Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Kwanini iwe ubaya? kwani alimteua kwa masharti kuwa "nitakuthibitisha baadaye"? Kama yeye Jaji Ibrahim anaona kuwa anacheleweshwa kuthibitishwa au anaona Jaji Mkuu mpya anacheleweshwa basi anachotakiwa kufanywa ni kuomba Rais amteue Jaji mwingine kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu. Very simple.

..unachokisema ni sahihi kabisa THEORETICALLY.

..Mtu aliyekaimu muda mrefu namna hiyo asipothibitishwa ktk nafasi husika huvunjika moyo kazini.

..unless awe haitaki nafasi husika.

..Nazungumzia zaidi KIUBINADAMU.
 
Present your case with specific/empirical evidence. Not generics
 
Hapa naona watu wanajaribu kutetea watendaji wazembe wazembe; sasa kiapo anachokula ni cha nini kama hana mpango wa kutumika kwa kadiri ya uwezo wake wote? Yaani, mnataka kusema mtu atakuwa mzembe au hatofanya kazi sana kwa sababu anaweza asipate nafasi hiyo rasmi? Hizi ni fikra gani hizi. Inawezekana watu wamo humku ambao wakipewa nafasi ya kukaimu basi hawatendi kwa kadiri ya uwezo wao wote na kwamba wasipopewa nafasi ya kushika permanently hawatoumia sana na kuona wamerukwa! Hii ni dalili ya kutetea uzembe. Ukiteuliwa kushika wadhifa fulani iwe kwa muda au rasmi ni lazima utende kazi kwa uaminifu na weledi wako wote maana hilo ni jukumu lako.

Sijui unachopinga kwenye hoja yangu ni nini hasa. Na pia sijui una mawazo huru kiasi gani katika kujadili hii mada. Suala la ofisa kukaimu au kutokaimu nafasi katika ofisi na katika mazingira gani ni la kitaalamu. Kwa vile suala katika mukhtadha huu sio kukosekana kwa jaji mwenye sifa ya kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu, laiti kama Raisi Magufuli angetaka kupatiwa ushauri wa mtaalam wa mambo ya utumishi kuhusu suala hili, hakika huyo mtaalam angemshauri ateuwe Jaji Mkuu moja kwa moja na sio kaimu.

Suala la kuzingatia hapa ni je, ni nini majukumu ya Jaji Mkuu? Fani ya personnel psychology inatufundisha kuwa kutakuwa na tofauti kubwa ya kiutendaji kati ya Jaji Mkuu kamili na Kaimu Jaji Mkuu. Kuwepo au kutokuwepo kwa kitendo cha kula kiapo kabla ya kuanza majukumu ya kiofisi hakubadili ukweli huu!

Kwa kuzingatia hoja hapo juu, ni lazima tuhoji: Magufuli alikuwa anawazia nini alipoteua Kaimu Jaji Mkuu badala ya Jaji Mkuu kamili? Je, uamuzi wake huu ulikuwa matokeo ya tafakuri ya kina (well-thought out decision) kwa kuzingatia maslahi mapana ya utoaji haki nchini?
 
Maajabu haya eti jaji mkuu mtu anakaimu tu. Mpaka lini!?
 
Bavicha mmekalia majungu na umbumbu wenu. Sasa ww una uwelewa wa sheria
 
Hivi kiwango cha Mwanakijiji kimeporomoka au ni kwamba lazima aandike tu kumuunga mkono ' mtu wa kwao ' ili aonekane yupo na anamtetea kwa udi na uvumba ?
 
Huyo vuvuzela wenu lisu ulisikia anahoji chochote si alibaki mdomo wazi. Hata babu yenu msigwa alibaki kupiga soga tu! =!
 
