Uchaguzi 2020 Dar: Yaliyojiri Kawe kwenye Mkutano wa kufunga kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Wakuu leo ndio hitimisho la kampeni nzito sana za Tundu Lissu zilizovurumishwa nchi nzima , kwa mafanikio makubwa sana , kwa tathmini ya Kisomi niliyoifanya Tundu Lissu anatarajiwa kushinda Urais wa Tanzania kwa angalau 70% ,

Hitimisho la kampeni hizi linafanyika Jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Tanganyika Packers , Jimbo la Kawe , na taarifa inaonyesha kwamba maandalizi yote yamekamilika.

Kama Kawaida mimi mtumishi wako nitakuletea kila kinachojiri kwa kila nukta , endelea kubaki hapahapa JF kwa taarifa za Uhakika

" RAIS MPYA OYEEE , TANZANIA MPYA OYEEE "




Subpost 1 - KAWE ( 640 X 640 ).jpg

Chagua Chadema Chagua Tundu Lissu  Chagua wabunge wengi wa Chadema.   Chagua Mad ( 640 X 640 ).jpg



==========

Taarifa kutoka Kilimanjaro Airport zinadokeza kwamba Mamlaka ya anga imechelewesha makusudi kibali cha Lissu kutua DSM , Hata hivyo Lissu amelazimisha kuruka bila kibali hicho ili kuwahi mkutano Jijini DSM , amesema Liwalo na liwe .

Hii njama ya kishamba ndio ilitumika kumzuia Lissu kutua Mtwara , lakini safari hii imegonga mwamba

Halima Mdee: Wamesha tepeta. Wanabadilisha majina tu, Mara Rashida. Kawe hatujawahi kupata Ushindi kilahisi. Kesho hadi kesho kutwa ndo kazi tutafanya. Kwenye Kampeni ilikuwa kawaida.

Boniface jacob: Wasiwadanganye, eti mkichagua Upinzani hawaleti Maendeleo. Ile flyover ya Ubungo ipo Chato? Barabara ya njia nane ipo Chato? Vyote vipo Ubunge na Mimi ndo nlikuwa Meya.

Mke wa Lissu: Kazi tumeifanya kilichobaki ni kesho. Kesho tukachague Madiwani, Wabunge na Tundu Lissu.

Tanzania tunayoipenda Imeugua kwa Miaka Mitano

Mnyika: Kuna mbinu chafu za kutaka Lissu Asishinde.

1. Nmedokezwa, kuna njama za kuzuia mawakala wetu kuingia kwenye vituo vya kupigia kura mapema. Muda wa kubembeleza Tume umekwisha Jana.

2. Wanataka Mawakala wetu wasiingie na simu. Nasema mawakala wetu waingie na simu. Kanuni kazijakataza.

3. Sirro kasema wakipiga kura watu waende nyumbani. Nasema tukipiga kura hakuna kwenda nyumbani.

4. Wamepanga kutompa wakala fomu ya matokeo na kubandika matokeo feki. Nasema hivi hakuna msimamizi kuondoka hadi Wakala wetu apate fomu ya matokeo.

5. Kanuni inasema watu waanze kutangaziwa kura za urais. Wamekuwa wakianza na diwani.

Magufuli alijua Tume itahesabia kura dodoma. Akakimbilia Dodoma. Majumuisho kitaifa yatafanyikia hapa Dar. Watu wa Dar tutaongozana kwenda mjini Centre kuhakikisha matokeo yanatangazwa.

Salum Mwalim: Nchi hii tumeona kuna shida ya maji.

Wachimbaji wadogo wanaminywa.

Majengo ya Hospital hayana Madawa, vitendea kazi wala Wataalam

Wafanyabiashara wanaingiliwa kwenye account zao na kuchukuliwa pesa zao.

Mzazi akijifungua hakabidhiwi mtoto hadi ajifungue(Tabora hupewi mtoto hadi ulipie elfu 45 hadi elfu 50)

Wafanyakazi hawajaongezewa mishahara.

