DAR: Zitto Kabwe(Mb) akamatwa na Polisi akiwa Uwanja wa Ndege akitokea Kigoma

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,483
2,000
Ndo taarifa zinavyodai...

======

TAARIFA KWA UMMA

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege wa JNIA, Dar es Salaam wakati akitoka Kigoma.

Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake.

Abdallah Khamis
Afisa Habari - ACT Wazalendo

======

UPDATE:

Zitto atasafirishwa kwenda Dodoma kesho tayari kwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo.

UPDATE 2:

Polisi wanasema madereva wametoka Dodoma usiku huu na gari la Bunge na wanatarajiwa kuingia saa nane Usiku. Zitto kasema haendi na gari Dodoma kwa madereva waliokuja usiku kwani hawaamini kama hawana ndege, yeye yupo tayari kulipa gharama lakini haendi na gari.
 

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,723
2,000
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akamatwa na polisi usiku huu, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), akitokea Kigoma. Kusafirishwa Dodoma kesho tayari kwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa athibitisha.
 

Othmorine

JF-Expert Member
Jul 25, 2014
694
1,000
Ndo taarifa zinavyodai...

======


TAARIFA KWA UMMA

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanj a wa ndege wa JNIA, Dar es salaam wakati akitoka Kigoma.

Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake

Abdallah Khamis
Afisa Habari - ACT Wazalendo
Aiseee....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom