Dar: Matukio na yanayojiri jijini...

Dar: Matukio na yanayojiri jijini...

Haya wa ILALA na kinondoni LETENI ZA KWENU
Mkuu Safari_ni_Safari, kama watu watanicheka acha wanicheke kwani ninachoeleza ndio ukweli. Hata kama nitaonekana mshamba poa tu. Ni watu wachache kama wewe ambao wanaweza kuwa na mtazamo tofauti kuhusu hili......nina siku chache tu Dar acha nizitumie vizuri.
 
Giraffe ya White Sand au wapi??
Mimi sio mwenyeji wa Dar, ila ni pale Temeke, mtaa unaitwa Sudan...usiniulize kwa nini panaitwa hivyo kwani utauchosha ubongo wangu kutafuta jibu.
 
Mkuu Safari_ni_Safari, kama watu watanicheka acha wanicheke kwani ninachoeleza ndio ukweli. Hata kama nitaonekana mshamba poa tu. Ni watu wachache kama wewe ambao wanaweza kuwa na mtazamo tofauti kuhusu hili......nina siku chache tu Dar acha nizitumie vizuri.

No disrescect to you sir...........umeleta events za wilaya ya TEMEKE ndio maana nikaomba hao wengine nao watujuze
 
No disrescect to you sir...........umeleta events za wilaya ya TEMEKE ndio maana nikaomba hao wengine nao watujuze
mkuu nashukuru sana kwa kunitia moyo ili niendelee na safari zangu za kulijua jiji. mtu anaweza kuwa temeke na asijue nini kinaendelea ilala, kiburudisho kwangu ni ili mtu asinidanganye eti "uwanja wa taifa upo karibu na ilala boma, au eti uko kigogo".napenda kuona vitu tofauti...Huwezi mwambia mtu wewe ni Mtanzania, unaishi Dar, halafu kiswahili hukijui, hiyo itakuwa ni aibu"
 
umekopi facebook. (Cheka upasuke)
Mkuu Mwitu, mimi ndio Thanda, niliahidi kuja Dar, na nimekuja Dar,,,haya ndiyo ninayoyaona na kuyashuhudia, huyo wa facebook kakopi kwangu ili kuwaonesha watu ushamba wangu ingawa mimi sio mshamba, ila ni mtu anayependa kuufahamu mji/jiji. Muulize Mwita Maranya, DefranceJf na Mystery watakwambia.
 
umekopi facebook. (Cheka upasuke)
LABDA KAMA MODS WAMEIUNGANISHA NA THREAD YANGU AU HUYU JAMAA KANIIBIA NA KUIHAMISHIA KWAKE...YANGU NI DarLive na hii nimeiita hivyo kutokana na tukio langu la kwanza kuliona eneo la DarLive kule mbagala, upande wa kulia kama unaelekea mbagala charambe. Dar kuna matukio jamani hadi humu JF mtu anadiriki kuchakachua ya wenzake..!!!!!!!!!!!nikirudi nyumbani nitasimulia.
 
kadri atakavyoendelea kukaa dar ataona mengi sana hata kuyaandika atashindwa ataamua kupotezea tu. kila la kheri
 
Dah! Huu ni utalii wa ndani...! BTW! Mbona TMK tu? Au ndiyo kwetu Mbagala?
Mbagala karibu na kituo kidogo cha polisi (Mbagala police post) kuna baa moja inaitwa annex,imepambwa na rangi ya bia ya kilimanjaro jana jioni mlo ulikuwa ni hapo...mhudumu akanywa na kulewa kuliko wateja wake, nakumbuka jina vile......anaitwa Pili (nimesikia wenzake wakilalamika), alilipwa hela na mteja sh 2000, akamuuliza mteja kwa sauti ya kilevi "hiii, hiii kama sh ngapi vile? mteja akamjibu elfu 10, aaaaaaaaaaaaaah kweli hii ni elfu 10 akamrudishia mteja change sh elfu 8, akamuongezea na tip ya sh elfu 5........nilicheka kidogo nife...Pata muda halafu ufike hapo.
 
kadri atakavyoendelea kukaa dar ataona mengi sana hata kuyaandika atashindwa ataamua kupotezea tu. kila la kheri
Iron Lady, ni kweli na ndio maana nafanya bidii kwani nina muda mchache hapa.....niacheni tu nifurahi..niongeze siku za kuishi.
 
Ndg zangu habarini za jioni! Jamani em nifundisheni ku-thread.
 
