Dar: Waziri Gwajima, Mkenda na Simbachawene wakutana kujadili Ukatili kwa Wanafunzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,816
11,992
Mawaziri watatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Desemba 21, 2022 wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili kuhusu suala la ukatili kwa wanafunzi wa shule na vyuo na kuweka mikakati ya kupambana na ukatili huo.
IMG-20221221-WA0026.jpg

Mawaziri hao, Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia naMhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana kulifanyia kazi suala la kuzuia ukatili dhidi ya watoto.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mkenda amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Kamishna wa Elimu ndio yenye jukumu kisheria la kutoa miongozo mbalimbali ya wanafunzi hivyo ina jukumu pia la kushiriki katika kuwalinda dhidi ya ukatili.

"Kikao hiki kitatusaidia kuongeza nguvu, badala ya kutumia Mwongozo wa Kamishna wa Elimu pekee ni vizuri akae na wataalamu kutoka Wizara nyingine husika ili kuangalia udhaifu upo kwenye miongozo au katika kuratibu utendaji na kisha kutolea taarifa," amesema Waziri Mkenda.

Mkenda ameongeza kuwa Wizara ya Elimu inalo jukumu la kusimamia mpaka ngazi ya vyuo, hivyo mipango na mikakati itakayowekwa itaangalia ngazi hizo pia.

"Ni ukweli watoto wetu wanatumia muda mrefu katika shule na vyuo hivyo ni wajibu wetu kama walezi kuhakikisha huko kunakuwa mahali salama kwa watoto," amesema Prof. Mkenda.

Kwa upande wake Mhe. Gwajima amesema kuwa ameshukuru kuungana katika mapambano dhidi ya ukatili, akitoa mfano mwaka 2021 takwimu zinaonesha jumla ya watoto 11,499 wamefanyiwa ukatili ikiwemo ubakaji, ulawiti na wengine kupata mimba za utotoni.

"Hao ni chini ya asilimia 15 ya walioripoti visa hivyo, ukatili huo ni pamoja na ubakaji, ulawiti na wengine kuishia kupata mimba za utotoni. Ukiangalia ukubwa wa tatizo na ukizingatia si wote wanaoripoti tumeona kuna ulazima wa kuangalia kwa pamoja wapi tuimarishe ili kukabiliana na tatizo hili," amefafanua Dkt. Gwajima.

Ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa washiriki kwa kiwango kikubwa kwenye suala hilo kwa kuwa takwimu zinaonesha asilimia 60 ya ukatili wa jinsia kwa watoto unafanyika majumbani ambapo kuna wazazi.

Kikao hicho kiliongozwa na Mhe. Simbachawene ambaye amesema kuwa Serikali imeipa umuhimu wa pekee suala hilo na hivyo kukubaliana kwa haraka sana kabla shule hazijafunguliwa kuwe na mikakati ya kuwalinda watoto itakayoshirikisha Wizara, Taasisi na makundi yote muhimu.

Mhe Simbachawene ameelekeza Makatibu Wakuu wa Wizara hizo Tatu wakiongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kuhakikisha wataalamu wanaandaa mikakati ya muda mfupi na mrefu itakayojadiliwa na mawaziri na wadau.

"Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Elimu, OR - TAMISEMI, Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na makundi yote ikiwemo ya wazazi ni lazima kushirikiana ili tupate maoni na kila mmoja aone wajibu wake kuhusiana na suala hili la ukatili kwa watoto," ameongeza Mhe. Simbachawene.

Aidha, Waziri Simbachawene ameagiza Mawaziri wote wanaohusika kukutana Januari 4, 2023 kupitia mikakati iliyowekwa na maoni yaliyotolewa na kutoa mapendekezo

yatakayowasilishwa kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya kuridhiwa.

IMG-20221221-WA0028.jpg
 
takwimu zinaonesha asilimia 60 ya ukatili wa jinsia kwa watoto unafanyika majumbani ambapo kuna wazazi.
Sasa wizara ya elimu inahusikaje huko majumbani kulimaliza tatizo hili?

