Dar: Majambazi yapora na kuua

Dar: Majambazi yapora na kuua

Sijui tunakwenda wapi,
Hizo hela haziwezi kuwafikisha hata wiki moja watakuwa wamechacha tena
R.I.P

Hekima inatutaka tujiukiza kwanini haya yanatokea sasa kwa wingi. Na ikibidi tutatue tatizo
 
mungu amlaze marehemu mahali pema peponi, amen,
wametoa roho ya mtoto wa watu maskini, mungu atawalipa malipo mabaya kuliko hayo waliomfanyia mama wa watu,
 
Hiwa nashindwa kuelewa mentality ya majambazi. Kwani kumuibia huyo dada ilikuwa kuna haja ya kumuua? Wangempokonya tu hela wakamuacha hapo?
 
Mbona hali ilikuwa imetulia kila siku majambazi yamepora yameua, sasa kwanini yanaua?na hao polisi wako wapi wasiyakamate?
 
Majambazi yapora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi muda mchache uliopita na kutokomea kusikojulikana. Tukio hilo limetokea leo saa 11:16 jioni inavyosemekana mdada huyo alikua akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikua yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo
aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa.

Mpaka tunaingia mitamboni hakuna habari yoyote ya kukamatwa kwa wahalifu hao.

Kwa hisani ya audifacejackson blog
View attachment 92621
Picha hiyo hapo wakuu...R.I.P dada
 
Wizi ni mwendelezo wa yule roho wa mauti anaendelea kuwatesa wana wa mungu, tujitaidi kumwomba mungu kwa nguvu zaidi
 
Back
Top Bottom