Wanajamii, niko Dar, Namba zangu za simu ni 0757 406 881, sijakutana na Mwita Maranya.....ushamba umenitoka kwa sehemu fulani. nimeshuhudia matokeo fulani fulani. nilifika hapa tangu tarehe 2.11.2012 nitaondoka tarehe 16.11.2012

Asante kwa wale walionipigia, tumeongea nimefurahi sana, mambo ya Dar ni makubwa

Yafuatayo ndiyo niliyoyashuhudia, Nikiongozwa na family friend wetu Khadija Mzanzibari, ni matukio ya siku tofauti tofauti, sio ya siku moja:

Temeke pale Sokota: Lori kubwa lililobeba kontena lilimkanyaga kondakta wake mguu umesagika, lilikuwa linapaki na yeye analiongoza.

Temeke eneo la KISUMA night Club: nyama ya mbuzi siyo fresh, machangudoa wote na mashoga bila kificho, Sijaona usalama wa kutosha jioni...kujiuza kwa wadada na wakaka ni jambo la kawaida hapo.

Tandale Sokoni: Vibaka wasio na uzoefu wakiwasachi watu

Nyuma ya The Girafe Hotel: Hapo kuna mtaa unaitwa Sudan, Nyumba imejengwa ina vyumba vidogo vidogo sana, wadada warembo wamekaa kila mtu mbele ya chumba chake kusubiria wateja. Ukifika hata usipoongea na yeyote we unaingia tu ndani na yule aliye mbele ya chumba chake anakufuata. Cha ajabu niliambiwa wote ni wahaya, na Mwenye hiyo nyumba kazi yake ni kuwasaidia kutafuta wateja. Wanakupa bei ya matumizi ya bila condom, matumizi ya condom, matumizi ya "njia ya haja kubwa" ila bei ni kuanzia TZS 2000 tu.

Sunrise Beach Resort, Kigamboni: niko na wife, nimepaki gari eneo sahihi akaja mdada mzuri sana na kuniambia kwa sauti ya upole "kaka unaweza kunipisha nipaki kwani hili ni eneo langu la siku zote, kabla sijajibu akapotea, nilishangaa sana.Tukahamia Kipepeo Beach Resort.

Tausi Guest House (Kwa nje) Kinondoni Morocco: Khadija Mzanzibari anatamani kitu, anashindwa kuniambia live,.."shem mi kuna kitu nakitamani sana" nini tena shem, namuuliza. yeye anaguna, halafu nami naanza kupata wasiwasi. "mpigie mkeo atakwambia, yeye nilishamwambia". Napata ahueni, nampigia wife, hayuko mbali, kaenda mara moja crdb bank kwa manyanya,,, "dad si nakuja" ananijibu. Khadija ananipa stori za Zanzibar, tunapata kinywaji,....wife huyu hapa kafika...."dad ni kweli Khadija alinieleza kitu, tumkubalie tu.....tunaondoka hadi Mbagala Annex, kwa Mr D. Tunaagiza chakula, na Khadija anaagiza chakula chake akipendacho...anakifurahia sana, "anasema now we can talk"

DarLive Ukumbini, Mbagala: Mrembo mmoja amelewa mchana na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine eti joto limezidi. Mara huyo kasimama ananiuliza "anko vipi, si ukanipe kimoja tu, namuuliza nini, ananiangalia...Khadija Mzanzibari akamuuliza"mbona unachotaka kumpa mi tayari nimeshampa?" yeye akajibu "ina maana utamu wote umeupata mwenyewe...kicheko pande zote, mi kimya.kidogo wife huyu hapa."dad twende zetu mambo ya Dar hutayaweza.

Temeke eneo la Kanisa la Wasabato: Nashuhudia umati mkubwa wa watu wakielekea usawa wa Temeke Hospital, eti kuna mtu amefumaniwa na mke wa mtu wakifanya mapenzi halafu wameng'ang'aniana...mara polisi hawa hapa, mabomu ya machozi kama kawaida.


Bado naendelea na michakato.

Hongera sana kwa ufukunyungu, mpaka uondoke hapa utakuwa umeandika book kama Bible. Ok, mtu wangu nikipata nafasi nitakutafuta.
 
Mimi sio mwenyeji wa Dar, ila ni pale Temeke, mtaa unaitwa Sudan...usiniulize kwa nini panaitwa hivyo kwani utauchosha ubongo wangu kutafuta jibu.
Utakuwa umetokea kusini.
 