Halafu waziri Simbachawene anatapika kuwa kabla shule hazijafunguliwa kuwe na mikakati yaa kuwalinda watoto . Mikakati my foot!

Nchi hii hakunaga watu wanaolitafakari Jambo ama tatizo kwa kina chake na kuleta suluhu ya maana, kila kitu zima moto tu.

Hawa mawaziri wamekutana ili kesho waandikwe gazetini, lkn hakuna cha maana wanachokijadili.
 
Sasa wizara ya elimu inahusikaje huko majumbani kulimaliza tatizo hili?

Halafu waziri Simbachawene anatapika kuwa kabla shule hazijagunguliwa kuwe na mikakati yaa kuwalinda watoto . Mikakati my foot!

Nchi hii hakunaga watu wanaolitafakari Jambo ama tatizo kwa kina chake na kuleta suluhu ya maana, kila kitu zima moto tu.

Hawa mawaziri wamekutana ili kesho waandikwe gazetini, lkn hakuna cha maana wanachokijadili.
Mkuu ukishamaliza kutoa kasoro na wasiwasi basi ni busara kutoa na njia sahihi au ushauri wa nini wangepaswa kufanya hao mawaziri. Hilo lingesaidia sana kuliko kuishia kulalamika tu.
 



Bado huko kwa wenzetu utakuta kuna joint strategic partnerships za children safeguarding.

Pamoja na sera luluki na ku involve wataalamu kibao; mfano team ya safeguarding kila wilaya inataka iwe ina walimu, polisi, dr, nurses, community leaders. Na kila mtu hapo ni muhimu kama mwingine……..

Ni story ndefu sana ulinzi wa watoto ndani ya jamii na huko kwa wenzetu kuna masheria balaa. Lakini sio suluhisho hiyo vita 80% ni media propaganda za vitisho, namna habari inavyokuwa reported kuonyesha unyama uliotendeka (demonisation ya tukio) na adhabu kali ya kisheria ambazo ni consistent.

Huko kwa wenzetu media zimechangia sana watu kuwaogopa watoto.

Sasa tunaweza zani utani, lakini hiyo ni vita ya propaganda zaidi kushinda chochote, Simbachawene, Gwajima na Mkenda watakuja na suluhisho gani la hayo mambo wakati sera za safeguarding zipo, sikia tu sasa huo mziki wake wa usimamizi in practice.
 
Fungia mitandao ya Jamii. hamtaki TT Twitah n.k
Wakati wakiwa mashuleni.

Woga woga tuuu!
Makamu wa Raisi anaweza sema "Polisi wafanye uchunguzi"
ni hayo tu.

Isitoshe, hakuna jipya bali historia kujirudia. Twende na Wakati.

...nayasubiri matokeo.
 

Mambo ya Wazungu na Waafrika wapi na wapi.
Hakuna baya, lakini hatuko njia moja ....Wazungu bado wanajifunza "Ubinadamu"

Aluta Continua
 
Mambo ya Wazungu na Waafrika wapi na wapi.
Hakuna baya, lakini hatuko njia moja ....Wazungu bado wanajifunza "Ubinadamu"

Aluta Continua
Tunataka kujifunza namna wenzetu waliofanikiwa kwenye ulinzi wa watoto hatua zao na wanafanyaje mambo au tunataka kuangalia rangi zao.

Swala la ulinzi wa watoto sio lelema, I can guarantee you Dorothy, Adolph na Simbachawene ata wakae mwaka mzima awawezi kuja na majibu.

Those are technically matters ambazo wenzetu kila siku wanajifunza namna ya kuboresha ulinzi, pamoja na kuweka sheria kali bado yanatokea huko kwao.

Sisi ata baby steps za kisheria na kupambana na hayo mambo bado sana policy wise.
 
Back
Top Bottom