Jpm kaweza sasa wale wanafunzi wa kukariri wamemkuta mwamba wa sheria sijui watakuja na upepo gani. Kwisha habari yenu kisiasa mmebaki kuhudhuria misiba tu
 
"Allen Kilewella, post: 20880835, member: 55849"]Nguruvi3 Hii hoja ajabu ya mwaka kwanza Mzee Mwanakijiji anaipindisha ama pia hataki kuijibu. Swali la Lissu ambalo halijajibiwa na huyo "mtoa darsa" wao na hata na Mzee mwanakijiji mwenyewe ni kwamba kuna sababu gani ya msingi mhimili kama Mahakama kuwa na kiongozi anayekaimu nafasi yake kwa miezi mitano sasa?
Prof Kabudi amejibu kuwa Rais Nyerere alifanya hivyo pia! Niliposikia hilo jibu nikajua siasa si mchezo, na sikuamini nilichosikia

Lakini, hata kama Nyerere atatumika kama 'template' bado kuna hoja. Mwl alieleza kwanini alichukua muda kumteua Jaji mkuu. Mwl alikuwa na presidential prerogative ya kumwacha Jaji mzungu. Kwa busara za wakati hakutumia prerogative hiyo kiholela
Aliitumia kwenda kutafuta Jaji kutoka Commonwealth kwa spirit ya matumizi sahihi ya prerogative. Leo Prof na MM hawana jibu kwanini nafasi hiyo nyeti ikaimiwe miezi 5
Mosi nakubaliana na hoja ya Mwanakijiji kwamba hakuna sheria iliyovunjwa, lakini kwa tukio hili lazima tugutushwe kwamba kama hakuna sheria ilivyovunjwa
Nimekubaliana naye kwa sheria kutovunjwa, nimekubaliana naye kwa ''prerogative power''.
Nisichokubaliana naye ni matumizi ya prerogative.
Prerogative iliwekwa makusudi ili kumpa uwezo wa kutenda ndani ya Busara

Rais ana prerogative ya kuteua wabunge 10. Kwa kutambua anaweza ku misuse prerogative, sheria ikasema wawepo makundi kadhaa.

Hapa busara zimetumika kuhakikisha Rais kwa jinsia yoyote hatatimiza masharti bila busara

Niliwahi kujadili, katika wabunge 10 Rais anaweza kuteua wote kutoka kwa familia yake na bado hajavunja sheria. Atakuwa ametumia prerogative, lakini je, busara za hilo zina impact gani na ni kwa national interest?

Prerogative ya kuteua kaimu Jaji mkuu ipo, lakini kama zingine imewekewa uzio na sababu zake. Haipo wazi tu kama MM anavyodhani, na asivyoweza kueleza jamvi kama alivyofeli Prof Kabudi

Ikitokea sababu muhimu nje ya zilizoanishwa kama ya Mwl, umma una haki ya kujua.

Hapo ndipo hoja ya Lissu si kuwa inapata miguu bali inatembea bila kupingwa.
Kabudi hakuweza, MM hadi sasa hajaweza. Pengine anajipanga tumpe muda
Bunge hili lililojaa wabunge wa CCM haiwezekani kupeleka hoja inayopingana na mtazamo na utashi wa Rais ikakubalika ama ikapitishwa. Tumeona ni kwa jinsi gani wabunge hao wanapoungana dhidi ya hoja yoyote ile inayopingwa na Serikali. Jibu ni rahisi, wabunge wanaujua ukuu wa chama (Party Supremacy) kwenye nafasi zao walizonazo za ubunge!
Wapinzani walitoa hoja ya kujadili hali ya usalama wa Taifa.
CCM-wabunge kwa kuelewa mhimili huo nao 'unakaimiwa' wakakataa
Siku tatu baadaye, CCM hao hao wakataka ijadiliwe baada ya matatizo Kibiti

Juzi wakati Prof Kabudi anajikanyaga kanyaga walikuwa wanapiga makofi.

Leo ukiwauliza kwanini nafasi hiyo ikaimiwe kwa muda mrefu hakuna anayeweza kueleza, afadhali ya Prof Kabudi alijihifadhi kwa Nyerere, MM anatumia prerogative

Kuna kiongozi aliteuliwa kwa prerogative, akapitishwa na chama kwa prerogative, na akachaguliwa katika taasisi nyeti kwa prerogative.

Matatizo ya taasisi ni kutokana na kiongozi kufanya kazi kwa 'fadhila' za prerogative

Masuala ya kitaifa yanajadiliwa akitazama 'prerogative' iliyomfikisha hapo. Tunafeli sote

Watu wengi wasichokiona ni umuhimu wa mhimili wa sheria.
Mhimili huo unapopoteza nguvu zake za asili ni hatari

Uchaguzi wa TLS uliingiliwa na serikali, tukasikia kauli zenye mwelekeo wa 'kisiasa'
Pengine hii ni katika kuonyesha misuli ya ''mhimili uliozama zaidi kwenda chini''

Swali, je, hayo ni kwa public interest au ni kwa interest ya mtu au watu?
 