Hongera sana kwa ufukunyungu, mpaka uondoke hapa utakuwa umeandika book kama Bible. Ok, mtu wangu nikipata nafasi nitakutafuta.
Uwe na amani ya kutosha mkuu, kuna maeneo mengi muhimu sijayatembelea....kuna jamaa kanipigia simu kanifurahisha sana..."eti nisisahau kumwona waziri wa mali asili na utalii" kuna zawadi yangu kwake,....haya bwana!!Nashukuru mkuu nitajitahidi ila sidhani kama yuko Dar.
 
Utakuwa umetokea kusini.
Kwa kutaja kusini unapata 30%...ila ni kusini ipi unayoiongelea mkuu? uko sahihi 30% tu, na ukicheza unawezakosa hata hizo 30%
 
Hongera sana kwa ufukunyungu, mpaka uondoke hapa utakuwa umeandika book kama Bible. Ok, mtu wangu nikipata nafasi nitakutafuta.
Mkuu hapo kwenye blue umeniacha.
 
Umesahau kuingia Girrafe Royal mida ya kuanzia saa 5 usiku. Kila siku ni ladies free. Utakutana na vichuchu vya kufa mtu.
Mkuu naendelea na Safari, ila hii ya watoa vyeti vya kuzaliwa ni rushwa,..... rushwa, rushwa......, nimefika Muhimbili Hospital, namuuliza mtu anioneshe wanapotoa vyeti vya kuzaliwa watoto, ananiambia twende kwani hata mimi naelekea huko. Tunafika getini, hapa kuna walinzi wawili wanaoelekeza watu mahali gani wakae. Kushoto kuna ofisi ndogo ya mapokezi na kibanda kidogo panauzwa soda. Bidhaa inayonunuliwa sana hapa ni kalamu....kila mtu yuko busy kujaza fomu aliyopewa...Kulia ni ofisi....makontena ya rangi ya krimu siyo meupe...ndipo yalipo mafaili, toka mikoani pia. Mbele kushoto ni mahali penye viti vya watu kusubiria. Kulia ni ofisi nyingine naelekezwa kule kwenye makontena ofisi ya chini..."kwani bro umetokea wapi", mimi nimezaliwa Morogoro, nimesoma hukohuko Morogoro, namjibu. "Halafu?" nikamjibu mbona maswali mengi ndugu yangu? "aaaahh kiswahili chako!!" nikamwambia naomba mwongozo kama nimekosea.

watoto waliwahi kuwa na vyweti? nikamjibu ndiyo, ila sio wote na hata wale wengine nimeelekezwa kuja kuvibadilisha, si mnatoa vipya? akajibu ndiyo.

Akanipeleka kwenye hili kontena la kwanza kabisa kwa "wa Mikoani" akaanza kupekua kwa alphabet, akakuta majina ya watoto wawili, "hii inawezekana" alijibu kwa haraka, ila itabidi urudi hapa baada ya wiki mbili. Nikamwambia bro sitaweza kwani ninaishi mbali kidogo, "wapi, mwanza?"kauliza. Hapana niko nje ya nchi hivyo sitaweza kuja ndani ya muda huo, kwani bei ni sh ngapi napaswa kulipa kwa cheti kimoja? Jibu lake lilinipa mashaka eti "kwa kuwa unatoka mbali, tena nje ya nchi, lipa elfu 30 kwa kila cheti halafu njoo chukua kesho asubuhi.....!! nikamuuliza vipi kuhusu huyu mdogo ambayo hakuwahi kuwa na cheti kabisa?....."huyo kazaliwa wapi.....hapahapa Dar? namjibu ndiyo. akaendelea "kwanini usilipe laki moja kabisa uje uchukue vyote, nikampa jina la huyo mdogo kwa ahadi ya kuja na picha zake kesho.....nani huyu tena ananivuta shati kwa nyuma?......Khadija Mzanzibari....hawa ni wezi wakubwa, unatakiwa ulipe sh 3500 tu kwa kila cheti,,,,acha nimuumbue.. nikamwambia hapana hebu mwache hadi mwisho wa huu mchezo..Nikamuuliza hivi ofisi za "Scorpion ni wapi-pale kwa Dr. Edward Hosea" Khadija hakuvumilia, " we kaka hebu njoo umfafanulie huyu baba, hajakuelewa vizuri.." akajibiwa kwa sasa niko busy aje kesho atakuta kila kitu tayari....katika uchunguzi wangu kwa wengine hakuna malipo hayo ya sh 30elfu wala nini.

Hayo yametokea leo.
 
Back
Top Bottom