Serikali ya Mtaa Kawe: Kweli kuna kundi la Wahalifu wanatumia kivuli cha Ulinzi Shirikishi, wanatuchanganya sana

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mzimuni, Kata ya Kawe, Raiya Nassoro akifafanua kuhusu matukio ya Uhalifu maeneo ya Kawe katika eneo la Tanzania Packers.

Mtaa huo una Ulinzi Shirikishi ukiwa umegaiwa katika Mitaa saba, moja kati ya maeneo hayo ni eneo la National Housing, ni kubwa lakini wameweka walinzi wachache nadhani ni wawili au watatu.

Kipindi cha nyuma kuna waliokuwa wanachama wetu wa Ulinzi Shirikishi huku Kawe tuliwashtukia kuwa ni watu wa matukio, tukawafukuza kwenye Ulinzi Shirikishi na baadaye wakakamatwa kwa kufanya uhalifu, wapo waliofungwa miezi nane, wengine mwaka n.k

Kwa sasa wezi hao wametolewa kwa kuwa kesi zao zimeisha, hivyo kumekuwa na changamoto kadhaa mitaani kwetu za masuala ya usalama na watu hao ni sehemu ya wanaodaiwa kufanya uhalifu.

Sehemu korofi zaidi ni kwenye pori la Tanganyika Packers, likiwemo na lile la National Housing ambalo kuna majani mengi yameota na kuna wahalifu wanajificha maeneo hayo.

Kuhusu Ulinzi Shirikishi wapo na wanafanya majukumu yao lakini kuna watu wanaitwa Vishandu wanatusumbua sana, baadhi tumewakamata na wapo ndani.

Vishandu ni wezi ambao wanatumia Bodaboda wanatembea kwa makundi ya Bodaboda mbili, tatu au zaidi, wanachofanya ni wenzao wakiwa wanafanya uhalifu wengine wanawalinda wenzao.

Nitoe wito kwa Wananchi kushirikiana na viongozi pindi wezi wanapopelekwa Mahakamani washirki katika kusimamia kesi Mahakamani kwa kuw ani haki zetu za msingi, kwani kuwaacha kunasababisha Polisi wawaachie kwa kuwa hakuna usimamizi wa mwendelezo wa mashtaka.

Kundi la Waharifu Tanganyika Packers
Kuna kundi lina watu kati ya saba hadi nane pale eneo la Kwa Mwamposa, wanavaa magwanda na kujifanya wao ni Ulinzi Shirikishi lakini sio, wao ni wahalifu na wanawasimamisha watu kwa nia ya kuwakagua lakini kumbe ndio wahalifu wenyewe.

Niwaombe watu wawe makini, hakuna Shirikishi anayetembea akiwa na mapanga na marungu kama mharifu, tuwe makini nao, kundi hilo linatia dosari Ulinzi Shirikishi halali.

Tumepata ripoti kadhaa za watu kuibiwa na kundi hilo. Wote wanaofanya uhalifu huo hatutawaacha, yajayo yanafurahisha.

Chanzo: Times FM

Pia soma:

= Dar: Wahalifu wadaiwa kutumia jina la ‘Ulinzi Shirikishi’ kufanya uhalifu maeneo ya Tanganyika Packers

= IGP Wambura na PT yake wamelishindwa Pori Hatari kwa Uhalifu Tanganyika Packers Kawe!
 
popoma njoo ucopy huku story za kawe then uje na story yako ya kuwahadaa watu kwamba upo kawe. Story yako itakuwa ya uongo ila utamtajia Raiya Nassoro ili uonekane upo kawe kweli.

Utoto raha sana nyie
 
Na pale darajani mlalakuwa kawe jioni/usiku hapafI kabisa

Ova
 
Sasa Hao walinzi Shirikishi halisi Wana alama gani ya utambulisho ili watu waweze kuwatofautisha na hao "walinzi shirikishi wahalifu"?
Tofauti yao hasa ni ipi au zipi kati ya hao Walinzi shirikishi original na hao feki???
 
Ukiacha Kuingiliwa Kinyume utabadilika.
🤣🤣🤣🤣 mtukane popoma matusi yote lakini usimwambie hajawahi kufika dar. Ukweli unauma🤣🤣🤣 walaumu wazazi wako.

Ila jikubali mkuu mkataa kwao mtumwa. Mbona Miso Misondo katoka kwao huko Nachingwea lakini anatesa Dar now?
 
Kawe kuna mazingaombwe mengi!! Mwenyekiti wa mtaa nyumbani kwao ni hapo hapo karibu na daraja la Mlalakuwa, lakini hapo hapo ndio uhalifu unatenfeka!
Hao wanaoshitakiwa kuwanyanyasa watu karibu na viwanja anakohubiri Mwamposa , Mbona kuna kituo cha polisi kiko karibu. ; inakuwaje wanashindwa kuwathiniti?
Askari wa Kawe wanajulikana kwa kushirikiana na wahalifu na RPc wao Muliro yupo yupo tu kumdanganya Chalamila kuwa wanafanya kazi!
 
🤣🤣🤣🤣 mtukane popoma matusi yote lakini usimwambie hajawahi kufika dar. Ukweli unauma🤣🤣🤣 walaumu wazazi wako.

Ila jikubali mkuu mkataa kwao mtumwa. Mbona Miso Misondo katoka kwao huko Nachingwea lakini anatesa Dar now?
Ukiacha kuingiliwa kinyume utakuwa na Akili.
 
Back
Top Bottom