Watu wanalazimika kuhamisha mitaji yao.

Makampuni mengi yamefungwa. Kila kazi ni JKT.

Muda kwa kufanya maamuzi ni kesho. Kesho tukapige kura.

Magufuli ameshaanguka. Ni kwenda kumaliza kazi. Waliosema haiwezekani, imewezekana.

Nawashukuru sana Watanzania pote nilipopita wakati wa Kampeni. Nashukuru chama changu. Tunawatakia Uchaguzi mwema kesho

Kila mtu ajiandae kisaikolojia kwamba rais anayekuja na Tundu Lissu

====

Tundu Lissu: Tumerudi tena baada ya miezi Miwili.

Kesho ni siku ya hukumu. Kesho ni judgement day.

Viongozi wa vita katika zama zote za kihistoria. Wamekuwa wakiwaandaa watu wao kwenda kwenye Mapambano ya mwisho.

Naomba nizungumze nanyi ili kuwaandaa kwa siku ya hukumu ya kesho.

Baada ya mazungumzo na Watanzania Nchi nzima. Hakuna mkoa ambao hatujaenda. Baada ya kuwasikiliza wananchi wa Tanzania na baada ya kuwaeleza maono yetu. Hiki nacho taka kukieleza ni hoja za Mwisho.

Katika miezi hii miwili, tumeona na kusikia mambo mengi sana. Tumefundishwa mambo mengi sana na Watanzania. Na sisi tumefundisha kiasi.

Imenithibitishia kwamba wala Watanzania sio wajinga, sio waoga sio kwamba hawajui kinacho endelea.

Watanzania Wamechoka, wana hasira na wapo tayari kwa siku ya kesho.

Baba mwamakula tumekuwa naye muda wote, shehe Rajab Katimba tumekuwa naye, Shehe Ponda Issa Ponda tumekuwa naye katika safari hii. Tuwapigie Makofi viongozi wetu wa kiroho. Asanteni kwa kutuombea. Tuwashukuru Madereva, Walinzi. Bila wao watanzania wangetugawana.

Kampeni yetu haikuwa rahisi. Namna peke ya mawasiliano ilikuwa mtandao yakijamii. Vyombo vingine, TV, Magazeti, yaligoma kuonesha mikutano yetu.

Nashukuru wandishi wa habari wa Mitandaoni.

Historia itarekodi, hatukwa na mabango ya mhombea urais hata moja. Watanzania walikuja wenyewe kwenye mikutano yetu. Licha ya mapungufu ya Rasilimali, tuliwakimbiza mchaka mchaka. Licha ya Umasikini wetu wa rasilimali kweye mahakama ya Umma tumewapiga CCM.

Yule ambaye alikuwa mbabe kwa miaka mitano safari hii amepiga magoti

Yule anayejifanya Mbabe, leo kashindwa hata kufanya mkutano wa kufunga Kampeni.

Yule mwenye vyuma mwilini, bado nipo fiti hata mkiongeza wiki mbili.

Watu zaidi ya 400 wameuawa. Mkuranga kibiti rufiji Kilwa, watu zaidi ya 400 wameuawa na Serikali haijawahi kusema. Wamekufa katika kipindi cha miaka 5. Nani anayesema hiyo ni amani.

Wilaya ya Nkasi mpaka kigoma, wavuvi wanauawa na Askari wa Tanapa wanatumbukiwa Ziwa Tanganyika.

Ukanda wa ziwa Victoria Misenyi kadi sirari ni misiba kila mahali.

Tulienda nyumbani kwa Magufuli Chato. Tumepewa majina ya wavuvi 62 wameuawa baada ya kwenda kuvua samaki kisiwa cha Rubondo.

Tumekwenda Nkome Geita vijijini. Wakatuambia hapa Nkome Wavuvi wanapigwa risasi wanatumbukizwa majini.