Nimesikiliza kwa makini kile kinachoitwa "darasa" la Prof. Kabudi jana Bungeni kuhusiana na suala la Kaimu Jaji Mkuu na hasa hoja nzima ya kukaimiwa kwa nafasi ya Jaji Mkuu. Inasikitisha kwanza kwamba kuna watu wanasifia kuwa ametoa "darasa" na kwamba watu walikuwa wanamsikiliza kama wanafunzi katika Shule ya Msingi Mtakuja!

Je, ni kweli kile alichokisema watu walikuwa hawakijui? Ni kweli wabunge na wanasheria walioko Bungeni walikuwa hawajui yale yaliyokuwa yanasemwa?

Kuna hoja ya kuuliza swali; kwamba - kwanini Rais amemteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu kwa muda wote huu. Swali ambalo halipaswi kuulizwa na tulilikataa wakati ule ni kuhusu mamlaka ya Rais kumteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu. Hili liko ndani ya mamlaka ya Rais (Presidential prerogative). Lakini pia swali hili kwa ukubwa wake halipaswi kuulizwa isipokuwa kisiasa (political question) ili watu kupata hoja za kisiasa au ujiko wa kisiasa. Kwamba, mtu anataka kuonesha kuwa Magufuli amekosa mtu wa kuwa jaji mkuu, au kwamba Magufuli ana tatizo na mahakama n.k. Hili si jambo sahihi; wabunge kama wanaona Rais anatumia muda mrefu kujaza nafasi ya jaji mkuu wana uwezo wa kubadilisha sharia na hata Katiba chini ya Ibara ya 100 ya Katiba yetu.

Kama wanataka nafasi ya Jaji Mkuu isikaimiwe indefinitely (kama hoja ya Lissu ilivyoashiria) namna pekee ni kubadilisha Katiba au sheria ili kuweka kikomo kama ilivyo katika baadhi ya nafasi za utumishi wa umma ambapo sheria inasema mtu atakaimu nafasi kwa muda fulani na baada ya hapo basi mtu wa kudumu ateuliwe au aliyekaimu athibitishwe. Wao wabunge (watunga sheria na wanaoweza kufanya mabadiliko ya Katiba) wanaweza kuweka kikomo labda kwa ajili ya mustakabali)

Kama kwa mfano Rais angejaza cheo cha Ujaji siku moja tu baada ya Jaji Othman kustaafu wapo ambao labda wangeweza kuja na hoja ya kwanini amejaza nafasi haraka bila kuonesha tafakari sana au klutumia muda kufanya utafiti wa kutosha! Lakini pia kuna swali ambalo inabidi liulizwe kwa wale wanaolalamikia - kwa Rais kuweka Kaimu Jaji Mkuu ni shughuli gani ya Mahakama Kuu ambayo haiwezi kufanyika sasa hivi kwa vile kuna kaimu Jaji Mkuu au ni kitu gani hakifanyiki katika mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambacho kinapaswa kufanywa na jaji mkuu peke yake. Hili ndilo linaweza kuwa hoja ya kwanini inahitajika Jaji Mkuu na siyo Kaimu Jaji Mkuu?

Lakini kung'ang'ania kitu ambacho wote wanajua hakipo - kwamba Rais hajavunja sheria wala Katiba, na kuwa hakuna kikomo cha muda kilichowekwa kwa hoja ya kuwa ni mazoea mapya haitoshi kuwa hoja.

Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala. Unapokaimu nafasi unakuwa na madara yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako. Hakuna hoja ya kumridhisha mtu au la. Makamu wa Rais anapokaimu nafasi ya Urais wakati Rais hayupo kwa mujibu wa sharia ana madara yote ambayo ameruhusiwa kuwa nayo kwa mujibu wa Katiba. Na hili ni kweli kwa mtu mwingine yeyote ambaye Rais anaweza kumpa nafasi ya kukaimu jambo lolote kwa niaba yake. Mtu yeyote professional hajali sana kama atamfurahisha mtu au la atafanya kwa mujibu wa madaraka aliyopewa. Mtu ambaye atajali kuwa akifanya jambo Fulani atamuudhi aliyemteua au chombo cha juu hafasi kushika nafasi hiyo.

