DAR: Zitto Kabwe(Mb) akamatwa na Polisi akiwa Uwanja wa Ndege akitokea Kigoma

Awe Mpole tu sasa Kijana Zitto

Vinu vyake vya kinyuklia Mwandiga vimeshateketezwa kwa Moto

Hana Ujanja Tena Leo tu kakamatwa Kama Masogange au Chidi Benz Airport
Njia rahisi ya kumpiga Adui ni kuteketeza ghala lake la Silaha
 
068f1665808bf172f697918eaa0055fb.jpg


Nimeanzisha thread ya kuhusu hii post ya zito mda mfupi uliopita naona wenye mtandao wao wameifuta thread yangu, jf bana, acheni uwoga
 
Dhalimu ndivyo alivyo! Eti anainyoosha nchi kumbe madudu matupu!

Ndo taarifa zinavyodai...

======

TAARIFA KWA UMMA

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege wa JNIA, Dar es Salaam wakati akitoka Kigoma.

Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake.

Abdallah Khamis
Afisa Habari - ACT Wazalendo

======

UPDATE:

Zitto atasafirishwa kwenda Dodoma kesho tayari kwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo
 
Ndo taarifa zinavyodai...

======

TAARIFA KWA UMMA

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege wa JNIA, Dar es Salaam wakati akitoka Kigoma.

Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake.

Abdallah Khamis
Afisa Habari - ACT Wazalendo

======

UPDATE:

Zitto atasafirishwa kwenda Dodoma kesho tayari kwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo



Serikali ina data zote za hawa wasaliti wa nchi, wacheni tu wakamatwe kwani hawana faida na nchi yetu wala majimbo yao.
 
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanj a wa ndege wa JNIA, Dar es salaam wakati akitoka Kigoma.

Kwamujibu wa Afisa habari wa chama hicho Abdallah Khamisi amesema Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake.
 
Ndugu kuna mambo yanakasirisha sana kiwango ambacho hata tusi kubwa halitoshi kuonesha hasira hiyo ndipo tunatumia maneno ya kihenga tu kuonesha namna hasira zilivyotujaa!
Just imagine kwa upande mmoja watu hawana maji tokea uhuru, kuna vijiji hadi leo umeme wanausikia tu kwenye vituo vya redio,kuna kata na wilaya zizizo na huduma za kuridhisha za afya, na huduma duni ama kutokuwepo na miundombinu kabisa ya elimu ila mijitu mingine iliyopewa dhamana unakuta iko so busy kupiga ramli fulani kasema nini na mwisho wa siku ni kutumia rasilimali fedha na watu kusafiri angani kwenda kwenye kesi ambazo mshitakiwa anasema hapana na kesi inakwisha...yaani( tusi kubwaa)


hahahahahahaha jaman nakufeel ulichoandika uwi ngj nicheke kwanza ! mie kinachonichosha zaid watz ni waoga jaman tushazoea kulalamika inaishia hapa yaan sisi wajukuu zetu watatulaumu sana sana ! nimecheka na tusi la mwisho jaman kha!

ila police na wakubwa wao nao wanavuta bangi si bure
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi kuna haja gani kuendelea kuwa na Bunge ilhali wabunge wanakamatwa na Polisi kwa makosa ya kikanuni Bungeni?
Ama ndio maisha ya porini kila mwenye nguvu anaonesha meno na makucha yake?
Hadhi na thamani ya Bunge inashuka kila uchao maana mtaani hatutofautishi kukamatwa kwa kibaka mwizi wa simu na waheshimiwa
 
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amekamatwa na jeshi la polisi usiku huu katika uwanja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam akitokea Kigoma.

Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa chama chake na kusema kuwa kwa sasa wanasheria wa chama hicho wanafuatilia kujua sababu ya kiongozi wa chama chao kukamatwa na jeshi la polisi.

"Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege wa JNIA, Dar es salaam wakati akitoka Kigoma. Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake" alisema Abdallah Khamis

Asubuhi ya leo kulikuwa na taarifa kuwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashililah alitoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata Mbunge huyo wa Kigoma Mjini na kutakiwa kumfikisha mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kauli ambazo amewahi kuzitoa juu ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Job Ndugai pamoja na Bunge lenyewe.
 
Now Tupo East Germany Kwa Sasa!
Wenzetu Wameshatoka Huko, Sisi Ndiyo Tunaingia sasa! Bado Kujengewa Huo Ukuta Wa Berlin tu tena....
 
kamati ya bunge inapelekewa watuhumiwa, asipohojiwa siku hiyo na kupangiwa kesho, anapelekwa wapi? Wabunge wana adhabu zao kutoka kamati hizi, au zimekuwa mahakama?
 
Back
Top Bottom