Daraja jipya la Kiyegeya limejengwa kwa teknolojia ya kisasa ambayo imetumika kujenga fly over ya Ubungo

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107

Kiyegeya 1.jpg

Mhandisi Musa Kaswahili ambaye ni Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro anasema: "Machi 03, 2020 daraja lililokuwepo katika eneo la Kiyegeya lilibomoka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha barabara hii muhimu ya kitaifa na kimataifa (Morogoro - Dodoma) kujifunga.

"Serikali iliiingia katika mpango wa dharura na kutenga fedha haraka kwa ajili ili kujenga daraja jipya la Kiyegeya (lililopo wilayani Gairo), Novemba 05, 2020 utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa daraja jipya la Kiyegeya ulianza kupitia mkandarasi CDI contractors wa Morogoro chini ya usimamizi wa Kitengo cha Wahandisi washauri wa TANROADS Morogoro kwa kushirikiana na TANROADS Makao makuu.

Kiyegeya 2.jpg

Kiyegeya 3.jpg

"Barabara ya Ludewa hadi Kilosa ni sehemu ya barabara ya mkoa ambayo inaanza Dumila hadi Mikumi kilometa 142.”

Daraja hilo ujenzi wake umetumia teknolojia ya kisasa ambayo imetumika katika ujenzi wa fly over ya Ubungo (Kijazi Interchange) na kwa kutumia viwango vya kimataifa.

Amesema “Hapo awali kabla ya ujenzi wa barabara ya Dumila hadi Kilosa, ilikuwa kutoka Dumila hadi ludewa unatumia saa tatu lakini kwa sasa ni takribani dakika 40 tu.”

Aidha, ameongeza kuwa Mkoa wa Morogoro una madaraja takriban 2,029, huku mtandao wa barabara ukiwa takriban kilometa 2,070. Serikali inaendelea kutenga fedha ili kuhakikisha barabara hizi zinahudumiwa ili kuweza kuhakikisha kwamba zinapitika muda wote na majira yote ya mwaka.
 
Kidumu Chama cha Mapinduzi
 
Back
Top Bottom