Somo ambalo Kabudi angepaswa kulitoa na labda wengi wanalihitaji kulielewa ni hili la Presidential prerogatives..
Nikukosoe hapo ulipozungumzia hoja ya pili!Kwanz umechanganya mambo mawili,Makamu wa Rais anapokaimu nafasi ya Rais anakuwa anajua yupo kwa muda mpaka Rais atakaporesume ofisi!Hapo Makamu anakuwa anajua yuko kwa muda mfupi tu na kuwa mwenye kiti atarudi!Anakuwa anafahamu fika hicho kiti hawezi kukikalia akawa Rais wa nchi!Tofauti na Jaji kukaimu,anajua hiyo nafasi ameishika kwa muda na anaweza ipata moja kwa moja au akaambiwa akae pembeni kwa matakwa aliyemkaimisha!Katika mazingira kama hayo,automatically Jaji huyo ni rahisi kutenda kwa matakwa ya aliyemuweka kwa maana anajua muda wowote ataambiwa fungasha!Leo Magufuli amesema amemtimua profesa mmoja Udom baada ya kugundua alimsema vibaya!Hilo tosha linaonesha jinsi gani Rais alivyo,akasisitiza hawezi mteua mtu halafu akamwacha tu amseme vibaya!Picha hiyo ndio inamjia mtu ambaye ameteuliwa kukaimu kwa muda,anajua tu kama kuna suala la utendaji basi lazima ataegemea upande wa aliyemteua ili endelee kukaimu!Hiyo ni logic iliyo wazi!
Ulichoongea umeongea as if kila mtu ni mwenye kusimamia kile anachokiamini,si kweli!Tumeona wengi wakijitoa ufahamu sababu ya kunogewa na madaraka!
Kwenye hiyo hoja umeingia cha kike,rudi ujipange!
 
..yes.

..siyo jambo la ajabu kwa mwanachama kutokubaliana na baadhi ya maamuzi ya chama chake.

Sasa mbona CCM wakitofautiana huwa mnasema imepasuka au waliokuwa tofauti wameonewa?
 
Umeeleza vizuri. Ndio yaleyale ukihoji kwa nini kafanya hivi utajibiwa kuwa katiba inamruhusu. Hata kama atafanya ujinga ina maana watu wasihoji!?

Nikukosoe hapo ulipozungumzia hoja ya pili!Kwanz umechanganya mambo mawili,Makamu wa Rais anapokaimu nafasi ya Rais anakuwa anajua yupo kwa muda mpaka Rais atakaporesume ofisi!Hapo Makamu anakuwa anajua yuko kwa muda mfupi tu na kuwa mwenye kiti atarudi!Anakuwa anafahamu fika hicho kiti hawezi kukikalia akawa Rais wa nchi!Tofauti na Jaji kukaimu,anajua hiyo nafasi ameishika kwa muda na anaweza ipata moja kwa moja au akaambiwa akae pembeni kwa matakwa aliyemkaimisha!Katika mazingira kama hayo,automatically Jaji huyo ni rahisi kutenda kwa matakwa ya aliyemuweka kwa maana anajua muda wowote ataambiwa fungasha!Leo Magufuli amesema amemtimua profesa mmoja Udom baada ya kugundua alimsema vibaya!Hilo tosha linaonesha jinsi gani Rais alivyo,akasisitiza hawezi mteua mtu halafu akamwacha tu amseme vibaya!Picha hiyo ndio inamjia mtu ambaye ameteuliwa kukaimu kwa muda,anajua tu kama kuna suala la utendaji basi lazima ataegemea upande wa aliyemteua ili endelee kukaimu!Hiyo ni logic iliyo wazi!
Ulichoongea umeongea as if kila mtu ni mwenye kusimamia kile anachokiamini,si kweli!Tumeona wengi wakijitoa ufahamu sababu ya kunogewa na madaraka!
Kwenye hiyo hoja umeingia cha kike,rudi ujipange!
 
Na wewe unadhani upo within a context perimeter?

Soma mada kuu, soma posts zangu kwa kituo then judge yourself if you believe you're within a proposed perimeter based on my posts and your argument!

It's not a matter of belief. It is a matter of facts and reasoning and empirical proof
 
Kumbe unatamani kuwa mtoto wa tajiri? chakarika na wewe uwe kama Lowasa ili familia yako ije kujisikia.
Ina maana baba yangu siyo nyumbu tena? Umeogopa kusikia Lowassa baba yangu hivyo naye ni nyumbu pia😀😀😀😀
 
Sasa mbona CCM wakitofautiana huwa mnasema imepasuka au waliokuwa tofauti wameonewa?

..binafsi sijawahi kusema ccm imepasuka.

..nyuma ya ccm kuna dola, hiyo inaweka nidhamu hata pale wanapotofautiana.

..kwa maoni hayo siyo rahisi kwa ccm kupasuka.

..kuhusu kuonewa ni pale ambapo unaona hatua za kinidhamu zinachukuliwa kwa baadhi ya wanachama, huku wengine waliofanya makosa kama hayo hawachukuliwi hatua.

..Kuonea ipo hata ktk utoaji maoni hapa JF. Kwa mfano, wapo wanaomwandama Lowassa kwa ufisadi wa richmond, lakini wanamuonea haya dikteta uchwara kwa ufisadi wa kuuza nyumba za serikali na kununua meli mkweche. Binafsi naona wote ni mafisadi tu.
 
Nimesikiliza kwa makini kile kinachoitwa "darasa" la Prof. Kabudi jana Bungeni kuhusiana na suala la Kaimu Jaji Mkuu na hasa hoja nzima ya kukaimiwa kwa nafasi ya Jaji Mkuu. Inasikitisha kwanza kwamba kuna watu wanasifia kuwa ametoa "darasa" na kwamba watu walikuwa wanamsikiliza kama wanafunzi katika Shule ya Msingi Mtakuja!

Je, ni kweli kile alichokisema watu walikuwa hawakijui? Ni kweli wabunge na wanasheria walioko Bungeni walikuwa hawajui yale yaliyokuwa yanasemwa?

Kuna hoja ya kuuliza swali; kwamba - kwanini Rais amemteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu kwa muda wote huu. Swali ambalo halipaswi kuulizwa na tulilikataa wakati ule ni kuhusu mamlaka ya Rais kumteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu. Hili liko ndani ya mamlaka ya Rais (Presidential prerogative). Lakini pia swali hili kwa ukubwa wake halipaswi kuulizwa isipokuwa kisiasa (political question) ili watu kupata hoja za kisiasa au ujiko wa kisiasa. Kwamba, mtu anataka kuonesha kuwa Magufuli amekosa mtu wa kuwa jaji mkuu, au kwamba Magufuli ana tatizo na mahakama n.k. Hili si jambo sahihi; wabunge kama wanaona Rais anatumia muda mrefu kujaza nafasi ya jaji mkuu wana uwezo wa kubadilisha sharia na hata Katiba chini ya Ibara ya 100 ya Katiba yetu.

Kama wanataka nafasi ya Jaji Mkuu isikaimiwe indefinitely (kama hoja ya Lissu ilivyoashiria) namna pekee ni kubadilisha Katiba au sheria ili kuweka kikomo kama ilivyo katika baadhi ya nafasi za utumishi wa umma ambapo sheria inasema mtu atakaimu nafasi kwa muda fulani na baada ya hapo basi mtu wa kudumu ateuliwe au aliyekaimu athibitishwe. Wao wabunge (watunga sheria na wanaoweza kufanya mabadiliko ya Katiba) wanaweza kuweka kikomo labda kwa ajili ya mustakabali)

Kama kwa mfano Rais angejaza cheo cha Ujaji siku moja tu baada ya Jaji Othman kustaafu wapo ambao labda wangeweza kuja na hoja ya kwanini amejaza nafasi haraka bila kuonesha tafakari sana au klutumia muda kufanya utafiti wa kutosha! Lakini pia kuna swali ambalo inabidi liulizwe kwa wale wanaolalamikia - kwa Rais kuweka Kaimu Jaji Mkuu ni shughuli gani ya Mahakama Kuu ambayo haiwezi kufanyika sasa hivi kwa vile kuna kaimu Jaji Mkuu au ni kitu gani hakifanyiki katika mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambacho kinapaswa kufanywa na jaji mkuu peke yake. Hili ndilo linaweza kuwa hoja ya kwanini inahitajika Jaji Mkuu na siyo Kaimu Jaji Mkuu?

