Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 256
- 1,301
Matukio ya kihalifu yameanza kurejea tena kwenye baadhi ya mitaa ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa leo nitazungumzia yanayoendelea Kimara Korogwe, njia ya kuelekea KAM College kupitia mji mpya.
Ndani ya mwezi mmoja kuna watu wawili wamekatwa mapanga na vibaka wanaotumia bodaboda. Matukio haya yote yanahusisha wasichana, ambapo mmoja ilikuwa ni saa 12 jioni anatoka kazini kurudi nyumbani na tukio lingine limetokea wiki iliyopita saa 1 asubuhi mdada mwingine akiwa anaenda kazini.
Kinachofanyika kinasikitisha sana. Vijana hawa huja na boda wakiwa wamepakiana, na mara nyingi huendesha kwa kasi huku wakimpita mhusika kwenda mbele kukagua kama kuna watu, wakiona hakuna watu hurudi kwa kasi tena na kutoa panga kisha huanza kukata sehemu yoyote wayaoona inafaa.
Kwa visa hivi viwili, mmoja alikatwa taya nusu lidondoke na mwingine kakatwa mkono. Na baada ya kufanya hivi hubeba simu/mkoba wake na kutokomea nao kusikojulikana.
Kwenye tukio la wiki iliyopa, baada ya kukata mkono wa huyo dada waliendesha boda yao ya kasi sana kuelekea Maeneo ya Kimara Bucha huku wakifukuzwa na watu lakini bahati mbaya kutokana na ujenzi wa barabara unaoendeelea litokea gari katikati likaziba njia wakawa wamenusurika vinginevyo wangeuawa. Kumbuka, hii ilikuwa ni saa 1 asubuhi.
Kwasasa wananchi tumeanza kujilinda, tunaomba mamlaka za ulinzi zifike eneo hili kuimarisha ulinzi. Vinginevyo mkisikia tumeua hawa vibaka msije kutusumbua.
MKUU WA WILAYA ATOA NENO
JamiiForums imewasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Jacob Twange kuhusu hoja hiyo amesema “Hilo suala kwangu ni jipya, ndio nalisikia lakini kwa kuwa aliyezungumza ni Mwananchi na sisi Viongozi tupo kwa ajili ya Wananchi, basi saa mbili kutoka sasa, mimi pamoja na Viongozi wa Jeshi la Polisi Ubungo tutaelekea hapo.”
Ameongeza “Tutaenda kuonana na Serikali za Mtaa kisha tutazungumza na Wananchi tusikie maoni yao kujua kinachoendelea, hiyo itatusaidia kujua tunachukua hatua zipi za kuchukua.”

========================