Kama hii ndio amani, tutafute maana nyingine.

Kuna kilio cha wafugaji wanatupwa Mtoni, huliwa na mamba. Ukisema amani wakati watu wanakufa hivi maana yake unataka yaendelee.

Wakulima, wavuvi wafugaji ni Masikini watupu.

Mtwara walipelekewa Majeshi kisa Korosho yao. Watu wakapigwa, wakauawa kisa korosho

Wataalam wetu wametuambia kesho Watanzania watapiga kura, kuiondoa CCM madarakani. Wataalam wetu wamesema Kati 65% hadi 70% Wataikataa CCM.

Wataalam wetu wamesema tutapata Wabunge wengi kuliko CCM.

Idaddi ya jumla ya kura ya Wabunge wetu, watapigiwa kura nyingi kuliko ya CCM.

Kesho ni D day. Judgment day.

Askari wetu wa kwanza ni Mawala wetu.

Tunawategemea Mawakala wetu. Tunawatazamia wawe macho kuliko kipindi kingine chochote

Tuwalinde Mawakala wetu tukiwa nje ili watulindie kura zetu. Mawakala wakivurugwa wasaidieni..

Tunaambiwa kuna kura zimeshapigwa na kuhesabiwa tayari.

Tunaambiwa tume tayari ina kura milioni 12 za Magufuli na Mil 3 za Magufuli. Na Watatangaza tarehe 29.

Kama hii ikitokea tarehe 29 wakatangaza matokeo ujue huo ni wizi ingieni barabarani mdai haki zenu. Msisubiri Tundu Lissu aseme, ingieni barabarani nchi nzima.

Kutangaza matokeo wakati majumuisho hayajaisha kwenye majimbo, ni kuleta fujo.

Jaji Mihayo na Mahera mnaingia ICC.

Wakitangaza matokeo tarehe 29 waksti maheabu hayajakamilika, ingieni barabarani. Msisubiri Lissu wala Mbowe aseme.

Wanategemea Jeshi. Polisi wamedhurumiwa kwa miaka mitano. Wanajeshi wanaolinda mipaka yetu wamekatwa hela za chakula.

Narudia wito wangu kwa wanajeshi wa nchi hioi

Kumbukeni kiapo chenu mbele ya baba wa Taifa. Kwamba nyie ni jeshi la watanzania na hamtageuza Silaha zenu kwa Watanzania.

Tuachieni Maguli tumalizane kesho

Hao wanaowatuma kuwaua watu Zanzibar. Nmeomba Mawakili wangu waandike barua. Nmemuagiza Bob Amsterdam aandike barua kwenda ICC kuanza Uchunguzi kwa haya mauaji ya Zanzibar.
Chagua Chadema Chagua Tundu Lissu  Chagua wabunge wengi wa Chadema.   Chagua Mad ( 640 X 640 ).jpg
Subpost 1 - KAWE ( 640 X 640 ).jpg
Subpost 1 - Dar es Salaam...  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania k ( 359 X 640 ).jpg
DAR ES SALAAM ( 426 X 640 ).jpg
IMG_20201027_170745_969.jpg
IMG_20201027_170801_088.jpg
IMG_20201027_170752_557.jpg

 

Attachments

  • VID_20201027_171733.mp4
    6 MB
Tunamtakia Kila la Heri Rais wetu wa awamu ya sita Mh Tundu A. Lissu. Watanzania walio wengi wameumizwa sana na utawala unaomaliza muda wake ila wanyonyaji wachache tu ndiyo hawaelewi.

Mkuu Erythrocyte asante sana kwa taarifa toka mwanzo wa kampeni hadi sasa, pamoja na kamanda Molemo na wengine wote waliotuhabarisha kuhusu kampeni za Mgombea wa Urais kupitia CDM.

Pamoja na vyombo vyote vya Habari kupigwa mkwara na waandishi wao Kufyata kuna wengine waliamua kusonga mbele.
 
Back
Top Bottom