Lakini kung'ang'ania kitu ambacho wote wanajua hakipo - kwamba Rais hajavunja sheria wala Katiba, na kuwa hakuna kikomo cha muda kilichowekwa kwa hoja ya kuwa ni mazoea mapya haitoshi kuwa hoja.

Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala. Unapokaimu nafasi unakuwa na madara yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako. Hakuna hoja ya kumridhisha mtu au la. Makamu wa Rais anapokaimu nafasi ya Urais wakati Rais hayupo kwa mujibu wa sharia ana madara yote ambayo ameruhusiwa kuwa nayo kwa mujibu wa Katiba. Na hili ni kweli kwa mtu mwingine yeyote ambaye Rais anaweza kumpa nafasi ya kukaimu jambo lolote kwa niaba yake. Mtu yeyote professional hajali sana kama atamfurahisha mtu au la atafanya kwa mujibu wa madaraka aliyopewa. Mtu ambaye atajali kuwa akifanya jambo Fulani atamuudhi aliyemteua au chombo cha juu hafasi kushika nafasi hiyo.

Somo ambalo Kabudi angepaswa kulitoa na labda wengi wanalihitaji kulielewa ni hili la Presidential prerogatives..

Ni kweli kwamba sheria huhalalisha jambo, kama ulivyoeleza. Ni kweli pia kwamba SI kila jambo ambalo linafanywa kwa mujibu wa sheria na Katiba ("bila kuvunja Katiba na Sheria") ni halali. In other words, a purely legal action can be illegitimate. Similarly, a purely illegal action can be legitimate. Kwa mfano, sheria inayokataza watu kutoa maoni yao haiwezi kuwa halali (legitimate) na kila mtu ana moral responsibility kupinga sheria ya namna hiyo. Inaweza kuwa ni kuvunja sheria (illegal) kutoa siri za serikali lakini kama siri hizo zinahusu jambo ambalo litakuwa na madhara makubwa kwa watu, ni halali na wajibu (moral responsibility) kutoa siri hiyo ili kuepusha madhara kwa watu. Kusema tu kwamba Rais hajavunja Katiba wala Sheria kuendelea kuwa na Kaimu Jaji Mkuu si hoja madhubuti na hakuhalalishi mapungufu yaliyoelezwa na Wakili Tundu Lissu.
 
Jibu zuri sana lakini halisemi tatizo hasa ni nini zaidi ya watu kuonekana kulalamika tu bila sababu ya msingi. Kama Rais hajavunja sheria, hajavunja Katiba, hatumia madaraka vibaya ni kwanini watu wanataka afanye jambo ambalo anapanga kulifanya anyway?
 
Katika mazingira kama hayo,automatically Jaji huyo ni rahisi kutenda kwa matakwa ya aliyemuweka kwa maana anajua muda wowote ataambiwa fungasha!Leo Magufuli amesema amemtimua profesa mmoja Udom baada ya kugundua alimsema vibaya!Hilo tosha linaonesha jinsi gani Rais alivyo,akasisitiza hawezi mteua mtu halafu akamwacha tu amseme vibaya!Picha hiyo ndio inamjia mtu ambaye ameteuliwa kukaimu kwa muda,anajua tu kama kuna suala la utendaji basi lazima ataegemea upande wa aliyemteua ili endelee kukaimu!Hiyo ni logic iliyo wazi!

Kama haya ni malalamiko ya Jaji Ibrahim; na kama anaona hawezi kufanya kazi kwa weledi kwa vile anachelewa kuthibitishwa au uwezekano wa kuteuliwa mtu mwingine unaweza kumvuruga mbona si lazima awe Kaimu Jaji Mkuu; anaweza kabisa kumuomba Rais ajiuzulu ili Rais ateue mtu mwingine. Hivi, kwanini unafikiria Jaji Ibrahim na weledi wake wote ni mtu petty sana kuhusu hivi vyeo?

Ulichoongea umeongea as if kila mtu ni mwenye kusimamia kile anachokiamini,si kweli!Tumeona wengi wakijitoa ufahamu sababu ya kunogewa na madaraka!
Kwenye hiyo hoja umeingia cha kike,rudi ujipange!

Umejuaje kama Prof. Ibrahim ni mtu wa namna hiyo? kwamba siyo professional enough kuweza kusimamia kiapo chake kwa muda wote ambao anakaimu cheo hicho?
 
Back
Top Bottom