nyakati ngumu ambapo raia wanapoteza matumaini na imani, juu ya maamuzi mbalimbali ya serikali, na-appreciate kazi yao.

Lakini Tanzania nchi yangu inasifa flani hivi ya heshma, kariba flani hivi ya kistaarabu, kiujumla Tanzania sio taifa la hovyo. Sasa baadhi ya wanasiasa na wanaharakati aidha ndani ya chama tawala ama vyama pinzani wanawasilisha hoja maoni ama hisia zao katika namna ambayo haiendani na hadhi ama sifa stahiki za Taifa la Tanzania (wanatumia pigo ambazo sio, unaona kabisa hizi pigo sio zetu, yaani sio maadili yetu kabisa! ni pigo za failed state huko.(Sasa huku ni kuiharibu nchi, kuna baadhi ya content kutoka kwa wanasiasa mashuhuri kama vile ngazi ya uwaziri zisiwe za kim-hemko na zisizagae mitandaoni maana zinaharibu taswira ya nchi)).
Kufifia kwa umoja na mshikamano katika taifa; tofauti za kimtizamo katika vyama, kiimani katika dini, kitamaduni na mila katika makabila, kimaslahi katika kanda, hoja na kauli tata zinazotolewe na viongozi pasipo kutafakari madhara yake kwa taifa, hari hii imekua ikichanua ndani ya taifa. na serikali haioneshi hata dalili za kushughulikia changamoto hii badala yake wanajibu hoja kimhemuko pasipo kuzingatia weledi katika nafasi zao. mfano; Hamieni burundi, kataa wahuni, genge la sukuma na msoga.
Udini kuna baadhi ya dini mafundisho yake yamejikita kwenye chuki, kujikweza na utengano.
 
Kinasubiriwa kitu gani huyu kupewa tuzo yake?
Kongole mwandishi umewaza na kuwazua
 
Back
Top Bottom