Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,658
- Thread starter
- #61
Nimepata sms asubuhi hii mdogo wangu amefariki kwa ajali ya basi lililokuwa linatokea Dar kwenda Mtwara. Maiti ziko hospital gani, aliyenipigia nimeshindwa hata kumuuliza sehemu ilipotokea ajali na jina la basi.
Hivi sasa simpati kwenye simu, simu ya bwana mdogo tangu jana haipatikani japo mchana akitoka Dar waliwasiliana na dada. Ma rafiki zake walioko Mtwara hata wao wanadai mawasiliano yalikata gafla.
Nisaidieni mlioko huko na tushamtuma dada yetu yuko njiani kwenda huko Mtwara na huku tukielekea stand kuanza safari.
Bwana mdogo!!! Tangulia ndugu yangu